Jinsi ya kuondoa au kupunguza mafuta tumboni kwa wanawake (Vitambi vya kike)

Jinsi ya kuondoa au kupunguza mafuta tumboni kwa wanawake (Vitambi vya kike)

Najaribu kuheshimu ombi lako kuwa unataka kujua dawa za kichina... lakini naomba niseme; kama unatafuta njia ya mkato utapungua lakini pia utaongezeka tena!! Wengi humu wamelisema hilo... unless tatizo ni constipation, hizo dawa za kichina hazibadilishi mahesabu ya unachoingiza (chakula) vs. unachotumia au kutoa (nguvu/energy) katika maisha ya kila siku. Dawa za kichina na GNLD mimi nina best ametumia na na baada ya kushindwa kumudu hiyo regimen akarudisha uzito woooote na kuongeza kilo zaidi.

Watanzania, tufanyeni mazoezi na kula kwa kiasi. Dunia ya leo kitambi ni ugonjwa na tumeelimika kujua hilo... tunasubiri nini? basi tukutane Leaders au gymn kwa mazoezi ya viungo!

Wakuu naomba kujua wapi naweza kupata majani ya chai kwa ajili ya kupunguza kitambi.

nasikia kuna chai za kichina ukinywa tumbo linapungua.

nipo jijini dsm.

achana na mambo kichina kaka tiba ya hiyo ki2 ni mazoezi na kupunguze kula kula ovyo

Jamani, achaneni kabisa na habari za dawa za kichina, mimi mwenyewe nimekunywa nikapunguaa vizuuuuri, ila loh! baada ya muda mwili umerudi wooooote na zaidi ya ule niliokuwa nao, kikubwa ni kucontrol fat na mazoezi, utazoea tu

CHANZO CHA VITAMBI, UZITO NA UNENE KUPITA KIASI NA NAMNA UWEZAVYO KUDHIBITI TATIZO HILI BILA DAWA:

Mfumo mkuu wa fahamu katika ubongo hutambua kushuka kwa kiasi cha nguvu kinachopatikana kwa ajili ya matumizi yake.

Hisia za kiu au njaa pia hutokea kunapotokea kupungua kwa nguvu mwilini.

Ili kuiamsha nguvu toka katika mafuta yaliyohifadhiwa, kunahitajika mwingilio maalumu wa ki-homoni. Zoezi hili huchukuwa muda mrefu zaidi (na pengine mazoezi zaidi kwa mishipa huhitajika) kuliko udharura wa uhitaji wa nguvu unavyohitajika na ubongo.

Sehemu ya mbele ya ubongo hupata nguvu ama kutoka katika nguvu inayozarishwa kwa nguvu za maji au kutoka katika sukari kwenye mzunguko wa damu. Nguvu zitokanazo na maji huhitajiwa kwa dharura zaidi siyo katika kuzarisha nguvu tu, bali hata katika mifumo yake ya usafirishaji ambayo hutegemea maji zaidi.

Kwa hiyo hisia za kiu na njaa huja kwa pamoja kuonesha mahitaji ya ubongo. Hatuzitambui hisia za kiu, na tunazichukulia hisia zote kuwa ni hitaji la kula. Tunakula chakula hata wakati mwili unapotakiwa upokee maji. Watu waliopunguza uzito wao kwa kunywa maji kabla ya kula, wamefanikiwa kuzitofautisha hisia hizi mbili. Hawakula kuzidi ya kipimo kuituliza kiu ya mwili kwa maji.

Hata hivyo, watu wengi sana kote duniani huwa hawafuatilii lolote kuhusu uzito wao. Uzito uliozidi ni ugonjwa na ni hatua ya kwanza katika kuporomoka kwa mwili wa binadamu. Kila mmoja anapaswa kujua kama uzito alionao unafaa kwa mwili wake au la.

Kwanini watu wanakula sana?

