Tila-lila2
JF-Expert Member
- Oct 20, 2019
- 652
- 1,058
Mimi ni MCCM damu damu - na hata Idukilo wananijua. Tena wananijua sana - kuanzia wafanyakazi na hata wasio wafanyakazi. Nimejulikana sana kutokana kufanya biashara ya mazao na kukopesha watu wenye shida mbalimbali kwa riba nafuu. Kadri siku zinavyoenda naona dalili hata mimi mwenyewe naweza nisipigie kura viongozi mbalimbali wa CCM wa kuchaguliwa kwa mwaka huu wa Uchaguzi.
Moja naanza na Diwani wa Kata yangu - Diwani wangu huyu iwapo ni kweli atarudi huyu huyu kwa upande wa CCM sitamchagua kabisa kwa sababu ukweli amekuwa mnafiki na hasemi ukweli na kila kitu anakipeleka kiutapeli tapeli. Diwani huyu hakuwahi kusema kuwa Uchaguzi wa Selekali za Mitaa ulikuwa sio halali - sasa kama anajua Uchaguzi huo ni halali kwake na mimi nina uhakika kuwa haukuwa halali sasa ni kwa nini mimi nimchague mtu mnafiki. Kwa hiyo wakimleta huyu nakula kicha mapemaaaaa manake sitaki mautani mimi. Kama atataka apate kura yangu lazima abadilike na kukiri kuwa yeye na Chama chake walikosea sana. Watu wa Idukilo tunamtazama tu na vichinjio vyetu.
Pili, Mbunge wangu wa sasa - kama Diwani - huyu pia iwapo watamrudisha kugombea, naye bila kujali nami ni MCCM mwenzake nitamlima hakika. Tena naye mapema tu - huyu kama Diwani aliona kabisa uchaguzi wa Serekali za Mitaa haukuwa wa haki kabisa ila hajawahi kufungua mdomo na kusema ukweli kuwa upinzani ulionewa. Wkt wa uchaguzi wa mwaka huu CCM hatutaweza kufanya kama tulivyofanya Uchaguzi wa Serekali za Mitaa na hatutakuwa tayari kukaribisha kuchukiana familia na famili, ndugu na ndugu na kusababisha hadi watu kufarakana katika maisha yao yote na kukosekana kwa amani. Wale viongozi wa kutoka upinzani hawakuwahi kuwa watu wabaya kwetu sasa kwa nini walifanyiwa vile na sisi tunaangalia tu.
Hii imeeneza sana chuki kati yetu na mwaka huu kwa kweli hamna kabisa kukubali na zaidi itakuwa ni jino kwa jino sisi na upinzani. Tayari wa upinzani wanajianda kwa hilo na mimi nawaunga mkono kwa sababu sioni ubaya wao iwapo hata kama wakishinda. Huyu Mbunge hata kule bungeni ameshindwa kueleza kuwa uchaguzi wa Serekali za Mitaa umeleta chuki dhidi yetu. Ameshindwa pia kueleza hata mambo mengine ambayo ni chukizo kwa upendo wa sisi kama ndugu.
Ndugu zetu waliokuwa wakituongoza kupitia upinzani hawakuwa na ubaya wowote na waliishi vizuri tu na sisi. Leo hii Yule Mwenyekiti wa Serekali za Mitaa aliyeletwa na CCM anawaweka weka watu rumande bila utaratibu wowote. Yeye kama ilivyo kwa Diwani walipaswa kueleza kwenye mikutano yao ya bungeni au hata mabarza ya madiwani kuwa uchaguzi wa Serekeli za Mitaa hatukuwatendea vema wenzetu wa upinzani. Kwa maana hiyo km watamrudisha mwenyewe nasisitiza tena nitamkata funua mapema sana. Simpi kura yangu mtu mnafiki.
Tatu, kwa upande wa URais pengine atayasema makosa yaliyofanyika kipindi chake na kuamua kuyarekebisha kwa uchaguzi ujao. Najua wa Chama changu atapewa nafasi tena - bila kuongelea kuwa makosa yalifanyika uchaguzi wa Serekali za mitaa simpigii kura. Asiposema kuwa kubinya haki za wapinzani (kama mikutano na maandamano) ilikuwa ni bahati mbaya kwa kipindi hiki - hapati kura yangu. Asiposema kuwa kuzuia nyongeza ya mishahara ya wafanyazi kwa miaka yake yote alikosea simpi kura. Asiposema kuna watu wameshtakiwa na hata kuadhibiwa kimakosa simpi kura. Asiposema awamu yake imezembea kufuatilia watu waliopotea katika mazingira ya utata simpi kura. Asiposema kutopeleleza na kupata ukweli kuhusu Tundu Lisu kupigwa risasi simpi kura. Asiposema kujali mauchumi makubwa ya kununua mindege ambayo mpaka sasa imepaki tu na kuacha kuwasaidia wananchi kuondokana na umaskini unaowakabili ni kosa napo simpi kura. Asipotoa sababu kwa nini ameamua kuhakikisha Chato wanapata miradi mingi zaidi ya kimaendeleo kwa upendeleo sitampa kura. Asiposema kuwanunua wapinzani na kuwahamishia CCM na kuwapa mavyeo na nafasi ilikuwa ni kero kubwa kwa sisi tuliopo CCM imetukwaza sana hadi tunajiona hatufai, sitampa kura hakika.
Ukweli kura yangu ni ya kumchagua nani haijajulikana mpaka sasa. Kuna uwezekano kwa mara ya kwanza nikaacha kupigia chama changu na kuwaongezea nguvu marafiki zetu wapinzani kwa sababu ya unafiki wa viongozi wetu na sisi wenyewe kujifanya kufumbia macho mambo ambayo kwa ukweli wa dhati ya Mwenyezi Mungu ni ya kijinga katika siasa na upendo wa nchi yetu.
Ukweli hayo ni machache tu ambayo tunategemea Rais atayatolea majibu. Sisi tunasubiri tu wakinyamaza na sisi tutanyamaza tu na kusikiliza matokeao yake redioni au kuangalia kwenye TV.