Jinsi ya kumlea mtoto wa mme

Jinsi ya kumlea mtoto wa mme

bora umchukue mumlee ila uwe na moyo wa kulea mtoto wa mwenzio namna ile ile ambayo unalea wa kwako. kama unahisi utamnyanyasa muache kwa *****. ukimchukua itasaidia kupunguza mawasiliano kidocho

Ina maana mama hatatakiwa kumjulia hal mwanae au kuja kumsalimia
 
Morning.Naombeni ushauri jamani,mme wangu ana baby boy umri yapata miaka 3 kutoka kwa X wake .naomba ushauri kwani nawaza mtoto aendelee kukaa kwa mama yake huku akiomba matunzo ya baba hapa naogopa mawasiliano ya moja kwa moja na mume wangu au tumchukue tuje kuishi nae nikiwa mama mlezi Naombeni ipi itakua njia nzuri ambayo nitaimudu na angalau itakua na tija kwenye ndoa yangu.
Mchukueni mkae nae mumlee wote. Wewe na mumeo
 
Unajitafutia pressure mwanmke mwenzangu, mtoto wa mtu ni wa mtu hata umfanye nini hana shukurani, ni wachache wenye kushukuru...wengine wanatumiwa na mama zao kukuharibia kwa mume wako mara unamnyanyasa, na wengine wanaweza kupeleka maneno ukweni/kwa mawifi ili uonekane mbaya..hapo ndio utaiona ndoa chungu japo umemchukua kwa nia njema inaweza kukufanya ukajuta baadae...na ukishamchukua kumuondoa inakuwa ngumu..

Usijitafutie matatizo mapema yote hii, we endelea na life na muamini mumeo kama anakupenda kwn angempenda huyo aliyezaa naye si angemuoa? tulia na muachie Mungu ila mwambie mumeo awe muwazi asifiche chochote na hata anapotaka kwenda kumsalimia ni vizuri mkaambatana nae..
 
Hongera Nyamayao wapo wachache sana wenye roho kama ya kwako. Nakumbuka wakati tunakuwa baba alizaa nje ya ndoa najua ndoa yao ilkuwa kwenye msusuko mkubwa sana kwasababu baba alizaa wakati yupo kwenye ndoa mama akaona sio kesi akamwambie kamlete huyo mtoto nitamlea baba akaongea na mzazi mwenzie wakakubaliana akamchua mtoto akamleta nyumbani akiwa na umri wa miaka 3 mama akamlea kama mwanae wa kumzaa kiasi kwamba yule mdogo wetu alijua yule ni mama yake wa kumzaa mpaka anamaliza std 7 watu wakaanza kumwambia kwamba huyo sio mama yako yeye akawa anamuuliza mama mbona kuna watu wananiambie eti wewe sio mama yangu mama akamwambia achana nao usiwasikilize,alipomaliza form 4 mama akaona ni muda muafaka wa kumuambia ukweli akamkalisha chini akamueleza ukweli wote.Wapo wanawake wachache sana wanaoweza kulea watoto wa kambo
asante, mie jamani binti yangu nampenda sana, yaani tena alivyo na wadogo zake hakuna mtu atahisi sio wangu wa kumzaa, na huwa sisemagi ni mtoto wa mume wangu, yule ni mtoto/binti yangu wa kwanza...
 
Last edited by a moderator:
Kuishi na huyo mtoto hakuzuii mwanaume kueneleza mahusiano na ex wake,

Unachotakiwa kukiwaza na kujiridhisha ni kimoja tu: uaminifu na msimamao wa mumeo

Kama mwanaume mzinzi haisaidii

Kama mwanaume ana stara basi hilo ndo la muhimu

Mwisho kumbuka huyo mwanamke ndo alobeba mimba na kuzaa na ndo mwenye uchungu na mwanae, akiamua kumleta mtoto sawa, asipoamua ni sawa afterall kisheria ni mpaka mtoto atimize miaka 7, msimkoseshe mwanamke kubond na mwanae na kulea mwanae na msimkoseshe mtoto mapenzi ya mama yake kwa insecurities zenu

nilijua mpenzi ila nahisi kama sina amani hivi coz huyo mama hajaolewa nahisi kama atakua huru na visingizio kibao kuhusu mtoto, natamani apate mume haraka nipunguze presha
 
Hajakwambia ni sababu ipi iliyomfanya mkaoana nyinyi na akaacha kumwoa huyo aliyezaa nae hapo kabla?
 
Hata kama huyo mtoto atabaki kwa mama yake, Inakubidi uwe makini katika mawasiliano yao kwani inakuwa rahisi huyo mumeo kushawishiwa na mzazi mwenzie wakajikuta wameongeza mwingine kitendo ambacho kwa vyovyote vile ni lazima kitakukwaza na hata kuharibu ndoa yako
 
Weeeeeeeeeeeeee! Ishia hapo hapo! Muache huko huko kwa mama yake!

