Jinsi ya kuondoa au kupunguza mafuta tumboni kwa wanawake (Vitambi vya kike)

Mtu kua na kitambi tafsiri yake kwamba anafikiri chini ya kiwango anachostahiri .Huyo mtu ni mvivu na mwenye kupenda kula bila ratiba maalumu.
 
Nisaidieni dawa ya kupunguza Kitambi ...tumbo langu linazid kuwa kubwa
Yaani asikudanganye mtu hakuna dawa ya kupunguza unene,zaidi ya kibadilisha mtindo wa maisha yako. mfano angalia style ya ulaji wako na aina ya vyakula na saa ngapi. Mfano siyo unakulakula hovyo tuu na ukila unahakikisha mahotpot yote yamekauka.inatakiwa ujue unahitaji kula pale unahisi kula.Kiufupi ukijitafakari utajikuta ulaji na unywaji wako hauko sawa.Na hii inatakiwa kuwa ni tabia.

labda tuelezee kiufupi ratiba ya msosi kwako ikoje?
 
Swala la kitambi ni mwiba unaochoma vibaya mno hasa endapo mwili ushakuwa mzito hata mazoezi ni ishu.

Kibaya zaidi vyakula vyote vitamu na vinono eti hutakiwi uvile ndio vinaleta kitambi. Sasa kweli mtu uache ugali nyamachoma kweli? Hebu tafakari tu kitimoto roast na ugali ndio kitu cha kukiacha kweli?

Chips kuku na Pepsi baridii vinaleta burudani ya pekee tumboni. Af anatokea mtu anakwambia ule papai na mchicha. Hii ngoma ngumu😁😁😁 haswaa!
 
Swala la kitambi ni mwiba unaochoma vibaya mno hasa endapo mwili ushakuwa mzito hata mazoezi ni ishu.

Kibaya zaidi vyakula vyote vitamu na vinono eti hutakiwi uvile ndio vinaleta kitambi. Sasa kweli mtu uache ugali nyamachoma kweli? Hebu tafakari tu kitimoto roast na ugali ndio kitu cha kukiacha kweli?
Noma sana, yataka maamuzi makali 😂
 
Ingia play store download app zipo kibao za kukufundisha mazoezi ndani ya week 2 tu kitamb chote kwisha.zingatia hili hakuna cha dawa wala nn fasta mapema tu unarudi sawa.
Kumbuka mazoez muhimu
Kitambi HAKIWEZI KUISHA ndani ya wiki mbili mkuu, Labda kama tumbo limejaa gesi (Bloated).

Kumaliza kabisa kitambi inategemea sana na level ya kitambi ulichonacho na inaweza chukua miezi mpaka miaka.
 
Yaani asikudanganye mtu hakuna dawa ya kupunguza unene,zaidi ya kibadilisha mtindo wa maisha yako. mfano angalia style ya ulaji wako na aina ya vyakula na saa ngapi. Mfano siyo unakulakula hovyo tuu na ukila unahakikisha mahotpot yote yamekauka.inatakiwa ujue unahitaji kula pale unahisi kula.Kiufupi ukijitafakari utajikuta ulaji na unywaji wako hauko sawa.Na hii inatakiwa kuwa ni tabia.

labda tuelezee kiufupi ratiba ya msosi kwako ikoje?
HAKUNA kudanganyana Kama ingekuwa Ni kupunguza mlo TU wasingekuwa wanakwenda fanyiwa upasuaji mkuu
 
Af nimegundua kutembelea gari ndio kunalemaza zaidi yani kama appetite yako iko juu ndani ya miezi kadhaa ushakua rick ross
Kweli, hata boda pia lawama. Mi ka ni mwendo mfupi, bora nitembee tu, ni save hiyo hela na bado na keep fit. Ukiwa mtumiaji wa gari sana sana, hutajua ukinenepa, ni ile pap ushafura ka hamri na shida huwezi piga zoezi 😂
 
Kitambi HAKIWEZI KUISHA ndani ya wiki mbili mkuu, Labda kama tumbo limejaa gesi (Bloated).

Kumaliza kabisa kitambi inategemea sana na level ya kitambi ulichonacho na inaweza chukua miezi mpaka miaka.
Hizi nyama za kando, za tumbo, kuzimaliza ni miaka tena hapo daily mazoezi intense
 
Kitambi HAKIWEZI KUISHA ndani ya wiki mbili mkuu, Labda kama tumbo limejaa gesi (Bloated).

Kumaliza kabisa kitambi inategemea sana na level ya kitambi ulichonacho na inaweza chukua miezi mpaka miaka.
Kinaweza Isha kwa wiki1,2au 3 kulingana na tiba lishe utakayo tumia.nilikuwa na kitambi Kama nimebeba pipa ndani ya tumbo baada ya kujilisha tibalishe kiliisha ndani ya wiki mbili TU na Sasa nafurahia maisha ya bila kitambi
 
Fanya mazoezi yapo mengi tu,ingia YouTube utajifunza na ukiwa serious utafanikiwa

NB:Hakuna dawa ya kupunguza kitambi, unajiletea shida tu hapo baadaye....
 
Kweli, hata boda pia lawama. Mi ka ni mwendo mfupi, bora nitembee tu, ni save hiyo hela na bado na keep fit. Ukiwa mtumiaji wa gari sana sana, hutajua ukinenepa, ni ile pap ushafura ka hamri na shida huwezi piga zoezi 😂
Mie nimeliacha kwa muda maana nilijaa kama Puto, af i was aging fast kabla ya umri 😁
 
Kuna jamaa yangu alianza program ya kuondoa kitambi, alipunguza mlo na kufanya mazoezi....akaishia kuwa mwembaba lakini kakitambi bado kamechomoza, anakuwa kama ameficha kofia ya Pikipiki tumboni.
Hahah
 
Kinaweza Isha kwa wiki1,2au 3 kulingana na tiba lishe utakayo tumia.nilikuwa na kitambi Kama nimebeba pipa ndani ya tumbo baada ya kujilisha tibalishe kiliisha ndani ya wiki mbili TU na Sasa nafurahia maisha ya bila kitambi
Mkuu ni Either unadanganya au haujui unachokisema Lakini kitambi hakiishi ndani ya wiki
 
Back
Top Bottom