Ulimbo
JF-Expert Member
- Aug 14, 2009
- 3,768
- 4,038
Wana JF
Sipati picha, wanachama wa CCM wananuna mtaani balaa, kati ya vitu ambavyo vimewakera ni pamoja na kwenda kinyume na katiba ya chama ambayo inasema kila mwanachama anayejiunga na chama cha mapinduzi lazima awe amekaa kwa kipindi flan ndipo atagombe kwenye nafasi za uongozi. Tunacho shuhudia hapa ni kuona walio kihama chama ndio wanao rudishwa kwenye maeneo yale yale, mpaka sasa wanachama wa ccm wanataka kupasuka maana wapo waliokuwa wanamendea hizo nafasi lakini hawawezi kupata tena, sasa ni dhahiri kuwa uchaguzi wa madiwani, wenyeviti na wabunge ndani ya chama kabla ya kuwasilisha tume ya uchaguzi utakuwa ni wa maamuzi na matakwa ya viongozi kwa kuamua nani atakae pewa au kuhidhinishwa agombee.
Inauma sana, ila inabidi iwe hivyo maana ni maagizo toka juu.