Jinsi ya kujua kirahisi ukubwa wa tatizo la corona jiulize kwenye ukoo wako wamekufa wangapi kwa Corona?

Jinsi ya kujua kirahisi ukubwa wa tatizo la corona jiulize kwenye ukoo wako wamekufa wangapi kwa Corona?

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Posts
36,900
Reaction score
52,056
Kujua kirahisi kama tatizo la corona in kubwa sana Tanzania au la jiulize kwenye ukoo wako upande wa baba yako na mama yako na mke au mume wangapi wameugua ugonjwa wa corona, wangapi wamekufa kwa corona, wangapi bado wanatibiwa corona na je maambukizi ya corona yanaongezeka kwenye hizo koo zako au yanapungua?

Hutakiwi kusema tu ohh serikali inaficha takwimu. Hakiki wewe mwenyewe kwenye ukoo wako; takwimu ambazo ni rahisi tu kuzipata sababu wewe ni sehemu ya wanaukoo.

Usilishwe takwimu hewa ya kufikirika za wazushi wawe Wa vijiweni,wanasiasa au mitandaoni hakiki mwenyewe. Uzuri kwa sisi Waafrika tuna koo kubwa sana na ni rahisi kujua tatizo likitokea kubwa kwenye ukoo, taarifa ni rahisi kupata.
 
Kwahiyo sasa hii ndio njia rasmi ya kupata takwimu za corona Tanzania?

Jr[emoji769]
Kauliza tu swali, jibu kama kuna mtu kafa kwenu. Halafu mshana, tukikagua chumbani kwako chini ya uvungu, lazima tutakuta misufuria ya nyungu yako mkeo na watoto tena ile meusiii kwa ajili ya kuni. Wewe mshana unataka kuniambia hupigi nyungu wewe? Acha kupotosha Ufipa wenzio.
 
Kwangu amefariki babu, lakini wakati anatibiwa hospital hawakuwahi kusema ni corona, alipofariki tu wakasema ni corona. Hakuna aliyewaamini maana ni ujinga tu. Mtu amestaafu utumishi 10yrs back, kufa kwa pressure related disease ni kawaida.

Hadi sasa ndugu jamaa na marafiki walioingia hofu wakidhani waliyemuuguza amekufa kwa corona, hakuna aliyewekwa isolation na hakuna aliyeathirika kwa lolote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kauliza tu swali,jibu kama kuna mtu kafa kwenu. Halafu mshana, tukikagua chumbani kwako chini ya uvungu, lazima tutakuta misufuria ya nyungu yako, mkeo na watoto tena ile meusiii kwa ajili ya kuni. We mshana unataka kuniambia hupigi nyungu wewe?Acha kupotosha ufipa wenzio
Vipi kabombe mbona maneno mingi alfajiri yote hii? Ni wapi nimepotosha?
Mimi tiba zangu ni za asili na nyungu naipiga sana. Na nimefanya hivyo hata kabla ya matangazo ya wanasiasa.

Jr[emoji769]
 
Mkuu Ukimwi upo na kuna familia hazijawahi pata toka umeingia.
Sijaongelea familia naongelea koo. Ukimwi koo nyingi zimepata Asilimia kubwa ya koo za Tanzania hajazijakosa mtu aliyekufa kwa ukimwi Kwa familia nakubali zipo familia hazijawahi pata lakini koo hapana hata ukoo wangu wako waliofariki kwa ukimwi lakini kwenye familia yangu hakuna.
 
Nenda kasome Mambo ya Walawi sura ya 13,14 mpaka sura ya 15 huu ujinga mpaka sijui afe kwa Corona ndo ionyeshe upo ni ujinga tu kama ujinga mwingine cha msingi fata maelekezo ya Watu wa Afya na uache kujidhalisha mkuu Ukimwi upo na kuna familia hazijawahi pata toka umeingia
Hakuna ukoo ambao haujaguswa na mgonjwa wa UKIMWI.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukoo wetu haujaguswa tangu umeanza huo ukimwi..
Ndio maana nimesema koo nyingi zimeguswa na ukimwi sijasema zote hazijaguswa yako imo kwenye hizo chache ambazo hazijaguswa hongera kama ni kweli unalosema!!!!
 
Back
Top Bottom