Jinsi Richard Branson alivyoanzisha kampuni ya ndege bila kuwa na mtaji wowote ule

Jinsi Richard Branson alivyoanzisha kampuni ya ndege bila kuwa na mtaji wowote ule

“Biashara Lengo huwa Sio ku TAKE Risk bali Lengo huwa ni ku MINIMIZE Risk”
Hii ina maana gani mkuu ielezee kidogo
 
Uzi wako mzuri ila wasomaji wako wajue kuwa Richard Branson alishakuwa na mawe ya kutosha kabla ya kuwa na wazo la kufungua kampuni ya ndege. Kufanya hizo movements za England - USA peke yake ni hela. Kabla ya kujiaminisha kuwa unaweza kuanza biashara kubwa bila mtaji anza na shughuli ndogondogo za kukupatia kipato. Mafanikio yana hatua nyingi sana ndogondogo. Kibongobongo ukipita njia ya Richard Branson unaweza kujikuta matatani na vyombo vya dola na ukaishia jela kwa kwa utapeli.
 
Na...

Jinsi Wewe Unavyoweza Kuanzisha Biashara yako pia!

Moja ya Changamoto ambayo Wajasiriamali wengi wamekuwa Wakipitia ni Jinsi ya Kuanzisha Biashara bila ya kuwa Mtaji.

Yaani…

Je kuna Njia yoyote RAHISI ya Kuanzisha Biashara bila kuwa na Mtaji?

Ukweli ni Kwamba…

HIYO NJIA IPO NA INAWEZEKANA!

Na…

Ili uweze Kunielewa Vizuri Nitakupa hii STORY ya kweli ya Billionea…

“Richard Branson”

Kama Humfahamu Tu…

Richard Branson ni Muanzilishi wa Kampuni ya…

“Virgin Group”

Yaani…

Kampuni Inayomiliki na Kuendesha Biashara Tofauti Tofauti ndani yake.

Mfano wake kwa hapa Tanzania ni Azam Group ambayo Ndani yake kuna…

Timu…

Media…

Hotels…

Usafirishaji…

n.k.

kwahiyo…

Hata Virgin Group nayo Ipo katika Mtindo huo ambapo Ndani yake ina Kampuni ya Ndege Inayoitwa…

“Virgin Atlantic Airways”

Kwahiyo…

Huo Ndio Utambulisho Mfupi wa Richard Branson…Story yake Inaendeleaje?

Angalia Hapa…

Mwaka 1984 Wakati Virgin Airways Inaanzishwa kulikuwa na Sheria moja ambayo Inasema Ili Uweze kuwa kwenye…

“Soko la Usafirishaji wa Anga kupitia Bahari ya Atlantic Ilikuwa ni Lazima Uwe na Ndege yenye Ukubwa at Least sawa na Boeing 747-200”

Yaani…

Kulikuwa kuna Vigezo inabidi Uvikidhi ili Uwe Tayari kuanza Kazi, Ikiwa pamoja na kuwa na Ndege ya aina hiyo.

Sasa kwa Kipindi hicho Branson alikuwa hawezi kwenda ku RISK Pesa zake kwenye Biashara Mpya ambayo Alikuwa hajua kama Itafanikiwa.

Na…

Kama tunavyofahamu Kwenye…

“Biashara Lengo huwa Sio ku TAKE Risk bali Lengo huwa ni ku MINIMIZE Risk”

Kwahiyo…

Branson ilibidi Atafute njia ambayo Itakuwa Salama kwake Kuanzisha Kampuni.

Na…

Kwasababu ukubwa wa Ndege Unaotakiwa ni sawa na wa BOEING 747-200. Kwa haraka haraka Ikabidi awacheki Kampuni husika…

Alivyoongea na Mtu wa Commercial Sales wa Boeing aliambiwa kuwa, Boeing huwa wana Sheria ya kuwa na Mteja Mmoja kwa kila Nchi…

Yaani…

Kampuni ya BOEING Huwa Inauza Ndege kwa Shirika Moja tu La ndege kwa Kila Nchi Duniani.

