kokudo
JF-Expert Member
- Oct 26, 2010
- 2,571
- 1,760
Mpaka linafika linakuwa na bei ganiKwenye balo la kg 100 unaweza pata blouse 600-750
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mpaka linafika linakuwa na bei ganiKwenye balo la kg 100 unaweza pata blouse 600-750
Bonge LA MadaHello wana bodi, natumai wote mko poa karibuni kwenye hii thread ambayo kwa namna 1 au nyingine inaweza kukupa idea ya kufanya biashara ya kuuza mtumba:
A. SIFA ZA MTUMBA WA CHINA
Belo za mtumba wa China uko vzuri na unatofautiana Kati ya supplier na supplier na wao wana chukua nguo Asia karibia yote then wanapeleka kiwandani wanauchakata baada ya hapo ndipo wanaanza kusupply kwa Wateja wao. Kuna wauzaji wengine wanagoma kabisa kuchanganya nguo kwenye balo moja mfano sijui blouse, nguo za watoto, jeans, T-shirt n.k na masherti yao ni lazima uagize kuanzia belo la KG 100 kwenda juu japo wengi wanahitaji uchukue kontena zima but kuna wachina wengi tu wanakubali kuanzia kg 100, 200, 300 et al.
JINSI YA KUAGIZA MTUMBA TOKA CHINA;
1. ANZA KWA KUDOWNLOAD APP INAYOITWA ALIBABA KAMA UNATUMIA ANDROID PHONE NENDA GOOGLE PLAY STORE, THEN JISAJILI KWA KUWEKA NAMBA YA SIMU AU GMAIL.
2. TAFUTA SHIPPING AGENT (MAWAKALA WA USAFIRISHAJI MIZIGO TOKA CHINA KUJA TANZANIA KWA MELI)
Hapa nakazia ndipo wengi wanafeli.. Kwanza kabisa kuna agents wengi nowadays kama Chief Izamwa, Silent Ocean, Mapembelo Cargo, Tosh Cargo, GNM cargo na wengineo, hivyo nenda Instagram utapata mawasiliano nao na ndipo watakupa address yao ya China ambayo utamrushia supplier wako ili apeleke mzigo kwao na hao agents watasafirisha mizigo yako hadi Tanzania pamoja na kufanya clearance ( watakulipia ushuru bandarini ) so wewe utaenda tu kwa warehouses zao kulipia na kuchukua mzigo wako bila Shida.
NB 1: Hapa na recommend SILENT OCEAN kwani wana app inayotrack mitumba yako itafika lini na unajua kabisa utalipia shilling ngapi kabla hata mizigo yako haujaipata.
NB 2: Mizigo kwa sasa inachelewa kufika ko itabid uwe mvumilivu kwani inachukua hadi miezi 2 sababu ya UVIKO. Pia usijiroge kusafirisha kwa ndege utajuta gharama za usafiri.
3. Fungua Airtel MasterCard kwani hii ndio iko fasta kuliko voda but sijajua kwa banks na mitandao mingine inakuwaje. Hii MasterCard itakuwezesha kumlipa mchina ili sundae mzigo wako ndani ya siku mbili hadi nne then atapeleka kwa shipping agent wako. Ukishalipia omba kwa mchina aandike jina lako pamoja na namba za simu ili mzgo usije potea Tanzania kwani mizigo inakua mingi mingi
4. BEI YA MTUMBA WA CHINA
Beii wapendwa zinatofautiana kwani hutegemea grade A, B hadi C. pia aina ya nguo unazohitaji na supplier uliyemchagua. Ila grade A maximum ni 600000 (laki sita) na usafiri makadirio ni 20000 ( laki mbili) kwa belo la KG 100 ambapo return yake hapo ni kuanzia 1800000 (milioni na laki nane) hadi 2000000 (milioni mbili kamili) inategemea na location uliyopo.
5. JINSI YA KUONGEA NA WACHINA
Kwanza inatakiwa ujue ngeli hta ya kuibia ibia tu, then utengeneze urafiki hapo mchina atakukubali hadi bei atakupunguzia
BAADHI YA NAMBA ZA WACHINA WANAOUZA MTUMBA
+8617888279050, +86-15917348531, +86 177 1568 6510,+86 151 7342 7075 ( Hizo namba ni za WhatsApp afu ni watoto wa kike, pisi Kali hatarii)
Pia ukishadownoload ALIBABA APP search neno hili "SECOND HAND CLOTHES IN BALES"
Pia unaweza kusearch Alibaba neno kama GRACER NA ZAGUMI nao wanamtumba mzuri hatari.
B. SIFA ZA MTUMBA WA DUBAI
Mtumba wa dubai upo vizuri ingawa sijawahi kuagiza but kwa videos na story nazosikia ni mzuri mno hasa ukicheki wanavyofungua mabelo yao, kwa ushahidi zaidi nenda YouTube.
1. Kuagiza mtumba wa Dubai haina haja ya kuwa na app special, nenda tu YouTube then google haji second hand clothes from Dubai utawapata.
2. Shipping agent nenda Instagram search Kilimanjaro cargo ( from Dubai to Tanzania) utawapata then Fanya nao mawasiliano na process zingine ni kama mwanzo huko juu nlivyoeleza.
3. Mtumba wa Dubai unawahi kufika ( ndani ya week 2-3) ila gharama yake IPO juu kidogo,
mfano kwa kg 45 gharama take ni 450000 ( laki nne na nusu na usafiri na inategemea na aina ya nguo).
4. Namba/ mawasiliano ya WhatsApp ya Haji brand
800-8259-8259
HIZI NI BAADHI YA PICHA, VIDEO NA BEI
View attachment 1954872
Naomba unk link na huyo dada wa arusha mkuu.Mi nachukua kwa dada mmoja yeye yupo arusha huwa anauza mtumba mzuri sana kwa dar sehemu nyingi ni magumashi japo wapo pia wanaouza mtumba mzuri inagemea na nguo unayoitaka
sawa kakaMfate pm
Nimeagiza na gnm umetumia 2month kasoroIla changamoto ya silent ocean ipo na kwa agents wengine mizigo inachelewa mpaka unasahau uliagiza ni nini? Miezi hadi 3?.....je? Huko kwingine kukoje?
Hao ndio nataka kujaribu this timesNimeagiza na gnm umetumia 2month kasoro
Wakuu naomba kujua vijora / Madera kwenye Alibaba nayapata kwa ku search jina gani?
Sehemu gani mkuuIvyo wanatengeneza hapa hapa bongo 🤣
Mkuu mimi nna experience ya kuagiza na gnm na silent toka china,nipo mkoani,mzigo wangu ukifika nalipia kwa simu then wananitumia release order,unaomba watu wa warehouse wanakutafutia gari au boda depending na ukubwa wa mzigo,then kwa my case hua wananipelekea ofices za abood msimbazi na unanifikia mkoani kwangu bila wasi wasiJe hao shipping agents akina Silent Ocean etc wana huduma ya kumfikishia mzigo mteja aliye nje ya DSM?
Au ni lazima kuifuata DSM kwa aliye mkoa?