Jinsi ya kumlea mtoto wa mme

Jinsi ya kumlea mtoto wa mme

ROHO MBAYA HIYO.

Yani wawe unataka kujaribu kumdhiti mumeo na ndoa yako kwa kumlipisha huyo mtoto kukosa malezi ya mama yake na baba pia? Kama humtaki nyumbani kwako unataka kumtoa kwa mama yake wa kazi gani? Wakati mnachumbiana na kuona ulikuwa wapi usijadili hili swala na mumeo au hata kulifikiria tu wewe mwenyewe? ACHA UBINAFSI. Mwache mtoto alelewe na mama yake na kama ni kwenda boarding akiwa na umri mdogo hivyo (kitu ambacho binafsi siafiki) acha uamuzi huo ufanywe na mama yake mzazi na sio wewe. Wewe subiri ukizaa wako ndio umtimulie boarding bila sababu ya msingi akiwa na umri huo.

asante kwa ushauri, hua sipendi ligi, message sent
 
Mtoto alelewe na mama yake mzazi, hakuna kitu bora kwa ukuwaji wa mtoto huyo bali kuwa na uhusiano wa dhati na mama yake. Mumeo, a hakikishe kafanya wajibu wake wa kutekeleza mahitaji ya mtoto huyo, pia ina wezekana mtoto huyo awe anakuja kwa baba yake mara kwa mara [at least when he is over 5yrs, he is too young now].

Nawe, kuwa na imani na ndoa yako.
 
Kwa kuongezea tu. . .
Ulifanya makosa makubwa sana kuolewa na mtu ambae tayari ana mtoto na mwanamke mwingine wakati hujiamini na una wivu ambao unaweza kuzaa manyanyaso kwa huyo mtoto uliyemkuta. Hauko tayari kumlea huyo mtoto, wala hauko tayari alelewe na mama yake. Ulitakiwa utafute ambae hana mtoto ili wivu wako uishie kwa watu ambao hauna uwezo wa kuwafikishia hasira zako kwa kuadhibu viumbe visivyohusika na matatizo yako siku ukitamani kufanya hivyo.

Acha huyo mtoto akae kwa mama yake, kama unataka mchunge mumeo kama mbuzi ili asije akala nyasi za jirani.

asante
 
Wasiwasi wako ni nini bibie? kuwa watakumbushia zamani au? Ujue chochote utakachopanga kufanya inategemea na akili ya huyo mzazi mwenzie mumeo. Usikute wala hawazii unayoyawaza wewe anataka malezi bora tu ya mtoto wao.
Usijitwishe mzigo wa kumlea mtoto wa mwenzio tena mtoto mdogo kiasi hicho ilhali ana mama yake mzazi aliye hai.Utaanza kuambiwa unamtesa mtoto wa watu nk. Kuwa na amani, kuwasiliana kwao hakuepukiki hata mtoto aende boarding au akae na nyie. Sema wewe na mumeo mngeweka misingi imara kuhusu suala hili..sanasana ukiliweka mawazoni litazidi kukuchanganya. Na please usimchukie huyo mtoto, hana hatia kabisa!!

asante bidada, wacha aendelea kukua kwa mama yake kwanza hadi atakapoamua kumleta
 
asante bidada, wacha aendelea kukua kwa mama yake kwanza hadi atakapoamua kumleta

Yes ufanye hivyo..cha muhimu ni mumeo kuwa na mawasiliano mazuri na muwazi kuhusu huyo mtoto wake. Kama huna mtoto/watoto na wewe huu ndiyo muda utafute maana utakuwa busy unalea. All the best!!
 
miaka 3!!?mwache alelewe na mama yake!kuzaa aze mwingine ulee ww kisa?tulia
..acha atume matumizi
...ww hujawa mama bado subiri wako!
....Km wana mpango wa kuendelea na hayo mawasilino,hata ukimchukua wataendelea tu,tena ndo utakua umewapa nafasi! Ww unafikiri huyo mwenzio anafurahi kuachwa?tena wanaweza kuongeza mwingine hawana akili hawa!
..acha awe busy kulea baba kazi yake ni kutuma matumizi mpaka mama atakapoolewa ndo aje kwako,kutuma matumizi sio lzm waonane unless kuna kitu kinaendelea
kwenye red hapo ....kwangu mimi siyo sababu ya msingi......
 
sims nawe upo tayari mtoto wako alelewe na mwingine
sipendi mtoto wangu alelewe na mwingine labda tu itokee kuna mazingira ambayo sina jinsi lakini itanipasa mtoto wangu alelewe na mtu mwingine.....lakini pia sina tatizo kumlea mtoto wa mwanamke mwingine....mana ntakavyowalea watoto wangu ndivyo hvyo ntamlea na huyo mtoto wa mtu mwingine......ntakachowafanyia watoto wangu nae ntamfanyia hvyohvyo.......
 
