Jinsi ya kuondoa au kupunguza mafuta tumboni kwa wanawake (Vitambi vya kike)

Jinsi ya kuondoa au kupunguza mafuta tumboni kwa wanawake (Vitambi vya kike)

Hivi hio procedure sio kwa watu wenye constipation??? mwenzako nataka kujaribu hii ya Forever Living, nimeona reviews ni nzuri nataka kujaribu, inaitwa C9
utachukuliwa hela zako bure mchawi wa kitambi ni chakula tuu, hizo dawa wanaita sijui lishe dawa na majina mengine ni namna tuu ya kutafuta hela na ukizingatia tushachanganyikiwa na uzito na vitambi, punguza wanga ama acha kabisa, acha sukari zote, acha pombe zote, tumia zaidi matunda yasiyo na sukari, vyakula vya proten kwa wingi pia mboga za majani
 
Hiyo ni lugha ya biashara tu mkuu,tathimini iliyotolewa na wataalamu wa magonjwa ya figo na ini inasema kuwa takribani 60+% ya magonjwa ya ini na figo chanzo chake ni madawa ya kienyeji,huku wahanga wakubwa wakiwa watu kutoka katika majiji na Miji mikubwa ambako hawa forever living,Bf suma, nk wamejikita sana,

Jiulize kwanini wagonjwa wasitoke vijijini ambako ndo watu wengi hupenda kutumia dawa za kienyeji?
lugha za kibiashara alamaarufu propaganda za kibiashara, chamsingi tujifunze zaidi na zaidi
 
Badilisha kula Asubuhi kunywa chai muhogo au viazi vitamu 2 kwa wiki moja, mchana kula mbogamboga kiasi kidogo na usiku matunda tu usile chochote ikifika saa 2 usiku. Kwenye wiki moja siku 3 kunywa kilasi 5 za juisi ya malimau(mfano jumamosi hadi jumatano glasi 1 kwa siku)Fanya hivyo kwa wiki halafu lete mrejesho.


Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
tatizo si rahisi avumilie njaa
 
Kula matunda kwa wingi
Vyakula vya wanga usile sana mfn nguna
Kunywa maji mengi
Fanya mazoez
Kula vegetables
Usipende kula nyama na vyakula vya mafuta
Thank me later
maji mengi yanasaidia nini mkuu

kwanini asipende kula nyama na vyakula vya mafuta?
 
Wavivu laiti wangejua miezi miwili ya kwanza tu ndiyo migumu, baada ya hapo results zinaanza kuonekana huwezi kuacha unakua addicted. Hua naona mtu anaenda gym siku mbili miguu inamuuma analia ka mtoto hataki kabisa kurudi [emoji23] Nashangaa sana mtu ambaye hafanyi mazoezi kusema kweli
Shida ya gym show off nyingi, yaani committed ni mmoja kati ya watano.
 
Mimi Ni Ke..Nina tumbo kuubwa, nimejaribu njia Tofauti Tofauti ila sijapata matokeo.

Nlikua nafanya mazoezi na nikipata matokeo chanya ..ila nikashtuka goti..nikifanya mazoezi linauma goti.

Je nitumie.njia gani.mbadala wa mazoezi ili nifikie lengo.
.nakosa confidence na hili tumbo langu.

N.B Picha Siwezi tuma kwa wale wapenda picha.
[emoji134][emoji134][emoji134]wengine tunatafuta kuongezeka matumbo japo kidogo,wengine wanahangaika kupunguza.

Anyways,tumia Detox..ni dawa ya iliyotengenezwa kwa mitishamba..ila ni kali Sana inabidi uvumilie.
Inaleta matokeo mazuri Sana..Kuna ndugu yangu ameitumia na kitambi kimepungua Sana.
 
Sikia.

Tukiwa tunanyanyua vyuma tunakua directed kula protini kwa wingi as protini hunenepesha mwili.

Ndiyo maana supplements nyingi zina protini nyingi sana.

Wanga? Asile wanga? Unajua kama wanga ndiyo inaupa mwili nguvu?
Protein hujenga mwili mkuu sio kunenepesha protein huupa mwili muscles za kutosha na sio kitambi au nyama uzembee.
 
Protein hujenga mwili mkuu sio kunenepesha protein huupa mwili muscles za kutosha na sio kitambi au nyama uzembee.
Jamani niacheni nipumzike. Hii mada nilishaachana nayo kila mtu abaki na anachojua.
 
Ok jitahidi kuji kamua sawasawa huwenda ni mlundikano wa kinyesi tuuh bibie
Kujikamua sswasawa sio salama kiafya yake kwani hupelekea kuzaisha pressure kubwa kutoka ndani kuja nje pressure ambayo inakuwa haina mavi na inaweza kumsababishia maumivu ya ndani ya utumbo mpana mara kwa mara,au ikawa chanzo cha bawasiri
 
Ingia play store download app zipo kibao za kukufundisha mazoezi ndani ya week 2 tu kitamb chote kwisha.zingatia hili hakuna cha dawa wala nn fasta mapema tu unarudi sawa.
Kumbuka mazoez muhimu
 
Nisaidieni dawa ya kupunguza Kitambi ...tumbo langu linazid kuwa kubwa
1. Kwanza kama unaweza kwenda kwa dokta ajue tatizo (wenda inaeza kuwa ni ugonjwa ndio unapelekea uwe na kitambi). Hii ni option na sio lazima kama unajiamini huna ugonjwa.

2. Badilisha ulaji wako (hii ni lazima)

3. Piga zoezi hasa la kukimbia (hii ni lazima).
 
Ungetoa maelezo ya kutosha kuhusu huyo babu rama na dawa yake ya kitambi ingesaidia sn pia kwa wasomaji wnginge
Msidanganyike. Hakuna dawa za kupunguza unene. Sana sana utadanganywa ubugie mavitu yenye madhara. Watu wengi wenye vitamba wanakula sana, tena vyakula vya aina fulani bila kufanya activities za kutosha.
 
Usidanganywe kuwa kuna dawa utauziwa kitambi kikate zaidi zinaweza kuja kukuletea complications.

Siku zote suluhisho la kitambi au ubonge nyanya au kupunguza uzito ni vitu viwili tu ambavyo kila mtu anaweza kufanya.

1. DIET - aina ya vyakula unavyokula na muda unaokula.
2. PHYSICAL ACTIVITIES - mazoezi, kuna aina nyingi za mazoezi kama jogging, aerobics nakadhalika.

Ukiweza kuzingatia hayo mambo utaona mabadiliko.
 
Back
Top Bottom