Festo Andrews
Member
- Apr 1, 2022
- 23
- 25
Kwa kawaida, watu wengi, hasa wale wanaoanza safari yao kwenye ulimwengu wa cryptocurrency, mara nyingi hupenda kuangalia bei ya coin. Wanafikiria, “Hii bei ni ndogo sana! Acha ninunue kabla haijapanda!” Lakini, rafiki, ngoja nikushike mkono na kukuonyesha siri kubwa ya soko hili kwani bei ya coin si kila kitu!
Leo, hebu tuzungumzie mambo mawili muhimu ambayo unapaswa kuyazingatia kabla hujaruka na kuwekeza kwenye coin yoyote: MARKET CAPITAL na PRICE TAG. Vitu hivi viwili vinaweza kuonekana kama mapacha, lakini vina tofauti kubwa ambayo kila mwekezaji anapaswa kuielewa
Watu wengi huchanganya mambo haya kwa sababu ya kufikiria kwa haraka. Unakutana na coin kama Shiba Inu, ina bei ya chini sana $0.00002261. Halafu unaona coin nyingine kama AAVE, yenye bei ya $321. Bila kufikiria mara mbili, unaweza kusema, “Nitanunua Shiba Inu! Bei yake inaweza kufikia Bitcoin siku moja!” Lakini, ukweli ni kwamba hii si kweli hata kidogo.
Ngoja nikueleze kwa mfano rahisi. Pichani hapo chini tuna coin tatu: Bitcoin, Shiba Inu, na AAVE. Bitcoin, ambayo kila mtu anaijua, ndiyo ya kwanza sokoni kwa thamani, lakini pia ina bei kubwa mno zaidi ya $96,000 kwa coin moja. Shiba Inu inashika nafasi ya 15 ikiwa na thamani ya $0.00002261 kwa thamani ya jumla na AAVE, kwa upande mwingine, iko nafasi ya 31 na bei yake ni $321 lakini kwenye rank inaonekana kuwa chini ya Shiba Inu.
Sasa, kuna kitu kinaitwa market cap, ambacho kinatumika kupima thamani halisi ya coin sokoni. Formula ni rahisi;
Market cap = Idadi ya Sarafu zilizopo sokoni x Bei ya sarafu moja
BITCOIN

= 19,805,021 BTC X $96,474.26
Market cap = $1,911,085,944,894.46.
AAVE

Market cap = 15,038,887 AAVE X $321=$4,839,664,225
Market cap=$4,839,664,225
Kwahiyo ili coin yoyote ipande bei mara mbili, inahitaji pesa zaidi iwekezwe sokoni. Kwa mfano,bei ya AAVE kwa sasa ni $321 kwahiyo ili AAVE ipande kutoka $321.81 hadi $643.62, inahitaji market cap yake iongezeke mara mbili kutoka $4,839,664,225 na kufikia $9,679,328,450
SHIBA INU
Lakini kwa Shiba Inu, safari ni ndefu zaidi. Itahitaji market cap yake iongezeke kutoka 13,334,727,500 mpaka 26,669,455,000

=589,250,000,000,000 SHIB X $0.00002263
Market Cap= 13,334,727,500
Hii inaonyesha kuwa ingawa Shiba Inu inaonekana kuwa na bei rahisi, inahitaji pesa nyingi zaidi sokoni ili bei yake ipande. Kwa upande mwingine, AAVE, licha ya bei yake kuwa juu, ni rahisi kupanda kwa sababu idadi ya sarafu zake sokoni ni ndogo.
Kwahiyo unapofananisha coin yoyote ile na coin nyingine Usiangalie bei ya hiyo coin iliyopo sokoni ( price tag) bali angalia Market cap yake. Na taarifa kama hizi unaweza ukazipata kwenye website kama Coin market cap na Coin gecko
1. Coin zilizopo sokoni (circulating supply)
2. Price ya coin
3. Market cap ya hiyo coin ni kiasi gani
Kwahiyo kabla hujanunua coin yoyote tumia market cap kwanza kuzicompare usitumie bei iliyopo sokoni utapotea
NB: Usione coin ina bei ndogo ukajua basi ndio bei rahisi HAPANA mfano mzuri tumechukua Shiba Inu na AAVE tumeona AAVE ana bei kubwa kuliko Shiba Innu lakini kimahesabu tumeona coin ambayo ina bei rahisi ni AAVE mwenye bei ya $321 kwa sababu anahitaji pesa kidogo tu ili hela yake ijidouble ukifananisha na Shiba Inu ambaye anahitaji pesa nyingi sana ili aweze kupush price yake iende mara mbili.