Ubongo wa binadamu una ukubwa kama 1/50 ya uzito wa mwili. Inasemwa, ubongo una seli neva kama tilioni 9 (kama chipu za kompyuta). Inasemwa, zaidi ya asilimia 85 ya seli za ubongo, ni maji.

Asilimia 20 ya damu yote mwilini imeelekezwa na inapatikana kwa ajili ya ubongo. Hii inamaanisha ubongo unahitajika kuchukua kila unachokihitaji kwa ajili ya kazi zake toka katika mzunguko wa damu.

Ubongo ni moja kati ya ogani pekee za mwili ambazo hufanya kazi muda wote hata katika usingizi mzito, huzishughurikia taarifa zote toka katika maeneo mbalimbali ya mwili na zile zinazouingia toka katika mazingira, jamii na hata zile toka mazingira ya ki-usumaku.

Katika kushughurikia kazi zote hizo, ubongo hutumia kiasi kikubwa sana cha nguvu. Wakati huo huo ubongo hutumia nguvu katika kutengeneza mahitaji ya mwanzo na jumbe kemikali (chemical messengers) ambazo zimetengenezwa toka seli za ubongo na ambazo zinatakiwa kusafirishwa kwenda miishio ya neva kuzunguka mwili.

Mfumo wa usafirishaji mwilini hutumia pia kiasi kikubwa cha nguvu. Kiasi hiki kikubwa cha matumizi makubwa ya nguvu yanayofanywa na ubongo ndiyo sababu ya ubongo kutengewa asilimia 20 ya mzunguko wa damu.

Seli za ubongo huhifadhi nguvu zake katika mifumo miwili. Stoo yake ya kwanza inaitwa Adenosine Triphosphate (ATP), na ya pili inaitwa Guanosine Triphosphate (GTP).

Baadhi ya maswali maalumu hujibiwa na nguvu zilizohifadhiwa toka stoo ya kwanza (ATP) ambayo inapatikana katika maeneo mbalimbali ya seli hasa katika kuta zake. Kwenye ukuta wa seli (cell membranes) ndiko ambako taarifa huingilia na ndiko ambako majibu huanzishwa.

Kuna mfumo wa mgawo wa 'nguvu' ambao hufanya kazi muda wote katika seli. Siyo madokezo yote ya maswali yanaweza kufanikiwa kupata majibu toka katika stoo ya nguvu ya kwanza (ATP).

Kuna vikwazo katika uelekezwaji wa nguvu kwa baadhi ya maswali. Ubongo unakokotoa na kukielewa kipi ni cha mhimu na kipi si cha mhimu katika bajeti yake ya nguvu.

Wakati inapopungukiwa nguvu stoo ya kwanza, baadhi ya madokezo hayapati majibu. Kupunguwa huku kwa nguvu toka stoo ya kwanza kwa baadhi ya seli za ubongo, kunatokea kujionesha kama hali ya uchovu katika baadhi ya kazi zinazosimamiwa na seli hizo.

Vivyo hivyo, matendo hayo hutokea pia kwa stoo ya pili ya nguvu (GTP). Katika baadhi ya matendo maalumu ya dharura, baadhi ya nguvu toka stoo ya pili inaweza kuelekezwa kuiongezea nguvu stoo ya kwanza kwa madokezo maalumu kushughurikiwa.

Hifadhi ya nguvu katika maghala ya nguvu za ubongo, inaonekana kutegemea zaidi upatikanaji wa sukari mwilini. Muda wote ubongo unachukuwa sukari toka katika damu ili kuyajaza maghala yake (ATP na GTP).

Hivi karibuni imegundurika kuwa, mwili unao uwezo wa kutengeneza nguvu kwa kutumia maji (hydroelectric energy), wakati maji peke yake yanapoingia kupitia kuta za seli na kuwasha pampu maalumu za majenereta ya kuzarishia nguvu yaitwayo kwa kitaalamu, 'cation pumps', ni kama vile bwawa la umeme linapojengwa karibu na mto mkubwa.

