Jinsi ya kufuta na kuondoa Michirizi (Stretch Mark) kwenye ngozi

Jinsi ya kufuta na kuondoa Michirizi (Stretch Mark) kwenye ngozi

Mafuta yapo yanaondoa michirizi wewe tu na utayari wako... Lakini utasahau kabisa tatizo la michirizi bila kuchubua ngozi yako
 
Habari warembo,je ni namna ipi sahihi ya kupunguza michiriz( stretch marks) kwenye ngozi inayosababishwa na sababu tofaut kama unene,kupungua,baada ya ujauzito n.k wenye ushuhuda wa ili atupe elimu kidogo.
Nunua mafuta ya parachute, makubwa 10000 madogo 5000
 
Tatizo humu hata ukimwambia mtu achangie gharama ili umtengenezee
mchanganyiko wa tiba harudi tena;

vinginevyo nitafute pm.
 
Leo nimepita kariakoo, nimepata ile dawa ya kuchanganya kwenye tiba ya Michirizi. Lakini inabidi kuchangia gharama. Karibuni.
 
Chukua colgate changanya na vaseline.

Kisha chukua kipande cha limao usugulie eneo la tukio,

Maji ya limao yakikauka paka mchanganyiko wa colgate na vaseline
 
FAHAMU AINA YA MICHIRIZI NA SULUHISHO LAKE
watu wengi hasa wakina dada wamejikuta wakikumbwa n tatzo la michirizi,(stretch marks)

Kuna aina kuu mbili michirizi
-michirizi inayotokana na uzazi.
-michirizi inayotokana na unene.
Ila wakati mwingine kuna michiriz inayobasabishwa na matumiz ya wadawa yenye kemikali,msuguano w mapaja n.k.

SULUHISHO
Jipatie wonderoil kwa ajili ya kuondoa michirizi
Bei ni 25,000tsh
Kwa mawasiliano
Whatsapp me/text/call me 0759827138
FB_IMG_1525336668092.jpg
 
Michirizi ni miongoni mwa matatizo yanayosumbua wanawake wengi. Huharibu muonekano mzuri wa ngozi na huweza kuwa inawasha pia. Kwa bahati nzuri inaeleweka jinsi inavyokuja na huweza kuzuilika na kutibika kwa urahisi tu. Leo tuangalia nini haswa husababisha michirizi.
michirizi 2.jpg


Ushawahi kuona wanawake wanaokuwa na michirizi mara nyingi huwa wanafanana kitu gani? Je, michirizi huweza kumpata mwanamke yeyote?

Kwa upande wangu tangu nimeanza kuhudumia wateja wenye michirizi sijakutana na wateja wengi ambao ni wembamba. Wengi wao huwa ni wanene, wajawazito na waliotoka kujifungua au walipata wakati wa ujauzito wao uliopita. Kwa wanawake wembamba huwa tofauti kidogo, yenyewe hutokana na matumizi ya vipodozi visivyo salama kama vile CARO LIGHT na CAROTONE.

SABABU KUU YA MICHIRIZI
Michirizi hutokana na kuongezeka haraka kwa mwili (kunenepa/ujauzito) kuliko uwezo wa ngozi kuweza kujiongeza na kutanuka vizuri kuweza kufunika ongezeko la mwili. Ngozi zetu zina vitu vinavyoitwa elastin ambavyo ndivyo husaidia ngozi kuvutika na kumudu kuongezeka na kufunika mwili wetu vizuri kila unavyoongezeka. Mwili ukiongezeka kwa kasi kuliko uwezo wa elastin kusaidia ngozi kutanuka na kuongezeka ndipo michirizi inapoanza, yaani ni kama ngozi inachanika kwa sababu imeshindwa kukua na kuvutika.

Wanawake wanene na akina mama wajawazito hupata zaidi michirizi kwa sababu hii. Na kwa kuwa miili ya wanawake wembamba haijaongezeka kwa kasi basi ngozi zao huweza kufunika vizuri na hakutokei michirizi. Ndio maana wanawake wengi wembamba hawana michirizi.

Kwa kuelewa vizuri hilo mwanamke anaweza akajikinga dhidi ya michirizi kwa kudhibiti ongezeko la mwili wake au kutumia dawa au vipodozi vinavyosaidia kupunguza na kuondoa michirizi.

Kwa upande wa vipodozi wanawake wote wanashauriwa kuepuka vipodozi vyote visivyo salama. Michirizi ni moja tu kati ya matatizo yatokanayo na matumizi ya vipodozi visivyo salama, lakini kuna matatizo mengi na makubwa zaidi ya hilo.
michirizi.jpg


USHAURI
Ni rahisi zaidi kujikinga dhidi ya michirizi kuliko kuiondoa. Pia ni rahisi zaidi kuondoa michirizi kabla haijakaa kwa muda mrefu au kuwa mikubwa kuliko kuchelewa na ikiwa mikubwa.

Mara zote jikinge dhidi ya michirizi na hakikisha unawahi kuiondoa kila mara inapoanza kujitokeza kabla haijawa tatizo kubwa.

Kama ulichelewa kidogo na ndo unaanza sasa kuiondoa basi kuwa mvumilivu kidogo maana huchukua muda kiasi kuanza kuona matokeo (takriban miezi mitatu) na kuimaliza kabisa.

Michirizi inazuilika na kutibika vizuri sana. Anza sasa.

Sasa kazi ni kwako kuchagua – kuendelea na mazoea au kufuata ushauri wa kitaalam.
AFYA ZAIDI (AZ) CONSULTANTS tunakushauri uachane na stori za kitaa na ufuate ushauri wa kitaalam. Pia usile kila kitu unachokutana nacho mtandaoni, vingine sio kwa ajili yako.

Uwe na siku njema!
michirizi 1.jpg


Kama unatumia whatsapp na ungependa kupata madarasa ya afya, urembo na vipodozi; orodha ya vipodozi visivyo salama; matatizo ya ngozi nk basi tucheki tu kwa namba 0719326693 na tutakutumia. Free for you!

Pia kama unahitaji kujifunza zaidi kuhusu afya, urembo na vipodozi kila siku hadi mwisho wa mwezi basi tutumie meseji whatsapp kwa namba hiyo hiyo na kisha tutakutumia link ya kujiunga na group letu la whatsapp na utapata elimu na ushauri zaidi. Free for you!

Kama unasumbuliwa na tatizo (afya, urembo au vipodozi) na unahitaji kuondokana nalo sasa tupigie simu au tutumie meseji au whatsapp na tutakushauri pia. Mawasiliano ya haraka ni 0743422883 na 0719326693; email ni afyazaidi@gmail.com

See you next time!
 
Back
Top Bottom