Morning.Naombeni ushauri jamani,mme wangu ana baby boy umri yapata miaka 3 kutoka kwa X wake .naomba ushauri kwani nawaza mtoto aendelee kukaa kwa mama yake huku akiomba matunzo ya baba hapa naogopa mawasiliano ya moja kwa moja na mume wangu au tumchukue tuje kuishi nae nikiwa mama mlezi Naombeni ipi itakua njia nzuri ambayo nitaimudu na angalau itakua na tija kwenye ndoa yangu.

Hili suala umelijua hivi karibuni au kabla ya ndoa?
 
Weeeeeeeeeeeeee! Ishia hapo hapo! Muache huko huko kwa mama yake!

Yaani ukilogwa kujitia una mamy spirit na kumleta jianadae na yafatayo

1. Badala ya mumeo kwenda kwa maza mtoto, mzazi mwenzie atakuwa anakuja humo kwenye jumba lako kumuona mwanae, and you will be supposed to be happy! Cause you asked for it! Na ndugu wa huyo mama mtoto nao wanakuja humo kwenye kasri lako kumuona mtoto! Mbona kazi utakuwa nayo!

2. Mfarakano na mumeo usioisha! No matter how sweet, devoted, dedicated you will be kwa yule mtoto mumeo ataona unamtesa, ama hufanyii the best he is expecting. Basi majangaa hayatoisha! Mwnaume atakununia hadi ukome.

3. Ukimchukua huyo, Watazaa mwengine! Coz matumizi hatoi hayamuumi tena, wanakumbushia, ama anaenda small house mpya anajisahau mnarudi square 1. Ila mzazi mwenzie akiwa nambuguzi na watu wa ustawi, vikao na wazazi, simu za kudai matumizi, hamu yoyote ya kutoka nje inamuisha akikumbuka tabu hio dudu yake inasinyaa yenyewe! Muache abebe msalaba wake.

Kwani sasa hivi angali hakai na mwanae kuna kinachomzuia kuongeza wa pili na huyo ex wake akiwa anaenda huko kumsalimia? What makes you think kuwa jamaa akienda huko hakumbushii sarakasi za zamani?
Nime peruzi tu na kudadisi tu Suprise usiogope.
 
Last edited by a moderator:
nisaidie faida za kumlea huyo mtoto ukiihusisha ndoa yangu tafadhali mkuu.pili nilikua nawaza kama nikimchukua tumchukue umri wa kwenda shule labda mwakani na tumtafutie boarding ili akirudi likizo awe anaenda kwa mama yake, unaonaje hili

Who are you kwa huyo mtoto mpaka uanze kuwaza mipango yakumchukua, kumpeleka boarding sijui kumpeleka wapi? Huyo mama yake hana akili timamu? Huyo mama yake hawezi kumlea? Yani unaona kumpeleka mtoto boarding ndio umemsaidia mtoto na ndoa? Unaona kumtenga mtoto na mama yake wakati ambapo umeshamtenga na baba ake ni haki.

Mtoto ulimkuta, ukakubali kuolewa, funga mdomo, lea ndoa uliyoitaka, muache huyo mtoto na mama yake. Hakuhusu hata kidogo labda siku mume wako akuambie namleta mtoto kwa sababu walizokubaliana wao wenyewe n ahuyo mama mzazi wake. Of which kama huyo mama ana AKILI hatakubali kumuacha mtoto wake mdogo hivyo akakulie mazingira magumu ya boarding.

Kwa kifupi ushauri wangu, kama huyo baba anamlea huyo mtoto muache alee damu yake, umemkuta naye, heshimu hilo, we fanya kilichokupeleka huko kwake, subiri Mungu akupe mwanao utamlea au akifika miaka mitatu utampeleka boarding pia. Sawa mama angu.............Usimwazie hivyo huyo mtoto, wala hutakiwi kujipa stress, utakujakumkosea Mungu bureeeeee. Be a mother and a wife.......Karibu tena.
 