Kwa hiyo ubongo hutumia mifumo miwili kwa ajili ya mahitaji yake ya nguvu, wa kwanza ni ule wa kiumetaboli wa chakula na kuunda sukari,na wa pili unahusisha matumizi ya maji kuzariha nguvu umeme zitokanazo na maji (hydroelectric energy).

Inajionesha wazi sasa kwamba ubongo unategemea zaidi nguvu zitokanazo na umeme wa maji hasa katika mifumo yake ya usafirishaji kwenye neva zake kwenda sehemu mbalimbali za mwili.

Ili kuhimili mahitaji ya ubongo, mwili umekuza mfumo maalumu ili kutunza kiasi cha kawaida cha sukari katika mzunguko wa damu. Hufanya hivyo kwa njia mbili, ya kwanza ni ile ya kusisimua ulaji wa vyakula vyenye protini na wanga ambavyo vitabadilishwa kuwa sukari ikijumuisha pia sukari yenyewe katika mlo, njia ya pili ni ya kubadili wanga na protini toka katika hifadhi ya mwili na kuwa sukari. Njia hii ya pili huitwa kitaalamu kama 'Gluconeogenesis', yaani utengenezwaji wa sukari toka katika malighafi zilizohifadhiwa. Utengenezaji wa aina hii wa sukari hufanyika katika Ini.

Utegemezi wa sukari kwa kazi nyingi zifanywazo na ubongo, kumepelekea mapenzi kwa vyakula vyenye radha ya utamu. Mwili umekuza mfumo kanuni maalumu, uunganikaji wa kazi na ogani zingine hasa Ini wakati radha ya utamu inaposikika katika ulimi.

Inapotokea hakuna sukari ya kutosha katika mzunguko, Ini huanza kuitengeneza na kuijaza kwenye usawa wa damu. Mwanzoni litaanza na wanga uliokuwa umehifadhiwa ukifuatiwa na protini na kiasi kidogo cha mafuta. Ubadilikaji wa mafuta kuwa sukari huchukuwa muda mrefu zaidi.

Mwili unahitaji kubaki bila chakula kwa muda fulani kabla kiasi kikubwa cha umetaboli wa mafuta hakijaanzishwa.

Protini hupatikana kiurahisi zaidi na umetaboli wake ni mrahisi zaidi kuliko mafuta. Dipositi za mafuta zimetengenezwa kutokana na yuniti nyingi mbalimbali za asidi mafuta ambazo zimeungana pamoja. Asidi mafuta za mtu ndizo huvunjwa (humeng'enywa) kwa ajili ya thamani yake kwa nguvu ya mwili.

Kila gramu 1 ya mafuta hutoa kalori 9 za nishati, kila gramu 1 ya protini au sukari hutoa kalori 4 za nishati. Hii ndiyo sababu mafuta yanapotumika kuzarisha nguvu, mtu hajisikii sana njaa.

Kwa watoto, stoo za mafuta zina rangi ya kahawia na zina mzunguko zaidi wa damu. Kwenye mafuta ya rangi ya kahawia, mafuta yanameng'enywa moja kwa moja na nguvu hutengenezwa. Baada ya miaka kadhaa baadaye, stoo za mafuta huwa na mizunguko michache ya damu na uwezekano mdogo wa kuvifikia vimeng'enya vinavyozihamasisha asidi mafuta kwa mabadiliko yake kwenye ini na mishipa.

Wakati mwili unapokuwa legelege, mishipa hushambuliwa kirahisi zaidi na protini yake humeng'enywa na kufanywa sukari. Ingawa, ikiwa mishipa inashuhulishwa, itaanza kumeng'enya baadhi ya mafuta yake yaliyohifadhiwa na kuyatumia kama chaguo la chanzo chake cha nguvu katika kufanya kazi na kuutunza au kuuongeza ujazo wake.

