Thamani yako kwake inategemeana na Kiasi cha hofu aliyonayo. Asipokuwa na hofu atakutreat vyovyote atakavyoona inafaa. Haya ndiyo mambo utakayoyafanya Kukusaidia uweze Kumtengenezea hiyo hofu.
1. Muoneshe wanaume wanaokutaka wanamzidi yeye. Hii haitakiwi Kwa kiburi wala dhihaka, bali Kwa namna yenye busara. mwanaume akiona wanaume wengine wanathamini thamani yako, anaanza Kujua ana Kitu cha thamani kubwa ambacho anatakiwa Kulinda.
2. Muoneshe Thamani Yako Katika Maisha Yake; Uwe mchango mkubwa Katika furaha, utulivu, na maendeleo yake. Mwanaume asiyeona thamani yako atadhani hata ukiondoka maisha yake yataendelea Kama Kawaida. Mfanye atambue wewe ni sehemu muhimu ya ufanisi wake. Mfanye ajue na aone anakuhitaji aendelee kuwepo kwa sababu ya thamani yako.
3. Mfanye ajue kama akikupoteza hatokupata tena. Kuwa mwanamke wa kipekee kwa matendo, nidhamu, na mvuto. Mfanye atambue yeye kubaki na wewe ni bahati ambayo si kila mwanaume anaipata. Na akikupoteza, hatapata tena mtu kama wewe. Kama akijua ukiondoka utarudi, akikupoteza anaweza kukupata tena hatokuthamini.