(Kwa Kipindi kile Sasa)

Na…

Alipokwepo Branson (England) Tayari Ilikwepo Kampuni ya Ndege ya…

“British Airways”

Kwahiyo…

Yeye alikuwa Hawezi Kuanzisha Biashara ya Ndege England kwa Kutumia Ndege za Boeing.

So,

Kisheria alikuwa HASTAHILI Kuanzisha kampuni ya ndege England.

Je Alifanyaje Branson hadi Kupata Ndege Kutoka kwenye Kampuni ya Boeing Japo Sheria Zilikuwa Haziruhusu?

Okay… Angalia Hapa

Baada ya Mauza Uza yote hayo Richard Branson Ikabidi Afike hadi Ofisi ya Boeing Nchini Marekani…

Alipofika Swali La Kwanza Aliwauliza…

“Vipi Mtakuwa na Ndege aina ya Boeing 747-200 ambayo Haitumiki/Iliyopaki?”

Mkurugenzi Akajibu… NDIO Ipo.

Richard Akauliza Tena…

“Vipi kama Moja ya Mashirika (Mteja) yenu Wangetaka Kukodisha hiyo Ndege, Je Wangelipia Kiasi gani kwa kila Mwezi?”

Mkurugenzi Akajibu tena… “Wangelipia kuanzia Dola 200,000 hadi Dola 300,000 kwa Mwezi”

Kumbuka hapo Richard Branson hana CASH ya Kuwapa…!

Sasa Angalia AKILI Aliyoicheza Richard Branson hadi Kuanzisha Kampuni ya Ndege huku Akiwa hana hata MIA Mbovu…

Kama unavyojua kwenye Usafiri wa Ndege huwa watu wana Tabia ya Kukata Ticket Mapema…

Mfano…

Mtu anaweza kuwa Anataka Kusafiri Mwezi wa 12 na Akakata Ticketi yake Mwezi wa 10, Maana yake…

Pesa Zinaingia kwanza Kabla ya Kufanya KAZI ya Kusafirisha Abiria.

Kwa Mjasiriamali na Benki zote Makini Duniani…

Unapompa Mtu PESA kwanza kabla ya Huduma, Yaani Unapolipa Advance huwa kuna Faida kwa Mjasiriamali au Benki Kuzungusha PESA na Kutengeneza Faida zaidi.

Kwahiyo…

Alichokifanya Richard Branson ni kwenda Kuiweka Kampuni ya Virgin Airways Sokoni huku Ikiwa haina Ndege Rasmi na Watu Wakaanza Kufanya Booking ya Ticket.

Baada ya Kulipwa Ticket za Mapema Ndipo alipokuja Kulipa KODI ya Ndege kwenye Kampuni La Boeing.

Then Guess What?..

Huo ndio Ukawa Mwanzo wa Kampuni ya Ndege ya VIRGIN AIRWAYS Unayoijua Leo hii.

Kwahiyo…

Ki Msingi Tunasema Richard Branson Aliweza Kuanzia Kampuni ya Ndege Akiwa hana hata Dolla Moja Mfukoni.

Sasa wewe kama…

Mjasiriamali wa Kibongo Unawezaje Kuanzisha Biashara bila kuwa na Mtaji wowote Ule?

Kama Ninavyopenda Kusema Kwamba…

Kila ninapokuwa Nataka Kufanya Kitu flani huwa Najiambia kuwa Kuna MILLIONS of ways za Kufanya hicho Kitu.

Kazi yangu ni Kuchagua Njia gani ni Sahihi zaidi na Ina RISK ndogo baada ya Muda.

Na…

Kwenye hiki Kitu tutaenda Kutumia Njia hiyo hiyo…

Sasa hapa Sitakupa Majibu ya Moja kwa Moja Unawezaje Kuanzisha Biashara Bila kuwa na Mtaji kabisa kama Richard Branson…

ILA…

Nitaenda Kukuonesha NJIA Ambazo Unaweza Kutumia Kupata Pesa kwaajili ya Kuanzisha Biashara yako.

Kwahiyo…

Kama umependa MODEL ya Richard Branson Unaweza Kuitumia na Ukaanza Safari yako…

ILA…

Kama hiyo Model Huiwezi basi Ishi na hizi NJIA Ambazo Zinaweza Kukupa Pesa ya Mtaji.

