Mwamuzi wa Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 15,486
- 45,256
Habari,
Nimetumia nafsi ya kwanza si kwamba Mimi ni trafiki , hapana bali nawasilisha mazungumzo tu niliyofanya na rafiki yangu mmoja ambaye sasa kahamia Trafiki kutoka kwenye kitengo kingine cha kipolisi hapahapa jijini Dar es salaam.
Huyu kijana ambaye anapenda sana maisha ya starehe alijikuta akiishi maisha magumu licha ya kuwa mtumishi wa umma anayelipwa mshahara na posho kama 2 hivi kwa mwezi.
Madeni kwake hayaishi, hayo ndio maisha yake kabla hajaukwaa utrafiki.
Mpaka mkewe ambaye ni Askari wa Magereza alimkimbia.
Majuzi aliacha lindo kidogo baada ya jamu kupungua ndipo tulipokutana.
Nikamuuliza hii gari ni yako ? Nilimuuliza hivyo kwakuwa najua huyu chalii akipata pesa suala la kuazima au kukodi gari kwaajili ya misele ilikuwa ndio kazi yake.
Akasema it's mine nimenunua kwa kufanya installment yaani alikuwa akilipa mdogo mdogo yard mpaka kamaliza pesa yote Ml. Kumi na ushehe ndani ya miezi kadhaa.
Akasema kuwa usiidharau ile elfu 2 ninayopewa na konda, kwa siku sikosi laki mbili mpaka Tano.
Alisema kuwa wanahakikisha kila daladala inayopita kituo chao inachajiwa 2000 mara moja kwa siku , na wanachokifanya ni kugawanya daladala (yaani zamu zamu) na si kugawanya pesa. Unachokipata ni chako na boss wako utaenda kumpooza baadaye.
Sasa jamaa haishi kwa madeni, mke wake karudiana naye na ana mpango wa kuanza kujenga.
Kuna mambo mengi ya hovyo yanafanywa na madereva wa daladala pamoja na Makonda wao kwa abiria kwakuwa matrafiki wamewageuza kuwa chuma ulete basi huwabeba . Labda wafanye makosa makubwa ndipo watashikwa.