Jinsi ya kumtengenezea mwanaume hofu ya kukupoteza

Jinsi ya kumtengenezea mwanaume hofu ya kukupoteza

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
446
Reaction score
1,113
Thamani yako kwake inategemeana na Kiasi cha hofu aliyonayo. Asipokuwa na hofu atakutreat vyovyote atakavyoona inafaa. Haya ndiyo mambo utakayoyafanya Kukusaidia uweze Kumtengenezea hiyo hofu.

1. Muoneshe wanaume wanaokutaka wanamzidi yeye. Hii haitakiwi Kwa kiburi wala dhihaka, bali Kwa namna yenye busara. mwanaume akiona wanaume wengine wanathamini thamani yako, anaanza Kujua ana Kitu cha thamani kubwa ambacho anatakiwa Kulinda.

2. Muoneshe Thamani Yako Katika Maisha Yake; Uwe mchango mkubwa Katika furaha, utulivu, na maendeleo yake. Mwanaume asiyeona thamani yako atadhani hata ukiondoka maisha yake yataendelea Kama Kawaida. Mfanye atambue wewe ni sehemu muhimu ya ufanisi wake. Mfanye ajue na aone anakuhitaji aendelee kuwepo kwa sababu ya thamani yako.

3. Mfanye ajue kama akikupoteza hatokupata tena. Kuwa mwanamke wa kipekee kwa matendo, nidhamu, na mvuto. Mfanye atambue yeye kubaki na wewe ni bahati ambayo si kila mwanaume anaipata. Na akikupoteza, hatapata tena mtu kama wewe. Kama akijua ukiondoka utarudi, akikupoteza anaweza kukupata tena hatokuthamini.

mwanaume kukupotez.png
 
Naona umeamua kuwapoteza wanawake wenzako mkuu....
Ila kwenye namba 2 upo sawa sana, lakini namba 1 na 3 umewaelekeza kibla wenzio mazeee.....
Maana sisi wanaume ukitaka kutulinganisha na kutuonyesha kama kuna wengi wanao kutaka, hapo tayari utapoteza sifa ya kuaminika na itafikia wakati hatuto ogopa kukupoteza
 
Kuna mmoja jana aliniambia kwamba amenichoka na anataka aondoke.....
Nikamjibu kwamba kabla hajaondoka kuna jambo nataka anisaidie....
Alipo uliza ni jambo gani...??
Nikamwambia.... natamani akiondoka asirudi tena, hapo atakua amenisaidia sana...😜
 
Naandika bila code, inayemhusu akisoma kama yupo jf atanijua😂

Kuna watu sogea tukae walikua wanagombana, siku hiyo nilikua nimeenda kuwasalimia.
Mwanamke akamwambia mwanaume usinibabaishe kuna daktari bingwa ananitaka kila siku, namkatalia kisa wewe

Mwanaume akamwambia kwa hasira nipe namba yake
Mwanamke akaona kamuumiza mwanaume kihisia kawin! Bibie kwa mbwembwe akamjibu nikupe ili iweje
Mwanaume akamaliza kibabe Nimpigie ili aje kukuchukua, anipunguzie mzigo.

Nilicheka sana.
 
Mwanaume wa wapi huyo utakayemuonesha kwamba kuna wanaume wengine wanakutaka ili yeye akupende na aogope kukupoteza?

Hutujui tu sisi wanaume wewe mama. Sisi wanaume tuna principle yetu kwamba mwanamke ni mzuri akiwa kwa mume wake ama mpenzi wake hivyo ukijichanganya kwenda kwa hao wahuni walikudanganya wanakuthamini kuliko mumeo umekwisha.
 
Naandika bila code, inayemhusu akisoma kama yupo jf atanijua😂

Kuna watu sogea tukae walikua wanagombana, siku hiyo nilikua nimeenda kuwasalimia.
Mwanamke akamwambia mwanaume usinibabaishe kuna daktari bingwa ananitaka kila siku, namkatalia kisa wewe

Mwanaume akamwambia kwa hasira nipe namba yake
Mwanamke akaona kamuumiza mwanaume kihisia kawin! Bibie kwa mbwembwe akamjibu nikupe ili iweje
Mwanaume akamaliza kibabe Nimpigie ili aje kukuchukua, anipunguzie mzigo.

Nilicheka sana.
Umezungumza ukweli mtupu dada mzuri.

Na huu ndiyo ukweli kuhusu wanaume. Yaani eti umuoneshe kwamba wapo wanaokuthamini kuliko yeye ndiyo azidishe kukupenda? La hasha!

Mleta mada atawaponza mabinti wa watu watapuyanga na kila mwanaume kama watamsikiliza.
 
Wanawake bwana;
Kwanza hakuna mwanaume ambaye ana hofu ya kumpoteza mwanamke.Hakunaga hiyo.Kuna mwanaume anayefurahia kuwa na mwanamke na siyo mwenye hofu ya kukupoteza.

Pili hakuna mbinu ya nyingine ya kuweza kumfanya mwanaume afurahie kukaa na wewe isipokuwa tu uwe "mwanamke" Uwe na "Heshima" Usiwe na "Kisirani" na Usiwe "Mjingamjinga"

Wanaume wengi wanaridhika na Good Food,Good Sex na Calm Home.Akivikosa hivyo atayumba yumba sana.

All in ALL Miss Halima Karibu JF
 
Back
Top Bottom