Jinsi TFF ilivyoamua kumuonea hadharani Feitoto na kuwatumikia Yanga Ni dhahiri zile ni hisia za bahasha kwenye ligi yetu

Jinsi TFF ilivyoamua kumuonea hadharani Feitoto na kuwatumikia Yanga Ni dhahiri zile ni hisia za bahasha kwenye ligi yetu

Wewe ni mpumbavu sana......unajua kwanini?.....Yaani mchezaji aamke asubuhi arudishe pesa aandike barua,aondoke kambini,sense uarabuni useme kavunja mkataba?…........hata Morrison na uchizi wake hakufanya ujinga Kama wa Fei.......hata akienda mahakama ya uhalifu fei atashindwa tu......hakuna Mambo ya kihuni yatakayo kuwa entertained Kama yanayofanywa na fei.........la msingi vumilia sense FIFA cas baada ya hapo utaehuhudia jinsi fei atavyoadhibiwa

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Sio kila kitu ni cha kukaa na mwajir, mnapenda sana reference ya onyangoy,, ngja aende CAS atakapo waumbua yanga na TFf yenu..suala hili limetatuliwa kisasa tu, huku sheria zikiwekwa pembeni.. kwanini hadi Leo hakuna ufafanuz wa kisheria... Mpira ni biashara huwez kulazimisha patnership katika biashara Kama maridhiano hayapo..fei aliweka wazi kipengeëele alichotumia,, hao tifutifu wameweka vipengeële walivyotumia?? Badala ya kutoa ufafanuzi kisheria wanafanya media tour kweli??

Uliwah kuona wapi hakimu anamfunga mtuhumiwa bila kutumia vifungu vya sheria.. au anamfunga Halfu anasema siku fulani atakuja kutoa ufafanuzi kwanini nimemfunga...?

CaS Dogo atapta haki yake htakama itaamliwa Bado ni mali ya yanga lkan hukumu yake itatoa mwelekeo Nini fei anatakiwa kufanya kuondoka ynga.. sio hao tifutifu wamekalia stor za vijiweni na za wanasiasa..
Wajinga wengi nchi hii, kila mchezaji aibuke anataka kuvunja mkataba huo mpira utachezwa kweli?
 
Wajinga wengi nchi hii, kila mchezaji aibuke anataka kuvunja mkataba huo mpira utachezwa kweli?
Hakuna kitu kidichovunjika.. cha msingi utimize kukivunja suala la kukaa na mwajir wako sio lazma.. yeye unampa taarifa Kwa mujibu wa mkataba..sio kila mtu anatka kuvunja mkataba...wengine wamerudhika na mazingira yao
 
Hakuna kitu kidichovunjika.. cha msingi utimize kukivunja suala la kukaa na mwajir wako sio lazma.. yeye unampa taarifa Kwa mujibu wa mkataba..sio kila mtu anatka kuvunja mkataba...wengine wamerudhika na mazingira yao
Acha ujuaji wa kijinga mchezaji hua ni mali ya club kwa maana nyingine mchezaji ni asset ya timu thamani ya club ni pamoja na mikataba ya wachezaji ndio maana ni kwenye michezo pekee mtu analipwa signing fee au ana nunuliwa kutoka timu nyingine niambie ni professional gani ambayo mtu ana pewa signing fee au kuuzwa kwenda kampuni nyingine? ukipata jibu hapo ujue Feisal ni mjinga kama wewe
 
1. Walianza na barua ya kingereza iliyomtoa uarabuni kwenye program zake wakitaka aje bila kubainisha makosa aliyoshitakiwa nayo ili awe tayari kuandaa utetezi wake. Barua ilikuwa fupi sana. Na kikubwa swala Hilo Feitoto angeweza kulijibu kwa maandishi tu bila kuwepo Sababu Ni la kimkataba. Lkn wanalazimisha arudi.

2. Wakaja na maamuzi yaliyo upande wa Yanga bila kushirikisha wapi Feitoto alikosea. Wakasema ufafanuzi Jana. Lkn maamuzi walishirikisha kwenye vyombo vya habari.

3. Jana hawakutoa ufafanuzi Bali Tuzo zilizoegemea Simba ili kuwazima washabiki wa Simba wanaofatilia swala la Feitoto.

Tff wanajua muda wa dirisha dogo Ni mfupi. Wanajua umuhimu wa uamuzi wa haraka kwa Feitoto kuliko Yanga. Dogo anatakiwa apate timu Kama akishinda. Kutotoa ufafanuzi tu baada ya masaa 72 baada ya hukumu kutolewa kunamyima fursa Feitoto kutafuta haki akiona ameonewa.


Hii Ni roho mbaya Kama sio ushetani. Toka hukumu ya Feitoto itolewe hakuna ata mwanasheria moja wa soka aliyeweza kuja kufafanua Ni vipengere vipi ambavyo vilimbana fei asivunje mkataba wake bila sababu wakati mkataba wake ulikuwa na vipengere hivyo.

