Tatizo la Rushwa Kwa nchi za Kiafrika ni kubwa na ni la kudumu. Katiba za Nchi za Kiafrika ni Mfadhili mkubwa wa Rushwa, wizi, uhuni na ufisadi wa kila aina. Katiba za Nchi nyingi za Kiafrika ni za kutawala kijeshi. Tatizo kubwa ni Tawala za Kiraia zinazotumia katiba za Kidikteta.
Raia we anaotawala kidikteta Kwa Katiba za Kijeshi mara nyingi wanatumia mwanya huo kushirikiana na kupora Mali za umma au kujihalalishia rushwa kwenye mifumo yote.
Hapa Tanzania ni Polisi tu ndio wananyooshewa sana vidole kutokana na kukutana na wananchi kila linapotokea jambo liwe la amani au Vinginevyo. Matokeo yake idara nyingine zimejichimbia na kuchota mabilioni ya fedha za umma ambazo tayari zimeshaingia kwenye mfumo wa hazina. Miradi isiyokidhi, malipo hewa ,vikao visivyoisha n.k. Nchi inayoongozwa Kijeshi haipaswi kuwa na matumizi Mengi badala ya maendeleo. Na vikao vinaweza kuwa ni Moja ya majukumu sio suala la kulipana pesa za miradi.
Leo hii akitokea Polisi asiyependa Rushwa halafu akastaafu Hana nyumba ,gari,hajasomesha watoto shule angalau nzuri, hajasomesha wadogo zake n.k. ataitwa mjinga na atasemwa na kutukanwa kuwa ana maisha magumu Kwa sababu ya laana za watu na atasemwa kuwa alikua hatendi haki ndio maana laana zimemfuata kumbe huyo ndiye aliyekuwa muadilifu.
Lakini kijana akitoka Chuo ha Polisi halafu Kwa mwaka mmoja akawa na nyumba ,gari, na matanuzi makubwa atasifiwa na kuonekana mjanja na anayejiandaa kustaafu vizuri. Hakuna anayeuliza kuwa mwenzetu umepata wapi Mapesa ya kujenga majumba ndani ya mwaka mmoja na kamshahara kadogo kama posho ya kikao kimoja Cha Mbunge.
Kama hatuna Sheria Kali ya maadili na kutaja Mali za viongozi na watumishi Kwa wazi ,rushwa itaondolewa na mtu kuamua Mwenyewe kukataa rushwa kulingana na Imani yake ya dini lakini sio mfumo wa kisheria na Kikatiba na usimamizi.
Vinginevyo ni lazima nchi za Afrika waweke mifumo Bora ya Kikatiba inayoweza kuchunguza Mali za watumishi wa umma na upatikanaji wake kuanzia juu mpaka chini.
Rwanda wamejitahidi sana. Tawala za Kijeshi ni sukuhisho Kwa nchi za Kiafrika Kwa nchi zenye urais wa kifalme na katiba za kifashist.
Uganda Idd amini alipindua nchi bila kumwaga damu na akarudisha nchi Kwa wengi na kuwatimua wanyonyaji na mawakala wao waliojivika jezi za kisiasa na udisadi kila mahali. Iddi Amini angeitwala Uganda Kwa Miaka 40 angefanya Uganda kuwa kama Lybya. Hata hivyo baada ya Iddi Amini kupinduliwa na nchi jirani Kwa kumwaga damu ni bahati Tena Nchi Korofi Kama Uganda kumpata shujaa Mwingine wa vita aliyeingia Kwa kumwaga damu za Mafisadi na kuitwaa nchi yaani Kaguta Yoweri Museveni. Nchi za Afrika zinapaswa kutawaliwa kidikteta na Kijeshi Kwa Miaka 20 mfululizo chini ya Katiba za Kikoloni.