Kwa kuongezea tu. . .
Ulifanya makosa makubwa sana kuolewa na mtu ambae tayari ana mtoto na mwanamke mwingine wakati hujiamini na una wivu ambao unaweza kuzaa manyanyaso kwa huyo mtoto uliyemkuta. Hauko tayari kumlea huyo mtoto, wala hauko tayari alelewe na mama yake. Ulitakiwa utafute ambae hana mtoto ili wivu wako uishie kwa watu ambao hauna uwezo wa kuwafikishia hasira zako kwa kuadhibu viumbe visivyohusika na matatizo yako siku ukitamani kufanya hivyo.

Acha huyo mtoto akae kwa mama yake, kama unataka mchunge mumeo kama mbuzi ili asije akala nyasi za jirani.

Nimekumisije jamani? Ulipotelea wapi shoga angu?
 
.ingekua wa kwangu ningemlea so hiyo isingekua swali kipindi hiki

There is the problem. Mtazamo ungekuwa sawa na wa Nyamayao ungeelewa mtoto wa mwenzio ni wa kwako. (infact in this case ur hubby...)
 
Mwache akalelewe na mama yake kwa sasa, mbona muda wa wewe kumlea utafika tu?
 
miaka 3!!?mwache alelewe na mama yake!kuzaa aze mwingine ulee ww kisa?tulia
..acha atume matumizi
...ww hujawa mama bado subiri wako!
....Km wana mpango wa kuendelea na hayo mawasilino,hata ukimchukua wataendelea tu,tena ndo utakua umewapa nafasi! Ww unafikiri huyo mwenzio anafurahi kuachwa?tena wanaweza kuongeza mwingine hawana akili hawa!
..acha awe busy kulea baba kazi yake ni kutuma matumizi mpaka mama atakapoolewa ndo aje kwako,kutuma matumizi sio lzm waonane unless kuna kitu kinaendelea

Kutuma matumizi si mpaka waonane!!!!!! Nadhani umesahau kuwa mtoto anaweza kuugua, baba anaweza kuwa na hamu ya kumuona mwanawe, so, you cant prevent the man from seeing his son and thus his son's mother.
 
sipendi mtoto wangu alelewe na mwingine labda tu itokee kuna mazingira ambayo sina jinsi lakini itanipasa mtoto wangu alelewe na mtu mwingine.....lakini pia sina tatizo kumlea mtoto wa mwanamke mwingine....mana ntakavyowalea watoto wangu ndivyo hvyo ntamlea na huyo mtoto wa mtu mwingine......ntakachowafanyia watoto wangu nae ntamfanyia hvyohvyo.......

asante, mie jamani binti yangu nampenda sana, yaani tena alivyo na wadogo zake hakuna mtu atahisi sio wangu wa kumzaa, na huwa sisemagi ni mtoto wa mume wangu, yule ni mtoto/binti yangu wa kwanza...
 
bora umchukue mumlee ila uwe na moyo wa kulea mtoto wa mwenzio namna ile ile ambayo unalea wa kwako. kama unahisi utamnyanyasa muache kwa *****. ukimchukua itasaidia kupunguza mawasiliano kidocho
 
Morning.Naombeni ushauri jamani,mme wangu ana baby boy umri yapata miaka 3 kutoka kwa X wake .naomba ushauri kwani nawaza mtoto aendelee kukaa kwa mama yake huku akiomba matunzo ya baba hapa naogopa mawasiliano ya moja kwa moja na mume wangu au tumchukue tuje kuishi nae nikiwa mama mlezi Naombeni ipi itakua njia nzuri ambayo nitaimudu na angalau itakua na tija kwenye ndoa yangu.

aisee mi nina mtoto wa huo umri x wangu kaoa hiv karibun usikute unawaza kumchukua mwanangu coz hata unipigie magot siwez kukubali na hata umlambe huyo mtoto miguu i will not appreciate nitawaza unamtesa tuu mwanangu kila siko zaa wa kwako mamii ee kuzaa nizae mm kulea ulee wewe wap na wap hat umshauri huyo mumeo asimlee mtoto siwez kuwapa bado nishakuachia huyo mwanaume kuwa na aman naomba mungu usiwe ndio mke wa x wangu kwan naona hatutawezana kabisaaa halafu kama huyo mumeo hajakwambia tumekubaliana mtoto ataish kwangu and am a mother hapa so nina kauli ya mwisho kwa mwanangu when am saying no hamna wakunichallenge
 
Back
Top Bottom