Ili kufanya hivyo, mishipa hukiamsha kimeng'enya chake cha mafuta, homoni iitwayo kwa kitaalamu 'lipase'.

Imedhihirika katika majaribio ya kujirudia huko nchini Sweden kwamba kimeng'enya hiki cha kuchoma mafuta huamka baada ya mwendo wa miguu wa saa moja MFULULIZO, na huendelea kumeng'enya mafuta kwa muda wa masaa 12.

Kwa hiyo ikiwa mtu atatembea kwa muda wa saa moja mara mbili kwa siku, atakuwa amekiamsha kimeng'enya (enzyme) hiki kufanya kazi kwa masaa 24 (siku nzima)!.

Kuendelea kutembea zaidi, ndivyo kimeng'enya hiki kinavyoendelea kujitokeza zaidi, kwa hiyo fungu lolote la mpango wa mlo lazima liegemee zaidi upande wa mahitaji ya mishipa kwa ajili ya matokeo ya muda mrefu ya moja kwa moja ya kifiziolojia katika kumeng'enywa kwa mafuta.

Ni kimeng'enya hiki hiki (lipase) kwenye mzunguko wa damu ambacho huisafisha mishipa dhidi ya mabaki ya mafuta, cholesteroli na dipositi zake.

Hivi ndivyo ilivyo rahisi kupunguza uzito na unene bila nguvu wala gharama yeyote!. Anza leo, tembea saa moja kutoka kituo A mpaka kituo B bila kupumzika KWA SAA MOJA, ITABIDI UWE NA SAA KABISA MKONONI asubuhi na jioni, baada ya wiki mbili pima tena uzito wako kuona namna ulivyofanikiwa kwa muda huo na muda gani uwekeze tena kumaliza tatizo hili linalosumbuwa watu wengi kote duniani.

Kumbuka pia kunywa maji kila nusu saa kabla ya kula.

Kazi zinazofanywa kwa kukaa (maofisini) katika maisha yetu ya kisasa, ni kipindi cha mabadiliko ya kiutamaduni. Fiziolojia ya miili yetu bado haijabadilishwa vya kutosha kuwezesha matumizi yasiyo ya kawaida ya mwili wa binadamu. Mwili bado unahitaji kushughulishwa kwa mishipa ili kuhimili hali ya kawaida ya kazi zake.

Ikiwa mwili unaendesha kazi zake katika hali yake ya kawaida, utaelewa ni muda gani wa kula na kwa kiasi gani bila kuizidisha hifadhi ya mafuta. Kila sehemu ya mwili itatumia kiasi chake cha nguvu iliyotengewa kwa ufanisi na kazi zinazoendeshwa vizuri zaidi. Hivi ndivyo mwili ulivyosanifiwa.

Ingawa, ikiwa ubongo umetumika zaidi (wakati wa mfadhaiko kwa mfano) na mwili haujatumika kwa uwiano huo huo kuusambazia ubongo mahitaji yake ya sukari, mtu mwenye uelewa mdogo ataangukia kwenye kula zaidi mara nyingi na kwa kiasi kikubwa.

Inashangaza zaidi inapotokea tunashindwa kuzielewa ishara za mwili unapoyahitaji maji kwa ajili ya mahitaji yake ya kusambaziwa nguvu, na badala ya kunywa maji, tunakimbilia kula zaidi.

Katika mfadhaiko (stress), mwili unakuwa umepungukiwa maji (dehydrated).

Sababu ya kwanini inatokea kuongezeka uzito ni rahisi. Tunakula ili kuusambazia ubongo mahitaji yake ya nguvu kwa ajili ya kazi zake masaa 24.

Kama ilivyofafanuliwa, mwili una vyanzo vitatu vya nguvu: Sukari, Mafuta na Maji/chumvi.

