Mwaka wa Mbele
JF-Expert Member
- Mar 5, 2026
- 1,013
- 3,017
Naandika bila code, inayemhusu akisoma kama yupo jf atanijua😂
Kuna watu sogea tukae walikua wanagombana, siku hiyo nilikua nimeenda kuwasalimia.
Mwanamke akamwambia mwanaume usinibabaishe kuna daktari bingwa ananitaka kila siku, namkatalia kisa wewe
Mwanaume akamwambia kwa hasira nipe namba yake
Mwanamke akaona kamuumiza mwanaume kihisia kawin! Bibie kwa mbwembwe akamjibu nikupe ili iweje
Mwanaume akamaliza kibabe Nimpigie ili aje kukuchukua, anipunguzie mzigo.
Nilicheka sana.
Mwanamke wa kufanya hivi labda mama yako mzaziHata kama nimekukosea , basi nichambe taratibu 😊😊😊😊.
Usiusemee moyo.Mwanamke wa kufanya hivi labda mama yako mzazi
Ahahaha.Kuna mmoja jana aliniambia kwamba amenichoka na anataka aondoke.....
Nikamjibu kwamba kabla hajaondoka kuna jambo nataka anisaidie....
Alipo uliza ni jambo gani...??
Nikamwambia.... natamani akiondoka asirudi tena, hapo atakua amenisaidia sana...😜
Ujinga uliopea viwango.Thamani yako kwake inategemeana na Kiasi cha hofu aliyonayo. Asipokuwa na hofu atakutreat vyovyote atakavyoona inafaa. Haya ndiyo mambo utakayoyafanya Kukusaidia uweze Kumtengenezea hiyo hofu.
1. Muoneshe wanaume wanaokutaka wanamzidi yeye. Hii haitakiwi Kwa kiburi wala dhihaka, bali Kwa namna yenye busara. mwanaume akiona wanaume wengine wanathamini thamani yako, anaanza Kujua ana Kitu cha thamani kubwa ambacho anatakiwa Kulinda.
2. Muoneshe Thamani Yako Katika Maisha Yake; Uwe mchango mkubwa Katika furaha, utulivu, na maendeleo yake. Mwanaume asiyeona thamani yako atadhani hata ukiondoka maisha yake yataendelea Kama Kawaida. Mfanye atambue wewe ni sehemu muhimu ya ufanisi wake. Mfanye ajue na aone anakuhitaji aendelee kuwepo kwa sababu ya thamani yako.
3. Mfanye ajue kama akikupoteza hatokupata tena. Kuwa mwanamke wa kipekee kwa matendo, nidhamu, na mvuto. Mfanye atambue yeye kubaki na wewe ni bahati ambayo si kila mwanaume anaipata. Na akikupoteza, hatapata tena mtu kama wewe. Kama akijua ukiondoka utarudi, akikupoteza anaweza kukupata tena hatokuthamini.
Title: dumb ways to loose your manThamani yako kwake inategemeana na Kiasi cha hofu aliyonayo. Asipokuwa na hofu atakutreat vyovyote atakavyoona inafaa. Haya ndiyo mambo utakayoyafanya Kukusaidia uweze Kumtengenezea hiyo hofu.
1. Muoneshe wanaume wanaokutaka wanamzidi yeye. Hii haitakiwi Kwa kiburi wala dhihaka, bali Kwa namna yenye busara. mwanaume akiona wanaume wengine wanathamini thamani yako, anaanza Kujua ana Kitu cha thamani kubwa ambacho anatakiwa Kulinda.
2. Muoneshe Thamani Yako Katika Maisha Yake; Uwe mchango mkubwa Katika furaha, utulivu, na maendeleo yake. Mwanaume asiyeona thamani yako atadhani hata ukiondoka maisha yake yataendelea Kama Kawaida. Mfanye atambue wewe ni sehemu muhimu ya ufanisi wake. Mfanye ajue na aone anakuhitaji aendelee kuwepo kwa sababu ya thamani yako.
3. Mfanye ajue kama akikupoteza hatokupata tena. Kuwa mwanamke wa kipekee kwa matendo, nidhamu, na mvuto. Mfanye atambue yeye kubaki na wewe ni bahati ambayo si kila mwanaume anaipata. Na akikupoteza, hatapata tena mtu kama wewe. Kama akijua ukiondoka utarudi, akikupoteza anaweza kukupata tena hatokuthamini.
😁😁😁Tulishakubaliana Ndoa ni moja ya utapeli tuko makini sasa hivi .