Jinsi ya kununua ardhi kwenye Metaverse (Decentraland)

Jinsi ya kununua ardhi kwenye Metaverse (Decentraland)

mkuu viwanja vipo usa au vya kufikirika? nikitaka kuendeleza na sio kuuza ina kuwaje? kuna huduma ya kwenda kuona viwanja kabla ya kununua? ktk viwanja kuna umeme na maji? km ngapi kutoka lami? au viwanja fikirishi?
Hio picha kwny ID yako imejieleza vzr.
 
Hio picha kwny ID yako imejieleza vzr.
IMANI YA CHAMA
Binadamu wote ni sawa; Kila mtu ana stahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake; Ujamaa na kujitegemea ndiyo njia pekee ya kujenga jamii ya watu walio sawa na huru
 
Aiseee...
Ukiona kwenye NFT watu wanavyouza arts za ajabu kwa mamilioni, mpaka wazazi wanaweka picha za michoro waliochora watoto wao kidigitali na kupiga hela ndefu.....
Hii sasa ya Land ndio hivyo, sisi wa dunia ya tatu tutaona ni ujinga wa mwisho lakini ndio hii dunia ya leo unaambiwa...you snooze..you looze, watu wanakesha cypto kusubiri just the bullish climb....
Hahaaaaaa Man this world is insane. Unanunua ardhi ambayo haipo duuuh
 
Labda kwa kuwaelimisha wale wenye akili ya shit hole countries...

Ni hivi hizo virtual land zinaweza kutumika kutengeneza mandhari ya kidigitali yenye muonekano unaoweza kutumika kwenye games hizi mnazocheza kila siku , na hata hamjui zimetengenezwaje...

EuroTruck, Grand Theft Auto au Fortnite......hayo mandhari ya majumba, barabara, na ma korobwezo yote...

Wale Game developer wa kibongo labda watatueleza zaidi................!!!
 
Jibu hoja mkuu
Huu ni ukichaa kama ukichaa mwingine eti mtu anatoa milions of dollars kununua ardhi kwenye metaverse karibu na snoop.
Nft bubble ipo siku itapasuka wajanja watakuwa washaondoka na utajiri
 
Huu ni ukichaa kama ukichaa mwingine eti mtu anatoa milions of dollars kununua ardhi kwenye metaverse karibu na snoop.
Nft bubble ipo siku itapasuka wajanja watakuwa washaondoka na utajiri
Hahahaaa! Mkuu huna imani kabisa na NFT?
 
Hahahaaa! Mkuu huna imani kabisa na NFT?
Unajua mkuu now tunapoingia web 3 watu wanatafta njia ya kutengeneza pesa. Katika hozo harakati kuna zitakazofanikiwa na kuna sitakazofail.
Hii ilitokea pia mwanzo wa internet watu waliona kuna potential lakini how to monetize it. Kulikuwa na idea funny sana na ziliwork kwa mida mfupi zikafa. Kila mtu alikuwa anajaribu anachoona. Kuna makampuni mengi yalivuma kwa muda mfupi yakafa.
Kuna mambo mengi kwenye NFT na metaverse hayamake sense. Bila shaka ni race ya kumonetize web 3 kama ilivyokiwa mwanzoni mwa web 2
 
Kipindi insane bitcoin luna wenzako waliandika kama ulichoandika. Hakuna kikomo Kenya kuyatafuta maarifa.
Bit coins na forex and alike huko hapana ain't my things nyie endeleeni na fantasy zenu
 
Metaverse ni ulimwengu wa 3D wa kidigitali ambao umetengenezwa kwa mifano ya vitu vyote vilivyopo kwenye dunia tunayoishi kwa sasa.

kupitia Metaverse watu wataweza kukutana,kushiriki michezo,kufanya kazi,kujenga miundombinu mipya na kufanya biashara mbalimbali

October 2021, Kampuni ya Facebook waliamua kubadili Jina lao na kujiita Meta na hapo ndipo teknolojia hii ya Metaverse ikashika kasi zaidi duniani.

Mimi leo nataka nikujulishe juu ya biashara kubwa sana ya mamilioni ya kifedha ambayo inaendelea katika ulimwengu wa metaverse kupitia kampuni ya Decentraland

Decentraland ni kampuni inayosimamia sarafu za kidigitali ziitwazo MANA ambazo hizi sarafu zinamuwezesha mtu kufanya manunuzi ya ardhi na vitu vingine kwenye ulimwengu wa metaverse kupitia soko lake

Thamani ya Sarafu moja ya Mana kwa sasa ni dola 3.06 na huwa inatabia ya kupanda thamani au kushuka thamani kulingana na soko la cryptocurrency

Umiliki wa ardhi kwenye metaverse una faida nyingi sana kama zilivyoorodheshwa hapa chini

1. Unaweza kuiuza kwa mtu mwingine kwa bei ya juu

2. Unaweza kuikodisha kwa watu wengine

3. Unaweza kujenga Nyumba(virtual house),hotels,malls au chochote kisha ukakodisha au kuuza pia

4. Ukinunua land tayari hiyo ni NFT pia

Hivyo kuna pesa nyingi sana ambazo unaweza ukatengeneza kupitia Metaverse

Jinsi Ya Kununua Kiwanja Kwenye Metaverse (Decentraland)

1. Hatua ya kwanza ni kununua MANA tokens kupitia masoko ya cryptocurrency

2 Hamishia hizo Mana kwenye wallets zinazosupport ERC 20 tokens mfano ni Metamask

3. Ingia kwenye marketplace ya Decentraland kupitia hii link : Decentraland - Marketplace

4. Chagua kiwanja chako kisha unaweza ku jump in kukiona live in virtual world,viwanja ni 16m kwa 16m(256 Square meters) na idadi yake ni viwanja 90601 tu.

5. Bonyeza BUY Button or Place a Bid mmiliki atareceive your offer na utakuwa umenunua kiwanja chako in a virtual world

View attachment 2073654
Naona hii project imefail japo meta wameweka mpunga mrefu sana. Takwimu zinaonyesha watu wengi wakiingia hawarudi na maeneo mengi hayajatembelewa na inatabiriwa kuwa biashara nyingi za huko zitakuwa zimefungwa by 2025.
Huenda ni wazo zuri lakini approach haikuwa sahihi same thing kilichotokea mwanzo wa internet watu walikuwa wanajaribu kila kitu.
 
Naona hii project imefail japo meta wameweka mpunga mrefu sana. Takwimu zinaonyesha watu wengi wakiingia hawarudi na maeneo mengi hayajatembelewa na inatabiriwa kuwa biashara nyingi za huko zitakuwa zimefungwa by 2025.
Huenda ni wazo zuri lakini approach haikuwa sahihi same thing kilichotokea mwanzo wa internet watu walikuwa wanajaribu kila kitu.
Ikigunduliwa VR gear set iliyokamilika ambayo haina usumbufu katika viewing angles, viewing quality na the problem with locomotion...Hii itapaa tena.
Na wale walionunua saiv kwa dola 3 watauza kwa millions of dollars
 
Back
Top Bottom