Hata hivyo, wakati chakula kimeliwa, ni karibu asilimia 20 tu za chakula ndizo hutumika na ubongo, sehemu inayobaki huhifadhiwa taratibu ikiwa shughuli za mishipa (mazoezi) hazitumiki kutumia kiasi chake cha chakula iliyotengewa.

Maji yanapotumika kama chanzo cha nguvu, stoo hii ya kuhifadhia sehemu iliyobaki ya chakula, haitokei, maji yanayozidi hutolewa nje kupitia mfumo wa mkojo.

Wakati mwingine utakaposikia njaa kati ya chakula cha asubuhi, cha mchana au cha jioni, badala ya kukimbilia kula chakula, chukua maji kunywa nusu yake kisha tafuna chumvi na umalizie maji yaliyokuwa yamebaki na kisha usubiri kwa muda wa dakika 20 na uone kama utaendelea kujisikia njaa. Zaidi ya asilimia 90 ya njaa yako itakuwa imepotea, hii ilikuwa ni namna ya ubongo wako kukuambia kuwa unahitaji maji.

Ubongo hauwezi kutuma ishara tofauti za njaa na kiu, ishara zote hutumwa kwa pamoja, hatuzitambui ishara za kutaka kunywa maji na badala yake tunakimbilia kula hata wakati mwili unahitaji maji.

Kujuwa zaidi namna ya kuyanywa maji kama tiba, waweza kunitumia sms tu katika namba 0769779533.

Kumbuka pia kuwa hii ni elimu tu na siyo kumuondoa daktari wako au chaguo lako la kutumia dawa, ni programu iliyopendekezwa kwa manufaa yako.

Changanya mdalasini kijiko kimoja, pilipili manga nusu kijiko, iliki unga nusu kiijiko, tangawizi unga nusu kijiko, ukwaju fumba, Chai i Kilimanjaro kijiko kimoja, mwarubaini maji nusu kikombe na pilipili kichaa nusu kikombe. Weka maji vikombe viwili chemsha na kunywa kijiko kikubwa kutwa mara mbili.:deadhorse:
hahahahahah mndee acha fix sasa bro upige pilipil kichaa nusu kikombe si unadanji fasta

umetisha kwa elimu mkuu....... zoezi kuanzia leo.

jogging ,kuruka kamba,push ups na squats moja,mbli punguza vyakula vya wanga,bia na vinywaji vyenye sukari nyingi,TUMIA mdalasini,asali,kunywa maji ya moto,kunywa maji mengi,matunda ,mbogamboga kwa wingi HUYO NDO MCHINA WA KWELI

Mkuu Fadhili bravo...umeshafikiria kuwa unaandika makala kwenye magazeti ya kiswahili mada moja baada ya nyingine, itasaidia sana watu!

Tumia Forever Living products kama Aloe Vera Gel ya kunywa na kuna vidonge maalum tunavyo.

Approved by World Scientific Laboratory, no side effects.

Mimi mwenyewe nimetumia

Mimi ni Approved Distibuter.

Na wewe pia unaweza kuwa distributor kama unapenda

Visit traveltipsam.blogspot.com

or NI PM

Umekaa kibiashara zaidi wewe....

rafiki yangu kungekuwa na chai ambayo unachemsha tu kisha unakaa sebuleni kwako ukinywa huku unabadili channel za Dstv, na bado kitambi kinaisha...kusingekuwa na mtu mwenye kitambi duniani.

Am afraid huna jinsi...kama kweli hukitaki hicho kitambi, na una nia ya kukitoa...no good news other than diet and exercise, tena sio exercise ya kitoto...hard and regular exercise!

Umekaa kibiashara zaidi wewe....

rafiki yangu kungekuwa na chai ambayo unachemsha tu kisha unakaa sebuleni kwako ukinywa huku unabadili channel za Dstv, na bado kitambi kinaisha...kusingekuwa na mtu mwenye kitambi duniani.

