Jinsi ya kununua ardhi kwenye Metaverse (Decentraland)

Jinsi ya kununua ardhi kwenye Metaverse (Decentraland)

Ikigunduliwa VR gear set iliyokamilika ambayo haina usumbufu katika viewing angles, viewing quality na the problem with locomotion...Hii itapaa tena.
Na wale walionunua saiv kwa dola 3 watauza kwa millions of dollars
Labda microsoft yeye naona ameamua build yako on top of ya meta. Na hisa za meta zimedrop kwa sababu ya hiki kitu
 
Yaani! Mpaka tutaelewa tu
JamiiForums-1502650973.jpg
 
Metaverse ni ulimwengu wa 3D wa kidigitali ambao umetengenezwa kwa mifano ya vitu vyote vilivyopo kwenye dunia tunayoishi kwa sasa.

kupitia Metaverse watu wataweza kukutana,kushiriki michezo,kufanya kazi,kujenga miundombinu mipya na kufanya biashara mbalimbali

October 2021, Kampuni ya Facebook waliamua kubadili Jina lao na kujiita Meta na hapo ndipo teknolojia hii ya Metaverse ikashika kasi zaidi duniani.

Mimi leo nataka nikujulishe juu ya biashara kubwa sana ya mamilioni ya kifedha ambayo inaendelea katika ulimwengu wa metaverse kupitia kampuni ya Decentraland

Decentraland ni kampuni inayosimamia sarafu za kidigitali ziitwazo MANA ambazo hizi sarafu zinamuwezesha mtu kufanya manunuzi ya ardhi na vitu vingine kwenye ulimwengu wa metaverse kupitia soko lake

Thamani ya Sarafu moja ya Mana kwa sasa ni dola 3.06 na huwa inatabia ya kupanda thamani au kushuka thamani kulingana na soko la cryptocurrency

Umiliki wa ardhi kwenye metaverse una faida nyingi sana kama zilivyoorodheshwa hapa chini

1. Unaweza kuiuza kwa mtu mwingine kwa bei ya juu

2. Unaweza kuikodisha kwa watu wengine

3. Unaweza kujenga Nyumba(virtual house),hotels,malls au chochote kisha ukakodisha au kuuza pia

4. Ukinunua land tayari hiyo ni NFT pia

Hivyo kuna pesa nyingi sana ambazo unaweza ukatengeneza kupitia Metaverse

Jinsi Ya Kununua Kiwanja Kwenye Metaverse (Decentraland)

1. Hatua ya kwanza ni kununua MANA tokens kupitia masoko ya cryptocurrency

2 Hamishia hizo Mana kwenye wallets zinazosupport ERC 20 tokens mfano ni Metamask

3. Ingia kwenye marketplace ya Decentraland kupitia hii link : Decentraland - Marketplace

4. Chagua kiwanja chako kisha unaweza ku jump in kukiona live in virtual world,viwanja ni 16m kwa 16m(256 Square meters) na idadi yake ni viwanja 90601 tu.

5. Bonyeza BUY Button or Place a Bid mmiliki atareceive your offer na utakuwa umenunua kiwanja chako in a virtual world

View attachment 2073654
Mkuu vipi huu uwekezaji.
Zuckebergy inasemekana kaizika rasmi sasa kahamia rasmi kwenye AI maana huku loss imekuwa kubwa na mafanikio 0.
Walionunua viwanja wavitelekeze tu
 
Back
Top Bottom