Jinsi "wasaliti " wanavyoula CCM, huku wafia chama wakitoswa



Inauma sana, ila inabidi iwe hivyo maana ni maagizo toka juu.
 
Hiyo ndiyo demokrasia, ukichoka chama unahamia chama kingine

Ufipa mbona mnasahau mapema sana mbona Mbowe alivyo mkaribisha fisadi Lowasa hamna mwana ufipa aliye kasirika?
 

Katiba yao inaruhusu fikra za mwenyekiti, zidumu fikra za mwenyekiti na ukipingana na hizi fikra hama chama.
 
Naomba unipe kifungu cha katiba kinacho sema hayo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu siye wengine ni wana CCM wa kufa na kupona na si wana CCM wa msimu wa mavuno ya pamba.
 
mmmh!
Lakini si hata CDM nako EDO alipata nafasi ya kugombea u presidia matokeo yake Slaa akatoswa?
Au hata hiyo nafasi ya Sumaye Pwani kwani hakuna watu wa CDM waliokitumikia muda mrefu wangefaa?
CCM ni chama kongwe, huwezi linganisha na Chadema ambacho kinahangaikia utanuzi wa uhai wake. Kinachofanywa na CCM Sasa ni dhihirisho la wazi ya madai ya EDO kuwa aliibiwa kura 6milioni. Kwa hakika CCM inatetea uhai wake, maana 2015 kilikaribia kukata roho, kikapona kwa risasi na wizi. Sasa kinatapatapa Kama mke anayejua kwa hakika kuwa mume ameshamtema hivyo kwa kihoro atajigonga hata kwa maadui wa mumewe ilimradi akifikiri mme huyo atamrudia, kumbe hola, wanamnajisi bure kwa hasara yake mwenyewe. Mwisho wa siku ni kufa kifo kisicho na kilio.
 
maneno kuntu
 
Hizo ni mbinu za Vita ndugu yangu, lazima uijaribu silaha ya adui yako ukiipata, sasa wamerudi ccm Yale waliyokuwa wakilalamika sasa wanapewa rungu, usijaribu kupita mbele yao utaumia si unaona hawana Matamko ya muweke ndani masaa48,pole Sana hiyo ndo siasa..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…