Jinsi "wasaliti " wanavyoula CCM, huku wafia chama wakitoswa

Jinsi "wasaliti " wanavyoula CCM, huku wafia chama wakitoswa

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Hili liwe angalizo kwa vijana wa CCM wanaokesha mitandaoni kutetea wanachokiita chama chao, lakini kumbe chama kina wenyewe.

Sasa ni dhahiri kwamba watu ambao kwa miaka mingi wameiponda CCM hadharani na gizani ndio wanaoteuliwa kushika vyeo ndani ya serikali, huku wanaojiita wafia chama wakipuuzwa na kuonekana vilaza.

Juliana Shonza, Kitilla Mkumbo, Augustino Mrema , Anna Mughwira, Julius Mtatiro , Mtella Mwampamba, Humphrey Polepole , Wilbrod Slaa , Ibrahim Lipumba ni baadhi ya majina machache tu ya walioiponda ccm kwa miaka mingi, lakini wakaonekana lulu baada ya kusaliti walikotoka.

Ndugu yangu unayejifanya CCM ni yako kiasi cha kutetea hata maovu, huu ni wakati wa kujitafakari nafasi yako ndani ya CCM , The time is now.

Majuto ni mjukuu.
 
mmmh!
Lakini si hata CDM nako EDO alipata nafasi ya kugombea u presidia matokeo yake Slaa akatoswa?
Au hata hiyo nafasi ya Sumaye Pwani kwani hakuna watu wa CDM waliokitumikia muda mrefu wangefaa?
 
mmmh!
Lakini si hata CDM nako EDO alipata nafasi ya kugombea u presidia matokeo yake Slaa akatoswa?
Au hata hiyo nafasi ya Sumaye Pwani kwani hakuna watu wa CDM waliokitumikia muda mrefu wangefaa?
Nisome nje ya mistari .
 
Hili liwe angalizo kwa vijana wa ccm wanaokesha mitandaoni kutetea wanachokiita chama chao , lakini kumbe chama kina wenyewe !

Sasa ni dhahiri kwamba watu ambao kwa miaka mingi wameiponda ccm hadharani na gizani ndio wanaoteuliwa kushika vyeo ndani ya serikali , huku wanaojiita wafia chama wakipuuzwa na kuonekana vilaza .

Juliana Shonza , Kitilla Mkumbo , Augustino Mrema , Anna Mughwira , Mtella Mwampamba , Humphrey Polepole ni baadhi ya majina machache tu ya walioiponda ccm kwa miaka mingi , lakini wakaonekana lulu baada ya kusaliti walikotoka.

Ndugu yangu unayejifanya ccm ni yako kiasi cha kutetea hata maovu , huu ni wakati wa kujitafakari nafasi yako ndani ya ccm , The time is now .

Majuto ni mjukuu .
Na wengi walioipigania CCM ikatokea wakakosea mahali hawajawahi kusaidiwa na chama hata pale walipojirekebisha.
 
Hapa Iringa aliyekuwa diwani kupitia CHADEMA Baraka kimata ndiye amependekezwa kuwania tena kiti hicho kupitia CCM huku wana CCM damu wakigeuzwa wapiga debe kwa ujira wa T-shirt na kofia!

Halafu CCM hawana shukrani kabisa kwa wafia chama wao!!
 
Makubaliano yalikuwa hayo , lakini ataangukia pua tu .
 
Hata hiyo Chadema ina wenyewe wameinunua kama kanga na sasa wanaitumia, Lowassa alipataje ile nafasi hivi alaf na lile kubwa la wajinga( Sumayee) nae alipataje nafasi Pwani, vp yule Mwenezi na Itikadi daah
 
Back
Top Bottom