Jinsi Richard Branson alivyoanzisha kampuni ya ndege bila kuwa na mtaji wowote ule

“Biashara Lengo huwa Sio ku TAKE Risk bali Lengo huwa ni ku MINIMIZE Risk”
Hii ina maana gani mkuu ielezee kidogo
 
Uzi wako mzuri ila wasomaji wako wajue kuwa Richard Branson alishakuwa na mawe ya kutosha kabla ya kuwa na wazo la kufungua kampuni ya ndege. Kufanya hizo movements za England - USA peke yake ni hela. Kabla ya kujiaminisha kuwa unaweza kuanza biashara kubwa bila mtaji anza na shughuli ndogondogo za kukupatia kipato. Mafanikio yana hatua nyingi sana ndogondogo. Kibongobongo ukipita njia ya Richard Branson unaweza kujikuta matatani na vyombo vya dola na ukaishia jela kwa kwa utapeli.
 
Kuna aya umesema "Alichokifanya Richard Branson ni kwenda Kuiweka Kampuni ya Virgin Airways Sokoni huku Ikiwa haina Ndege Rasmi na Watu Wakaanza Kufanya Booking ya Ticket"

Naomba ueleze aliweza vipi kusajiri hio kampuni na kuuza tickets bila kukidhi matakwa ya mamlaka ya usafiri wa anga yaliyomtaka awe na ndege kwanza.
 
Uzi bora, mpangilio mzuri wa kujenga hoja, mtiririko mzuri usiochosha..wa kujifunza hakosi cha kujifunza,wa kupuuza pia hawakosekani but who cares,kwanza hatulipii wazo lako.
 
Unajua maana ya Mtaji ?

Mtaji sio pesa hata convincing power, appearance kupiga sound na wewe mwenyewe pia ni mtaji..., Richard baada ya kuwa na Virgin (aliyoanzisha kwa kuuza CD) na Salesmanship yake ni mtaji tosha..., yote aliyofanya yeye angeenda kapuku mwingine huenda asifanikiwe....

Na kwa taarifa yako watu wengi kwenye biashara wanatumia other people's money kufanikisha mambo yao wala sio pesa yao (wanauza idea au potential ya faida kwa muwekezaji)
 
Shukrani kwa kunisaidia kwenye hili Kiongozi. Shida yetu sisi WABONGO ni Exposure tu.
 
I got it right, that's why I asked. Didn't mean I want to debate
 
Umesema hakuwa hata na mia mfukoni halafu hapo hapo anamiliki kampuni ya usafirishaji wa anga ya Virgin airways 😀 kitendo tu cha kumiliki kampuni ya usafirishaji tena kwa anga/ndege, huyo tayari ni wa kishua vibaya mno! Hao Boeing wenyewe mpaka wakukodishie ndege yao kwa mwezi mzima maana yake una Mortgage/Pesa ndefu ya kishika uchumba! Ila nice try, Nice motivation.
 
Kama umesafiri na ndege utagundua sheria za Aviation ni kali sana,tofauti na basi. Lazima wajue uwezo wako wa kuwabadilishia ndege abiria moja ikikwama, mikataba ya muundaji wa ndege na guarantee yake, Kuna masaa (life span ya ndege yakifika isitumike tena), na vigezo vingi. hadi unaona wamerank Singapore namba 1,Qatar 2 ,Emirate 3, jua imefanyika kazi.
 
Kwa hiyo mkuu wewe ukiwa na Exposure unaweza kwenda Boeing ukawaambia unataka Boeing 757 una kampuni yako ya ndege unaanzisha alafu wakakupa tu kirahisi rahisi? 😀
Watacheka mpaka machozi yabubujike kama yule shumileta luka....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…