1). Raise Capital Kutoka kwa Watu au Investors

Hii ndio OLD SCHOOL Model ya Kupata Mtaji Mkubwa ambayo Imekuwa Ikitumiwa Miaka na Miaka.

Hapa unachohitajika ni uwe Umesajili Kampuni au Biashara yako kisha Unatafuta watu wa Kukupa Fund (Pesa)

Yaani…

Unauza baadhi ya Vipande vya Biashara yako (Hisa) kwa Watu watakao kuwa Tayari.

Zaidi Unachohitaji Hapa ni…

Uwe Unajua Kitu Unachokifanya na IDEA yako iwe Sustainable. Tofauti na hapo UTACHOMA Biashara yako na Pesa za watu.

Na…

Hii Mbinu Nimeona Ikitumika Mara ya Kwanza…

Miaka ya Nyuma kwenye Kampuni moja aidha La Cement au Benki kama Sijasahau.

Yaani…

Walikuwa wanapita Kule Kijijini kwetu Shelui na Walikuwa Wanauza HISA zao kwa Watu waliokuwa Interested.

Na…

Kuna Mzee Mmoja Maarufu sana pale Alinunua ambapo hadi Leo huwa anakula Gawio lake.

Sehemu ya pili Nimeshuhudia Ilikuwa Chuo…

Kuna Rafiki yangu Mmoja yeye ana Kampuni yake ya Kilimo na Alikuwa anauza Hisa zake kwa Wanafunzi.

Alikuwa anaitisha Mkutano anafanya Presentation ya IDEA yake Then watu Wananunua Hisa.

Na…

Kila mwisho wa Mwaka anatoa GAWIO kwa Wanahisa wake.

Kwahiyo…

Hiyo ndio Njia ya kwanza Unaweza Kuitumia Kupata Mtaji wa Kuanzia.

TAHADHARI: Kabla ya Kufanya hiki Kitu hakikisha Unafuata Utaratibu wa ki Sheria otherwise Unawezakuta Unafanya Utapeli. Hakikisha Unawaona Wataalamu.

2). Fanya Partnership na Watu wenye Pesa.

Kama una Idea na una Imani kwamba Inaweza kuwa ni GREAT Business basi Usiogope Kutafuta Partners.

Faida ya Partners ni kwamba Watakupa…

“SYNERGIC EFFECT”

Yaani…

Wewe bila wao Huwezi kwenda na Wao bila Wewe Hawawezi kwenda.

Sawa na ki Hesabu kwamba… 1 + 1 = 3

Maana yake ni kwamba Biashara inakuwa na NGUVU kama Mkiwa wote kuliko Ukiwa Pekee yako.

Kwahiyo…

Hapa unatafuta watu ambao Unajua wana PESA na Hawajui Wazifanyie nini na Wewe mwenye IDEA ambayo Hujui Uipeleke wapi.

Hapa Ongea na Washikaji zako, Ndugu zako, School Mates then Wekeni Makubaliano. Then Here We Go. SIMPLE

Hapa Unatakiwa uwe Vizuri kwenye USHAWISHI Tofauti na hapo Huwezipata Kitu.

3). Tafuta MKOPO Usio na Riba.

Yeah… Sijakosea!

Tafuta mahala ambapo Utakopeshwa Bila Riba na Bila Masharti Magumu ya Muda wa Kurudisha.

Bila shaka Kila Mtu anaishi Mtaa au Mazingira ya Karibu na Watu wanaojiweza…Ongea nao then Waeleze Future yako.

Nenda nyumba yoyote ya Mfanyabiashara Mkubwa then Mwambie PLANS na Kila kitu unachotaka Kukifanya.

Wengi ni Waelewa na Wameshakuwa huko…Anaweza Kukukopesha Bila Riba hasa akikuona una Future ya maana.

Ikishindikana…

Ongea na Ndugu yoyote mwenye KIPATO ambaye ana Ajira. Mtafute face to face Uongee nae.

Nimesema Mkobo Usio na Riba Kwasababu…

Biashara Sio STRAIGHT LINE kama Ajira. Sio kila kitu kitakuwa sawa hasa Pindi Utakapoanza.