Yaani ukilogwa kujitia una mamy spirit na kumleta jianadae na yafatayo

1. Badala ya mumeo kwenda kwa maza mtoto, mzazi mwenzie atakuwa anakuja humo kwenye jumba lako kumuona mwanae, and you will be supposed to be happy! Cause you asked for it! Na ndugu wa huyo mama mtoto nao wanakuja humo kwenye kasri lako kumuona mtoto! Mbona kazi utakuwa nayo!

2. Mfarakano na mumeo usioisha! No matter how sweet, devoted, dedicated you will be kwa yule mtoto mumeo ataona unamtesa, ama hufanyii the best he is expecting. Basi majangaa hayatoisha! Mwnaume atakununia hadi ukome.

3. Ukimchukua huyo, Watazaa mwengine! Coz matumizi hatoi hayamuumi tena, wanakumbushia, ama anaenda small house mpya anajisahau mnarudi square 1. Ila mzazi mwenzie akiwa nambuguzi na watu wa ustawi, vikao na wazazi, simu za kudai matumizi, hamu yoyote ya kutoka nje inamuisha akikumbuka tabu hio dudu yake inasinyaa yenyewe! Muache abebe msalaba wake.

Well said
 
Hongera Nyamayao wapo wachache sana wenye roho kama ya kwako. Nakumbuka wakati tunakuwa baba alizaa nje ya ndoa najua ndoa yao ilkuwa kwenye msusuko mkubwa sana kwasababu baba alizaa wakati yupo kwenye ndoa mama akaona sio kesi akamwambie kamlete huyo mtoto nitamlea baba akaongea na mzazi mwenzie wakakubaliana akamchua mtoto akamleta nyumbani akiwa na umri wa miaka 3 mama akamlea kama mwanae wa kumzaa kiasi kwamba yule mdogo wetu alijua yule ni mama yake wa kumzaa mpaka anamaliza std 7 watu wakaanza kumwambia kwamba huyo sio mama yako yeye akawa anamuuliza mama mbona kuna watu wananiambie eti wewe sio mama yangu mama akamwambia achana nao usiwasikilize,alipomaliza form 4 mama akaona ni muda muafaka wa kumuambia ukweli akamkalisha chini akamueleza ukweli wote.Wapo wanawake wachache sana wanaoweza kulea watoto wa kambo
Baba hakuongeza tena mtoto wa nje?
 
Suprise alitakiwa alete part two hii, maisha yameendeleaje huko teh....
 
nisaidie faida za kumlea huyo mtoto ukiihusisha ndoa yangu tafadhali mkuu.pili nilikua nawaza kama nikimchukua tumchukue umri wa kwenda shule labda mwakani na tumtafutie boarding ili akirudi likizo awe anaenda kwa mama yake, unaonaje hili
Mimi ningekuwa mama wa huyo mtoto... Haki ningekutandika ngumi haswa. Umchukue mwanangu wa kiume umpeleke boarding akiwa na miaka minne.... Hujui uchungu wa kuzaa ndio maana unaongea unachoongea.
 
kiukweli ningekua mimi nahisi ningeendelea tu mlea mwanangu coz naamini sana katika mapenzi ya mama kuliko baba nachowaza ni hiyo cake ya mapato kuigawanya huku na huku
Selfish woman. Inaelekea uko na huyo mwanamume sababu ya vipesa vya kubadilisha mboga. Ingekuwa ni mwanao usingefanya hivyo. Huyo sio mwanao ndio sababu unafanya hivyo????.... Na sio kwamba hata una mapenzi na huyo mtoto. Mmmmm.....!!
 
nisaidie faida za kumlea huyo mtoto ukiihusisha ndoa yangu tafadhali mkuu.pili nilikua nawaza kama nikimchukua tumchukue umri wa kwenda shule labda mwakani na tumtafutie boarding ili akirudi likizo awe anaenda kwa mama yake, unaonaje hili
Dada kweli mtoto wa miaka minne unawaza kumpeleka boarding? Kweli mama ni aliyekuzaa...
 
Selfish woman. Inaelekea uko na huyo mwanamume sababu ya vipesa vya kubadilisha mboga. Ingekuwa ni mwanao usingefanya hivyo. Huyo sio mwanao ndio sababu unafanya hivyo????.... Na sio kwamba hata una mapenzi na huyo mtoto. Mmmmmxxxxxxyyyyyy.....!!
Umewahi kulea mtoto wa kambo? Labda km una experience hiyo ndo umshambulie mtoa mada........
 
Dada kweli mtoto wa miaka minne unawaza kumpeleka boarding? Kweli mama ni aliyekuzaa...
Yaani kuna wanawake hatari Sana kwenye hii jamii tuliyopo. Angekuwa ni mwanae wa kumzaa kweli angempeleka boarding mtoto wa miaka minne?? Hivi anajua mtoto wa miaka minne anafananaje na kuwekwa boarding??
 
She don't deserve hata kuwa na huyo baba...Hana nia ya kulea the kid...
 
Back
Top Bottom