Jinsi ya kuifunga Yanga ya Gamondi

Jinsi ya kuifunga Yanga ya Gamondi

SAYVILLE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
7,895
Reaction score
12,975
Nimeshuhudia ASAS Djibouti, KMC na hata JKT wote wakicheza mpira unaofanana walipocheza na Yanga ambao umesababisha wakaadhibiwa vibaya. Leo nitatoa maoni yangu kwa timu zingine zitakazokuja kucheza na Yanga siku, wiki na miezi inayokuja nini wanatakiwa wafanye ili wapate matokeo.

Kwanza punguzeni pasi za kurudisha mipira nyuma (backpasses). Yanga ni timu ambayo sasa hivi inazingatia sana kukaba sana na wanakaba kwa ile filosofia ambayo kocha wa Simba Robertinho amekuwa anaiongelea sana, kukabia kutokea juu. Maana yake timu pinzani zinapata ugumu wa kufikisha mipira hata katikati ya dimba. Tumeshuhudia KMC hawakupiga shuti hata moja on target wala off target langoni kwa Yanga kwa dakika zote 90. Sasa cha kushangaza pamoja na ugumu huu, timu zote hizi zilizofungwa zilikuwa na tabia wanaweza kufika katikati ya uwanja au kunyang'anya mpira kutoka kwa mchezaji wa Yanga, ila badala ya kuongeza pressure kwenda mbele wanarudi nyuma, matokeo yake unashindwa tena kufika hata kati kabla ya kupokonywa mipira. Jana JKT kila walivyokuwa wanarudisha mpira nyuma nilikuwa nasema hawataweza tena kuufikisha tena kati kabla ya kuupoteza na kweli ilikuwa hivyo. Ukiangalia ASAS walipojaribu kupress mwishoni mwa kipindi cha kwanza kama nakumbuka vizuri, kidogo walionekana kusumbua ila hawakuwa na muendelezo huo wakaishia kufanya hayo niliyosema hapo juu. Hili nalisisitiza sana maana ndiyo tatizo sugu.

Pili, acheni kucheza vipasipasi visivyo na maana mkiwa eneo lenu la ulinzi. Focus kwenda mbele haraka inavyowezekana. Afadhali uoshe halafu mpira upotee kwenye final third ya mpinzani kuliko upotee kwenye eneo lenu la ulinzi. Jambo rahisi kulielewa lakini inashangaza timu nyingi zinashindwa kulitekeleza.

Tatu, labda kama timu yako ina wachezaji kama Denis Kibu wanaoweza kupambania mipira mirefu ya juu na kuishinda, epuka kucheza mipira mirefu ya kugombania. Asilimia 98 ya mipira yote mirefu ya JKT ilikuwa inapotea. Cheza mpira wa chini wa kwenda mbele ukzingatia jambo la kwanza nililosema. Kwa kiasi kikubwa inavyowezekana mipira mirefu ya juu labda iwe ya kona, krosi au faulo. Kwa viwanja vya mikoani vyenye milima na mabonde, timu zote mbili zinapata shida kucheza mpira wa chini kwa hiyo mipira mirefu inaweza kutumika.

Mwisho lakini siyo kwa umuhimu, wiki 2 kabla ya mechi nyang'anya simu wachezaji wenu au kama kuna uwezo monitor mawasiliano yao yote. Kinga ni bora kuliko tiba.

Ila najua haya mawazo wala hayatazingatiwa maana hivi vitimu wala havijitambui. Hivi wewe mchezaji wa Jeshi la Kujenga Taifa unasukumwa na mtu kama Musonda halafu unanyong'onyea?
 
Nimepitia uzi wako vizuri kabisa nahoja zangu.

1. Quality players..huwezi kupishana na timu kubwa kama YANGA halafu wachezaji wako wanauwezo mdogo utegemee matokeo mazuri jibu ni hapana maana wachezaji wazuri wanambinu za KILA namna wanakupanua kulia, kushoto, katikati msako utatoa hutoi.

2. Kucheza KWA teamwork : Timu kama Yanga ikitokea timu inauwezo mdogo wacheze tu kama timu uwezi kupelekwa tu mpira Mbele Maana ukifika kati utazuiliwa hapa ni mashambulizi ya kushtukiza mazuri lazima Nidhamu itakwepo tu.

3. Timu pinzani zijitahidi zisiruhusu makosa mengi eneo la box japo ni ngumu ila team ikishirikiana hakuna lisilowezekana
 
Umeongea vyema. Ila kwa mtizamo wangu, timu inayoshambulia mwanzo mwisho ni ngumu kuihimili kama na ww hauishambulii kurudisha nyuma wingback zake pamoja na viungo.

Kwa style ya uchezaji wa yanga wa sasa itaimudu pekee timu ambayo ni giant yenye wachezaji wazuri ambao wataweza kupishana na yanga bila shida na kuilazimisha yanga kurudi nyuma ikishambulia kwa kwa umakini.

Mfano Azam aliamua kutumia misuli na miguvu bila akili mwishowe akapasuka. Simba nae aliamua kupak bass huku akisukuma counter attack ingawa yanga alishindwa kupata goli.
 