Am afraid huna jinsi...kama kweli hukitaki hicho kitambi, na una nia ya kukitoa...no good news other than diet and exercise, tena sio exercise ya kitoto...hard and regular exercise!

umeona ee! Hakuna shirt cut. Tatizo watu ni wavivu sana. Hakuna chai ya mchina wala forever living! Amka alfajiri nenda ukakimbie. Ukirudi fanya push ups na sit ups. Acha kula mifuta, wanga na sukari. Habari ndo hiyo.

Wakuu naomba kujua wapi naweza kupata majani ya chai kwa ajili ya kupunguza kitambi.
nasikia kuna chai za kichina ukinywa tumbo linapungua.
nipo jijini dsm.

unapenda dawa za kichina eeeh? hongera! najua ukifanikiwa utaanza kuulizia na dawa ya kuongeza makalio umpelekee mkeo au uitumie mwenyewe!!

Hii ni makala njema sana mkuu na hasa kwetu wenye miili inayoelekea 'kuporomoka', Thx na nitajitahidi kutembea saaa mbili kila siku ila sitaanza leo

Ok tayari baadhi ya watu wame ni PM kwa ajili ya dawa za kupunguza kitambi

Safi, mwingine kupunguza tumbo na unene

KAKA NITUPIE NA MIE KWENYE PM MAANA NAHITAJI SAna

Wakuu naomba kujua wapi naweza kupata majani ya chai kwa ajili ya kupunguza kitambi.
nasikia kuna chai za kichina ukinywa tumbo linapungua.
nipo jijini dsm.
Hayo majani yanaitwa green tea na unakunywa bila kuweka sukari na nivema ukanywa every time yaani ikawa ndo juice yako au maji yako ya kunywa, inasaidia sana kupunguza cholestrol mwilini na ina anti-oxidant kwa wingi ambayo hupambana na free radicals ambazo ni visababishi vya cancer pia, pia ni anti bacterial nzuri hata kwa kulinda fizi.

So kwa dar nenda kwenye super market kama shoprite utakuta ila kwa mie huwa nachukulia kwenye restaurant za wachina we ukienda waambie unataka chinese green tea wanazo wanaweza kukuuzia kishkaji au wakachukua oda yako wakakwambia njoo siku flani utapata. Au tuma hawa wafanyabiashara wanaokwenda china wakuletee kama kuna unaemjua.

Its very nice drink especially kwa afya na kwa sababu ya faida zake za kiafya ndo maana chinese, japanese na koreans wamekifanya kinywaji hiki kuwa kama culture yao pili mtu atembelewapo na mgeni au hata unapoenda kwenye ofisi unapewa hicho kinywaji. Sisi mgeni akija unampa soda yaani unamuongezea matatizo juu ya yale aliyonayo.

Ni kinywaji ambacho waweza kunywa kikiwa baridiiii, vuguvugu au moto ni wewe tu. na kuna grades zake so unapoagiza ujue unaagiza grade ipi.
Hope nimekupa ABC ya swali lako

Jamani, achaneni kabisa na habari za dawa za kichina, mimi mwenyewe nimekunywa nikapunguaa vizuuuuri, ila loh! baada ya muda mwili umerudi wooooote na zaidi ya ule niliokuwa nao, kikubwa ni kucontrol fat na mazoezi, utazoea tu

Kauliza majani hajauliza dawa! Majani ndio yapo na ni green tea na hata hapa kwetu bongo yanalimwa na yako packed nenda supermarket shoprite utakuta ila kinachotofautisha ni kuwa hapa kwetu bongo hayawekwi kwenye grade mbalimbali ila kwa wachina, wakorea na wajapan wao wameyaweka katika grades mbalimbali na yanalimwa under organic farming kitu ambacho kinaongezea ubora zaidi. Sio dawa ni majani ya chai tu

Back
Top Bottom