Kwahiyo…

Kama utakopa kwenye Mikopo Kausha DAMU Itakuwa ni Rahisi Kupoteza…

Kwasababu…

Kelele na Miluzi Itakuwa kibao MIXER Marejesho ya kila Wiki…Probably Lazima Utauwa Biashara yako.

So…

Hiyo ndio Summary Fupi ya Kupata MTAJI wa Kuanza Biashara.

Kilichobaki ni Uthubutu wako na Ujuzi Kuhusu Kitu Unachoenda Kukifanya.

…THAT’S ALL GUYS!

I Hope huu ujumbe kuna Mtu unamuokoa huko Njee.

All the Best…

Uwe na Siku Njema.

SN: Story ya Richard Branson Nimeikata na Nimeiweka ili Ifikishe huu Ujumbe Kwahiyo Ukienda Kuisoma au Kuisikiliza Mahali Unaweza Kujifunza zaidi.

Seif Mselem!
Kuna aya umesema "Alichokifanya Richard Branson ni kwenda Kuiweka Kampuni ya Virgin Airways Sokoni huku Ikiwa haina Ndege Rasmi na Watu Wakaanza Kufanya Booking ya Ticket"

Naomba ueleze aliweza vipi kusajiri hio kampuni na kuuza tickets bila kukidhi matakwa ya mamlaka ya usafiri wa anga yaliyomtaka awe na ndege kwanza.
 
Uzi bora, mpangilio mzuri wa kujenga hoja, mtiririko mzuri usiochosha..wa kujifunza hakosi cha kujifunza,wa kupuuza pia hawakosekani but who cares,kwanza hatulipii wazo lako.
 
Unajua maana ya Mtaji ?

Mtaji sio pesa hata convincing power, appearance kupiga sound na wewe mwenyewe pia ni mtaji..., Richard baada ya kuwa na Virgin (aliyoanzisha kwa kuuza CD) na Salesmanship yake ni mtaji tosha..., yote aliyofanya yeye angeenda kapuku mwingine huenda asifanikiwe....

Na kwa taarifa yako watu wengi kwenye biashara wanatumia other people's money kufanikisha mambo yao wala sio pesa yao (wanauza idea au potential ya faida kwa muwekezaji)
 
Rudia kusoma vizuri, kasema inakodishwa kwa dola 200,000 kwa mwezi. Na inawezekana, Boeing 747 zina hadi seat 500. Kwa trip moja kila abilia akilipa dola 200 tu, ni sawa na 500 x 200 = 100,000. Dola laki 1, hiyo ni trip moja tu. Sasa kwa mwezi hiyo ndege ikikodishwa kwa dola laki 2 ugumu uko wapi!?..
Shukrani kwa kunisaidia kwenye hili Kiongozi. Shida yetu sisi WABONGO ni Exposure tu.
 
Rudia kusoma vizuri, kasema inakodishwa kwa dola 200,000 kwa mwezi. Na inawezekana, Boeing 747 zina hadi seat 500. Kwa trip moja kila abilia akilipa dola 200 tu, ni sawa na 500 x 200 = 100,000. Dola laki 1, hiyo ni trip moja tu. Sasa kwa mwezi hiyo ndege ikikodishwa kwa dola laki 2 ugumu uko wapi!?..
I got it right, that's why I asked. Didn't mean I want to debate
 
Umesema hakuwa hata na mia mfukoni halafu hapo hapo anamiliki kampuni ya usafirishaji wa anga ya Virgin airways 😀 kitendo tu cha kumiliki kampuni ya usafirishaji tena kwa anga/ndege, huyo tayari ni wa kishua vibaya mno! Hao Boeing wenyewe mpaka wakukodishie ndege yao kwa mwezi mzima maana yake una Mortgage/Pesa ndefu ya kishika uchumba! Ila nice try, Nice motivation.
 
Kama umesafiri na ndege utagundua sheria za Aviation ni kali sana,tofauti na basi. Lazima wajue uwezo wako wa kuwabadilishia ndege abiria moja ikikwama, mikataba ya muundaji wa ndege na guarantee yake, Kuna masaa (life span ya ndege yakifika isitumike tena), na vigezo vingi. hadi unaona wamerank Singapore namba 1,Qatar 2 ,Emirate 3, jua imefanyika kazi.
 
Back
Top Bottom