Super Don
JF-Expert Member
- Dec 10, 2016
- 1,978
- 1,781
Tanzania ni moja ukiwa zanzibar it means upo tanzania so upo kwenuKila sehemu kuna mila, taratibu, desturi, tamaduni, silka zake. Zanzibar ilitawaliwa na waarabu na kwa asilimia 99 ya wazanzibari ni waislam. Kama sikosei walitaka kujiunga na OIC miaka ya nyuma huko kitu ambacho kingeitambulisha Zanzibar kama taifa la Kiislam. Muungano wa Zanzibar na Bara ndio uliosababisha hadi leo hii Zanzibar kukwama kuwa taifa la Kiislam. Hivyo basi kulingana na maelezo hayo mafupi utaona ni jinsi gani Zanzibar ilivyo. Hivyo basi wapo Wakristo ambao nao pia wamezaliwa na kukulia Zanzibar lakini wanafuata mila, taratibu, desturi, tamaduni, silka za kizanzibar. Sasa basi ikiwa umekwenda ugenini kwa watu jaribu sana kuelewa ni kipi wenyeji wako wanapenda na kipi hawapendi ili kuweza kuendana na sehemu husika na sio kutaka kufanya vile unavyoona kwako inafaa wakati huo huo ukiwaudhi wenyeji wako.
Kama ukiona unashindwa au unanyanyasika unaweza kurudi nyumbani kwa maana hujafukuzwa. Lakini pia kwanini uteseke na una kwenu? Vile vile kuharibika kwa mila, taratibu, desturi, tamaduni, silka za kwenu kusisababishe ukataka na ugenini kwako kuwe hivyo hivyo.
Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app