Nimepitia uzi wako vizuri kabisa nahoja zangu
1.Quality players..huwezi kupishana na timu kubwa kama YANGA alafu wachezaji wako wanauwezo mdogo utegemee matokeo mazuri jibu ni hapana maana wachezaji wazuri wanambinu za KILA namna wanakupanua kulia,kushoto ,katikati msako utatoa hutoi
2.Kucheza KWA teamwork : Timu kama Yanga ikitokea timu inauwezo mdogo wacheze tu kama timu uwezi kupelekwa tu mpira Mbele Maana ukifika Kati utazuiliwa apa ni mashambulizi ya kushtukiza mazuri lazima Nidhamu itakwepo tu
3.Timu pinzani zijitahidi zisiruhusu makosa mengi eneo la box japo ni ngumu ila team ikishirikiana hakuna lisilowezekana
Ndiyo maana nimesisitiza wacheze kwa nidhamu zaidi ya jinsi hizi timu zilivyoonyesha
 
Umeongea vyema. Ila kwa mtizamo wangu, timu inayoshambulia mwanzo mwisho ni ngumu kuihimili kama na ww hauishambulii kurudisha nyuma wingback zake pamoja na viungo.
Point nzuri. Hauwezi kucheza dakika 90 unakaa kusubiri mashambulizi tu. Tena afadhali wangekuwa wanapaki basi tujue moja wamekuja kujilinda ila unacheza mpira wa wazi wa kumuachia mpinzani wako acheze anavyotaka na afike hadi kwenye 18 yako kwa jinsi anavyojisikia, utapigwa tu.

Hizi timu zote ukiziangalia zilivyokuwa zinacheza dakika 25-30 unajua kama hawatabadili uchezaji wao wanaenda kupigwa tu.
 
Yanga ni timu inayopenda kushambulia, Ina mabeki was pembeni wenye Kasi na wanaopenda kupanda na kuanzisha mashambulizi. Kmc na Jkt wore walicheza mchezo unaofanana yaani kukaa nyuma. Madhara ya mchezo huo ni kuruhusu muda wore mpira kuchezwa golini kwako.
Unawazuiaje, njia pekee ni kuhakikisha unakuwa na mawinfa wenye Kasi na kushambulia ilu usiwape nafasi mabeki wao kupanda na kuanzisha mashambulizi.
 
Nimeshuhudia ASAS Djibouti, KMC na hata JKT wote wakicheza mpira unaofanana walipocheza na Yanga ambao umesababisha wakaadhibiwa vibaya. Leo nitatoa maoni yangu kwa timu zingine zitakazokuja kucheza na Yanga siku, wiki na miezi inayokuja nini wanatakiwa wafanye ili wapate matokeo.

Kwanza punguzeni pasi za kurudisha mipira nyuma (backpasses). Yanga ni timu ambayo sasa hivi inazingatia sana kukaba sana na wanakaba kwa ile filosofia ambayo kocha wa Simba Robertinho amekuwa anaiongelea sana, kukabia kutokea juu. Maana yake timu pinzani zinapata ugumu wa kufikisha mipira hata katikati ya dimba. Tumeshuhudia KMC hawakupiga shuti hata moja on target wala off target langoni kwa Yanga kwa dakika zote 90. Sasa cha kushangaza pamoja na ugumu huu, timu zote hizi zilizofungwa zilikuwa na tabia wanaweza kufika katikati ya uwanja au kunyang'anya mpira kutoka kwa mchezaji wa Yanga, ila badala ya kuongeza pressure kwenda mbele wanarudi nyuma, matokeo yake unashindwa tena kufika hata kati kabla ya kupokonywa mipira. Jana JKT kila walivyokuwa wanarudisha mpira nyuma nilikuwa nasema hawataweza tena kuufikisha tena kati kabla ya kuupoteza na kweli ilikuwa hivyo. Ukiangalia ASAS walipojaribu kupress mwishoni mwa kipindi cha kwanza kama nakumbuka vizuri, kidogo walionekana kusumbua ila hawakuwa na muendelezo huo wakaishia kufanya hayo niliyosema hapo juu. Hili nalisisitiza sana maana ndiyo tatizo sugu.

Pili, acheni kucheza vipasipasi visivyo na maana mkiwa eneo lenu la ulinzi. Focus kwenda mbele haraka inavyowezekana. Afadhali uoshe halafu mpira upotee kwenye final third ya mpinzani kuliko upotee kwenye eneo lenu la ulinzi. Jambo rahisi kulielewa lakini inashangaza timu nyingi zinashindwa kulitekeleza.

Tatu, labda kama timu yako ina wachezaji kama Denis Kibu wanaoweza kupambania mipira mirefu ya juu na kuishinda, epuka kucheza mipira mirefu ya kugombania. Asilimia 98 ya mipira yote mirefu ya JKT ilikuwa inapotea. Cheza mpira wa chini wa kwenda mbele ukzingatia jambo la kwanza nililosema. Kwa kiasi kikubwa inavyowezekana mipira mirefu ya juu labda iwe ya kona, krosi au faulo. Kwa viwanja vya mikoani vyenye milima na mabonde, timu zote mbili zinapata shida kucheza mpira wa chini kwa hiyo mipira mirefu inaweza kutumika.

Mwisho lakini siyo kwa umuhimu, wiki 2 kabla ya mechi nyang'anya simu wachezaji wenu au kama kuna uwezo monitor mawasiliano yao yote. Kinga ni bora kuliko tiba.

Ila najua haya mawazo wala hayatazingatiwa maana hivi vitimu wala havijitambui. Hivi wewe mchezaji wa Jeshi la Kujenga Taifa unasukumwa na mtu kama Musonda halafu unanyong'onyea?
JKT walicheza vizuri kipindi chote Cha kwanza,wangendelea na ule mpira mpaka mwishoni wangeweza pata hata drop

Walikaba vyema,walipress vizuri sana

Shida ilianza kipindi Cha pili
 
Back
Top Bottom