1. Tengeneza juice ya ukwaju pure (uchemshe na usiweke sukari au asali) na kunywa asubuhi kabla ya kula chochote. Ukiweza kunywa na jioni. Utaharisha. Komaa na hii kitu kwa hata miezi miwili. Kama upo Dar, ukwaju unapatikana masokoni kama Kkoo, Mwenge, Mabibo.
2. Punguza au acha kabisa kutumia sukari (chai, soda, juice za hotelini ambazo zimejaa sukari, pombe iliyozidi etc)
3. Anza kula nusu ya kiasi cha chakula unachokulaga normally (chapati moja instead of 2, mpakuo mmoja wa wali instead of 2, nusu ya samaki badala ya mzima etc etc)
4. Zidisha unywaji wa maji
5. Fanya mazoezi simple. Kama huwezi kujog, tembea. Kama huwezi kutembea, fanya home. Download app za mazoezi. Mimi natumia Nike Training (NTC) ipo kwa Android na Apple as well
Kila la kheri!