Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
🤣🤣sasa hivi imebaki ya matangazo ya wizara ya afya kuhamasisha wasukuma wanaume kwenda cinik na wake zao
msituletee huo uchuro huku tarime
Fredy Bundala(Skywalker) now anamiliki online TV inaitwa Simulizi na Sauti...Kutoka hapo kwa uchache kabisa nawakumbuka
Ahmed Ally sasa yupo msimbazi
Baruan Muhuza na Ivona Kamutu (Azam)
Fredy Felix(Freduwaa) -RIP
Rahabu Frdedy (mke wa Freduwaa)sijui yuko wapi
Msabaha yule wa nyimbo za kikongo nadhani pia RIP
Mtani Wambura mzee wa lugha gongana
Kuna somebody Bundala sijui yuko wapi(michezo)
Anselim Tryphone Ngaiza (Soggy mzee wa vikombe huyu na wenzie wale wa hotpot family)
Ongezeeni list....
Mzee samadu Hassan ripKutoka hapo kwa uchache kabisa nawakumbuka
Ahmed Ally sasa yupo msimbazi
Baruan Muhuza na Ivona Kamutu (Azam)
Fredy Felix(Freduwaa) -RIP
Rahabu Frdedy (mke wa Freduwaa)sijui yuko wapi
Msabaha yule wa nyimbo za kikongo nadhani pia RIP
Mtani Wambura mzee wa lugha gongana
Kuna somebody Bundala sijui yuko wapi(michezo)
Anselim Tryphone Ngaiza (Soggy mzee wa vikombe huyu na wenzie wale wa hotpot family)
Ongezeeni list....
Rip Zuberi Msabaha, kweli nyakati zinakimbia sana.Dah kulikuwa na kitu anaitwa bolingo time
Jacob Marcus yuko wapi siku hizi?Mzee samadu Hassan rip
Jacob usungu
Deo kaji makomba(kwa sasa reporter wa dw)
Fatma shemweta
Husna mlanzi rip
Glory Robinson
Roy maganga
Prince baina kamukuru
Jacob Markus
Naona bado hawajajirekebisha kwenye hili, haswa upande wa TV.Wasikilizaji walipoanza kuona Radio Free Afrika ikipendelea upande mmoja wa kisiasa hasa Chama Tawala walipoteza imani na kituo hicho. Hali hii ilipelekea kupungua kwa idadi ya wasikilizaji, na kwa hivyo, kupungua kwa mapato yanayotokana na matangazo.
Du Samadu Hassan kumbe ka-RIP? alikuwa na sauti nzito flani sawa na Charles Machugu upande wa star tvMzee samadu Hassan rip
Jacob usungu
Deo kaji makomba(kwa sasa reporter wa dw)
Fatma shemweta
Husna mlanzi rip
Glory Robinson
Roy maganga
Prince baina kamukuru
Jacob Markus
Vyombo vya Habari vyenye mrengo wa kisiasa vinakufaUkizungumzia miongoni mwa vyombo vya Habari ambavyo vina uwekezaji mkubwa kwenye miundombinu naamini RFA kutoka Sahara Media itakuwa namba 1 kabisa. Radio hii imewahi kuwa na Watangazaji bora kuwahi kutokea na waliokuja kubadili kabisa sekta ya Utangazaji nchini.
Lakini Radio Free Afrika ilijikuta katika hali ngumu kutokana na wamiliki wake (Mbunge wa zamani na Waziri Anthony Diallo) kujiingiza kwenye siasa kwa kiasi kikubwa mno hadi kushindwa kuitenga media yake na Siasa.
Hali hii ilisababisha matatizo makubwa katika utendaji na uchumi wa kituo hicho. Hii ni hadithi ya jinsi kituo hiki maarufu cha habari kilivyoyumba:
Athari za Kujiingiza kwenye Siasa
1. Kugawanyika kwa Wafanyakazi: Wamiliki walipoanza kujihusisha na siasa, baadhi ya wafanyakazi walijikuta katika hali ya kukosa msimamo, huku wengine wakiwa na maoni tofauti kuhusu mwelekeo mpya wa kituo. Hii ilisababisha mgawanyiko na kushuka kwa morali miongoni mwa wafanyakazi.
