Mwaka wa Mbele
JF-Expert Member
- Mar 5, 2026
- 1,013
- 3,017
Naandika bila code, inayemhusu akisoma kama yupo jf atanijua😂
Kuna watu sogea tukae walikua wanagombana, siku hiyo nilikua nimeenda kuwasalimia.
Mwanamke akamwambia mwanaume usinibabaishe kuna daktari bingwa ananitaka kila siku, namkatalia kisa wewe
Mwanaume akamwambia kwa hasira nipe namba yake
Mwanamke akaona kamuumiza mwanaume kihisia kawin! Bibie kwa mbwembwe akamjibu nikupe ili iweje
Mwanaume akamaliza kibabe Nimpigie ili aje kukuchukua, anipunguzie mzigo.
Nilicheka sana.
Ila kwenye Mahusiano, wote mkiwa wababe, wote mkiwa na EGO (kwamba unajiona ni bora kuliko mwenzio) , basi hayawezi kudumu.
Mkilumbana kidogo , basi unafikiria kama je mwenzangu ana haki ya kulalamika?. Kama anayo. Bas ww unatulia unamsikiliza.
Na kama una la kujitetea . Unajitetea . Yanaisha kikubwa namna hiyo.
Sio Mwanaume amepanic , alaf mwanamke badala atulie anaanza kuleta kamdomo kake.
Aisee, Wanawake hamjui tu jinsi gan wanaume sisi hatupendi kufokewa.
Hata kama nimekukosea , basi nichambe taratibu 😊😊😊😊.