Habari wadau,
Nilikuwa nawadharau sana vijana wanaoimbaimba na kucheza cheza TikTok. Nawaona wapuuzi hawana kazi ya kufanya na wajinga.
Mtoto wa shangazi yangu ni mmojawapo wa hao wapuuzi wa TikTok. Ana followers laki 6 huko TikTok. Ni binti ana miaka 21 na anasoma chuo kikuu kimojawapo nchini.
Shangazi alikuwa analalamika anahisi mtoto wake amekuwa tapeli ama amepata madanga. Maana amekuwa na pesa huku hana ajira yeyote, mara kanunua boda boda, mara kanunua simu ya gharama, mara kanunua mavifaa ya saloon ya kike.
Baada ya dogo kuhojiwa sana akafunguka hela anavyozipata. Yupo chuo mwaka wa pili now. Akasema hela anazipata kupitia TikTok. Wasanii wa bongo fleva wanataka nyimbo zao zitrend TikTok.
Hivyo wakitoa nyimbo zao huwa wanawafata watu wenye followers wengi TikTok na kuwaambia waanzishe challenge za nyimbo zao ili kuwainfluence followers wao na wao waige na mwisho nyimbo inakuwa hit song.
Hivyo wasanii huwa wanawalipa hao TikToker wa kuanzisha challenge kama yeye. Mfano yeye anachaji elfu 30 kwa challenge ya wimbo wa msanii.
Wasanii wapo kibao na wengi ma underground na nyimbo mpya zinatoka kila siku. Hivyo kwa siku iliyokuja vizuri anaweza kuhudumia hata wasanii 10 na kuingiza laki 3 easy tu japo pia kuna siku huwa hapati mteja hata mmoja.
Pia kuna wasanii wa Kenya na Nigeria nao wana mchezo huu. Pia waimba nyimbo za injili na kwaya kina Rose Muhando, Bukuku na wengineo nao wameiga mchezo huu. Hivyo ndio inampa hela anazonunua vitu.
Dogo katuonesha inbox yake TikTok na Instagram tukaona wasanii kibao wamemfata DM na wanavyomtumia miamala kaonesha ili kutetea hela zake kwamba anazipata kihalali.
Binafsi nimeshangaa sana na kumpongeza dogo kwa jinsi alivyojiajiri.