2. Kupoteza Uaminifu wa Wasikilizaji: Wasikilizaji walipoanza kuona Radio Free Afrika ikipendelea upande mmoja wa kisiasa hasa Chama Tawala walipoteza imani na kituo hicho. Hali hii ilipelekea kupungua kwa idadi ya wasikilizaji, na kwa hivyo, kupungua kwa mapato yanayotokana na matangazo.
Ubaya zaidi ulikuja baada ya Diallo kutoka kwenye Ubunge na baadaye kutaka kurejea kwa kujipendekeza kwa hayati Magufuli. RFA ilitumika kufanya kampeni zote za Magufuli kwa ahadi kuwa akishinda atamkumbuka Diallo.
JPM hakutunza ahadi hiyo, hali ilizidi kuwa mbaya zaidi kwa Sahara Media hadi kiasi cha madai ya Wafanyakazi kufikia zaidi ya Tsh. Bilioni 5.
Matatizo ya Kiuchumi
1. Kushuka kwa Mapato: Pamoja na kupungua kwa wasikilizaji, matangazo ambayo ni chanzo kikubwa cha mapato kwa vituo vya redio yalipungua. Wafadhili na kampuni mbalimbali waliondoa matangazo yao kwa hofu ya kuhusishwa na siasa.
2. Mishahara ya Wafanyakazi: Matatizo ya kifedha yalisababisha kuchelewa au kushindwa kulipa mishahara ya wafanyakazi. Hali hii ilileta msukumo mkubwa kwa wafanyakazi ambao walikuwa tayari na hali ngumu kutokana na mgawanyiko wa kisiasa.
Kuondoka kwa Wafanyakazi
1. Kutoridhika na Mazingira ya Kazi: Wafanyakazi wengi walihisi kutoridhika na mazingira ya kazi kutokana na siasa kuingilia kazi zao za kila siku. Hii ilisababisha wengine kuacha kazi na kutafuta fursa nyingine ambako wanaweza kufanya kazi bila shinikizo la kisiasa.
2. Ukosefu wa Motisha: Kutolipwa kwa mishahara kwa wakati, pamoja na mgawanyiko wa ndani, kuliwakatisha tamaa wafanyakazi wengi. Hii ilisababisha kuacha kazi kwa baadhi ya wafanyakazi muhimu, hali iliyozidisha matatizo ya utendaji katika kituo.
Kwa ujumla, Radio Free Afrika ilijikuta katika mtego wa siasa ambao ulisababisha matatizo makubwa ya kifedha na kiutendaji. Ili kituo chochote cha habari kiwe na mafanikio, ni muhimu kudumisha usawa na kutoegemea upande wowote wa kisiasa ili kudumisha imani ya wasikilizaji na wafadhili.
Pia Soma: Radio Free Africa na waganga wa kienyeji
Kweli. Media yoyote kubwa nchini lazima kujiegesha kwenye siasa ili kufaidika na mfumo unaokuwa madarakani. Labda media changa au ndogo isiyo na jina kubwa ndiyo inaweza kuwa haina uchawa kisiasa lakini nayo ikishakuwa ugeuka chawa.Wewe lazima ulikua mfanyakazi RFA, ukweli ni kwamba Radio zote zimejaa siasa hapa Tanzania hazina vipindi vya kujenga vijana zaidi ya uchawa michezo na miziki, radio free Africa alibweteka sanaa ndo kushuka kwake.
🤣🤣🤣🤣🤣🤣sasa hivi imebaki ya matangazo ya wizara ya afya kuhamasisha wasukuma wanaume kwenda cinik na wake zao
msituletee huo uchuro huku tarime
Biashara ni watuWewe lazima ulikua mfanyakazi RFA, ukweli ni kwamba Radio zote zimejaa siasa hapa Tanzania hazina vipindi vya kujenga vijana zaidi ya uchawa michezo na miziki, radio free Africa alibweteka sanaa ndo kushuka kwake.