Jinsi ya kuishi na mwanamke kwa furaha na amani katika ndoa

Pole mkuu kwa kuingia chaka..wadada wa kinyakyusa watata sana, na wengine wanajisifu...
Mimi mnyakyusa ila nimeapa siwezi oa hawa dada zetu, maana wao jeuri wanaona sifa!
 
wengine ukiwafanyia hivyo ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa.Haelewi kitu.Kinachoeeleweka zaidi kuwa na pesa tu
 
Kuna ukweli na ka lugha ka kinafiki.

Kuwa mkweli, akikosea mkosoe kwa upendo na mrekebishe uwezapo. Akifanya vzr, mpongeze sana!!

Ukweli utawapeni uhuru-Maneno matamu ya Yesu!
 
Wanawake wengine hata uwafanyie haya yote uliyosema gubu ndo asili yao yani ni kazi bureeeee
 
Tulia na mkeo na watoto michepuko sku zote huwa ni pasua kichwa tu mzeee
 
Mi wangu ni wakutafuta trouble atashika Simu atachunguza akikosa ataenda kukagua gari akikosa mabag yangu maana mi mtu wa safari akikosa kote ataanzisha na watu tunaoishi nao humu ndani na mkigombana atataka kila mtu ajue au watu wajue tunachogombana
MI WANGU ANAANZA KWA KULALA MZUNGU WA NNE,NA MIMI NAUCHUNA HATA WIKI MBILI .
 
Ndoa ili iwe ndoa inabidi Mshabihiane, Maana yake kosa litazamwe ni kosa kwa muktadha wake halikadhalika jambo zuri litazamwe kwa uzuri wake, sasa ikitokea Mume anasema Mke wangu hapa umekosea then Mke anasema hili sio kosa hapo ndo shughuli inapoanzia coz inabidi mkubaliane kutokukubaliana mwishoe kila Mtu atakuwa anapuyanga kivyake!
Panapohitaji sifa basi Mume mwaga sifa sana na panapohitaji kukosolewa basi mkosoane ingawaje hapa ndo busara huwa inahitajika sana Maana unaweza kuambulia kichambo kitakatifu hadi ukaishia kumnasa Makofi.., hili la kurekebishana mnapokoseana litatoa vifundo na chuki Moyoni hatimae kuishi kwa amani..,
Haiwezekani Mkeo anatoka amevaa Mapazia eti umsifie kuwa ametoka Chicha huu utakuwa unafiki wa kiwango cha lami, na utaishia kutamani Wanawake wa nje waliopendeza vema coz unataka Mkeo awe hivyo ila ndo hivyo unashindwa kumwambia unabaki kusifia hata akivaa Magunia. Aidha ni ngumu kuishi kisanii ndani ya ndoa maisha yako yote labda muwe hamuishi pamoja!!!
 
Ungesema tu ulikuwa safar mbona tungekuelewa eti Sweden majigambo ya kishamba sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…