Zaidi utasikia oh "mkataba hauvunjwi kihuni".

Fei aliweka kipengere Cha kuvunja mkataba bila Sababu kwa kulipa tsh m 100. (Nakumbusha bila Sababu) na mishahara mitatu.

Tulitegemea Tff ije iseme hakuna kipengere hicho kwenye mkataba wa Feitoto au itoe tafsiri ya hicho kipengere.

Kuvunja kwa Sababu zilizoanishwa na FIFA fei asingelipa chochote.. ikiwa Ni pamoja na kutolipwa mshahara au kukaa benchi 90% ya muda kwa mechi kumi bila sababu

Msitumie tuzo kwa Mgunda na Chama kuzima kimya kimya Swala la Feitoto.

Mliwapa muda kijanja Yanga wa kumrudisha bongo Feitoto ili wapate na gepu waongee nae. Nazani imeshindikana.

Ni muda Sasa wa swala lake kuwa wazi tu.
Na nyinyi muache kulialia bila ya sababu za msingi. Kama hamjaridhika na hayo maamuzi, nendeni mkaungane na lile jopo la mawakili wake, mkate rufaa ngazi zinazofuata.
 
Acha ujuaji wa kijinga mchezaji hua ni mali ya club kwa maana nyingine mchezaji ni asset ya timu thamani ya club ni pamoja na mikataba ya wachezaji ndio maana ni kwenye michezo pekee mtu analipwa signing fee au ana nunuliwa kutoka timu nyingine niambie ni professional gani ambayo mtu ana pewa signing fee au kuuzwa kwenda kampuni nyingine? ukipata jibu hapo ujue Feisal ni mjinga kama wewe
Profesional Ziko nyingi tu ambazo mtu anashift kutokana na ujuzu wake au talenti yake..so hio haiapply tu kwenye michezo ndg...hta kwenye kada zingne hicho kitu Kipo..tatizo umezaliwa sigimbi na unaishi sigimbi sasa unajua tu kwenye michezo tu.. kampuni kubwa Dunian zikimtaka mtu fulani, wanaongea na kampuni yake wanachumkua. Au wanaongea namna ya kumalizana
 
Fei ni mpumbavu , hata kama kuna upenyo huo wa kuvunja mkataba , ni kuwakosea Yanga , tujiulize Yanga wamemkosea nn Fesal? Kulikuwa na malumbano yoyote?

Kama kulikuwa hamna shida kulikuwa na haja gani ya kuwatoroka....ikumbukwe mpira ni biashara , mchezaji anapopanda thaman , na ikatokea timu ikamhitaji tunatarajia mchezaji kulipwa vizur timu atakayokwenda ( hii ni faida Kwa mchezaji) , na pia timu anayotoka ambayo kimsingi ndo imempandisha thamani na wenyewe wapate.

Sasa yeye anatoroka kupitia mlango wa nyuma , timu ibaki haina kitu , ni Ujinga mkubwa Sana huo , dogo hafai hata kidogo , na hili ni tatizo la elimu duni Kwa hawa vijana ,

Yalianzia kwenye mziki akina harmonize, Ray-vanny (yaan wanataka wachukue chote) na sasa yameanza kwenye mpira
Huyu dogo anakwenda kukiharibia carrier yake kwa ujinga wake na wale walio nyuma yake.
 
Kijana wa watu anashauriwa na watu ambao hawana hekima wala huruma. Unapokutana na mambo madogo kama haya halafu unaona watu wanatumia the hard way kutafuta ufumbuzi ndipo hapo unagundua sio kila mtu anaweza kuwa kiongozi.
Watu wazima wamwambie tu Feisal arudi Yanga na muda si mrefu watamwuuza kuliko njia ya hovyo anayotaka kupita. Wengi wanaoshabikia hapa hawajui vifungu vilivyomo kwenye mkataba zaidi ya kukariri ile mistari miwili ambayo ni sehemu tu ya mkataba wenye page zaidi ya tano. Kwenda CAS ni matumizi mabaya ya akili na fedha kwasababu Feisal akitayarishiwa statement fupi tu na mtu mwenye akili Yanga watasema mwacheni mtoto wetu aende akatafute maisha. Lakini yeye anatunisha misuli jambo ambalo hata akishinda kesi huko CAS bado yeye ndiye victim. Kuna watu wazima wa kimpira kama akina Ragge, Tenga etc wanaweza kumsaidi kuliko hawa wengine ambao hawajui chochote cha maana. Ajifunze somo kidogo kwa Morisson ambaye aliondoka Yanga kwa kesi lakini leo hao hao ndio waajiri wake. Feisal ni kijana mtanzania ambae tungetamani alisaidie Taifa akiwa mchezaji na hata baada ya kustaafu. Wrong choice ndizo zimewafanya baadhi ya watu wafanikiwe na wengine kushindwa vibaya.
 
Back
Top Bottom