Jinsi ya kuondoa au kupunguza mafuta tumboni kwa wanawake (Vitambi vya kike)

Hivi hio procedure sio kwa watu wenye constipation??? mwenzako nataka kujaribu hii ya Forever Living, nimeona reviews ni nzuri nataka kujaribu, inaitwa C9
utachukuliwa hela zako bure mchawi wa kitambi ni chakula tuu, hizo dawa wanaita sijui lishe dawa na majina mengine ni namna tuu ya kutafuta hela na ukizingatia tushachanganyikiwa na uzito na vitambi, punguza wanga ama acha kabisa, acha sukari zote, acha pombe zote, tumia zaidi matunda yasiyo na sukari, vyakula vya proten kwa wingi pia mboga za majani
 
lugha za kibiashara alamaarufu propaganda za kibiashara, chamsingi tujifunze zaidi na zaidi
 
tatizo si rahisi avumilie njaa
 
Kula matunda kwa wingi
Vyakula vya wanga usile sana mfn nguna
Kunywa maji mengi
Fanya mazoez
Kula vegetables
Usipende kula nyama na vyakula vya mafuta
Thank me later
maji mengi yanasaidia nini mkuu

kwanini asipende kula nyama na vyakula vya mafuta?
 
Shida ya gym show off nyingi, yaani committed ni mmoja kati ya watano.
 
[emoji134][emoji134][emoji134]wengine tunatafuta kuongezeka matumbo japo kidogo,wengine wanahangaika kupunguza.

Anyways,tumia Detox..ni dawa ya iliyotengenezwa kwa mitishamba..ila ni kali Sana inabidi uvumilie.
Inaleta matokeo mazuri Sana..Kuna ndugu yangu ameitumia na kitambi kimepungua Sana.
 
Sikia.

Tukiwa tunanyanyua vyuma tunakua directed kula protini kwa wingi as protini hunenepesha mwili.

Ndiyo maana supplements nyingi zina protini nyingi sana.

Wanga? Asile wanga? Unajua kama wanga ndiyo inaupa mwili nguvu?
Protein hujenga mwili mkuu sio kunenepesha protein huupa mwili muscles za kutosha na sio kitambi au nyama uzembee.
 
Protein hujenga mwili mkuu sio kunenepesha protein huupa mwili muscles za kutosha na sio kitambi au nyama uzembee.
Jamani niacheni nipumzike. Hii mada nilishaachana nayo kila mtu abaki na anachojua.
 
Ok jitahidi kuji kamua sawasawa huwenda ni mlundikano wa kinyesi tuuh bibie
Kujikamua sswasawa sio salama kiafya yake kwani hupelekea kuzaisha pressure kubwa kutoka ndani kuja nje pressure ambayo inakuwa haina mavi na inaweza kumsababishia maumivu ya ndani ya utumbo mpana mara kwa mara,au ikawa chanzo cha bawasiri
 
Ingia play store download app zipo kibao za kukufundisha mazoezi ndani ya week 2 tu kitamb chote kwisha.zingatia hili hakuna cha dawa wala nn fasta mapema tu unarudi sawa.
Kumbuka mazoez muhimu
 
Nisaidieni dawa ya kupunguza Kitambi ...tumbo langu linazid kuwa kubwa
1. Kwanza kama unaweza kwenda kwa dokta ajue tatizo (wenda inaeza kuwa ni ugonjwa ndio unapelekea uwe na kitambi). Hii ni option na sio lazima kama unajiamini huna ugonjwa.

2. Badilisha ulaji wako (hii ni lazima)

3. Piga zoezi hasa la kukimbia (hii ni lazima).
 
Ungetoa maelezo ya kutosha kuhusu huyo babu rama na dawa yake ya kitambi ingesaidia sn pia kwa wasomaji wnginge
Msidanganyike. Hakuna dawa za kupunguza unene. Sana sana utadanganywa ubugie mavitu yenye madhara. Watu wengi wenye vitamba wanakula sana, tena vyakula vya aina fulani bila kufanya activities za kutosha.
 
Usidanganywe kuwa kuna dawa utauziwa kitambi kikate zaidi zinaweza kuja kukuletea complications.

Siku zote suluhisho la kitambi au ubonge nyanya au kupunguza uzito ni vitu viwili tu ambavyo kila mtu anaweza kufanya.

1. DIET - aina ya vyakula unavyokula na muda unaokula.
2. PHYSICAL ACTIVITIES - mazoezi, kuna aina nyingi za mazoezi kama jogging, aerobics nakadhalika.

Ukiweza kuzingatia hayo mambo utaona mabadiliko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…