Jinsi ya kupata kazi za remote katika mashirika ya kimataifa yaliyo nje

Mjomba, kila kitu kinafaa kwa wakati wake.
Huwezi kula tunda muda wote.

Na huwezi fanya kazi muda wote.

Vyote muhimu lkn kwa wakati wake.

Hawa wajumbe humu, ndio hawa hawa wachangiaji kwa uzi wa kimasihara pia😂😂
Hahahahaha..!!!
 
Watu wengi humu wana stress za TGS na wengine ni jobless.

Akisikia mtanzania mwenzie analipwa pension yake ya uzeeni kwa miezi miwili tu basi roho inaumuuma na kumfukuta.

Sema ndio life.
Yaani kwa kweli, unashangaa mtu ana comment kwa hasira kweli kweli. They should just take a chill pill.
 
Leo ningependa kuzungumzia namna kijana yoyote wa Kitanzania ambae una utaalamu na/au ujuzi katika eneo fulani unavyoweza kupata kazi katika mashirika na makampuni ya kimataifa yaliyopo popote duniani na kuweza kufanya kazi remotely ukiwa hapa hapa nchini. Kwa mfano mimi nafanya kazi katika mradi wa kimataifa; makao makuu yao yako USA, lakini mimi nafanyia hapa hapa bongo. Kupata hii nafasi nilishindana na watu kutoka ataifa mbalimbali kama vile USA, Ehtiopia, Nigeria, na Kenya. Nilifanya raundi tano, nakumbuka hadi raundi ya mwisho tulibaki mimi na jamaa mwingine wa kutoka Ethiopia. Hivyo, inawezekana kabisa hata wewe kijana wa Kitanzania ukapata kazi za namna hii, you just have to be competent, and know where to look. Kufanya kazi remote kuna faida kubwa sana, kwani ukiacha kutokua na mizunguko ya kwenye magari/daladala kila siku asubuhi na jioni, pia unakua unalipwa kwa dola za Kimarekani, wakati wewe matumizi unafanya kwa pesa za madafu (Tshs), hakuna kitu kizuri kama kulipwa kwa $$ halafu unafanya matumiz kwa Tshs.

Nitaongelea kila kitu hapa hapa jukwaani, yeyote mwenye swali aliweke hapa hapa, nitalijibu hapa hapa, nitamaliza kila kitu kwenye uzi huu huu, hakuna cha PM wala wapi.
NItaongelea platforms ambazo unaweza pata kazi hizi, pamoja na nini ufanye ili uweze kuji position na kuwa competitive katika kupata hizi kazi.

Kitu cha kwanza kabisa ambacho ni muhimu kuliko vyote, lazima uwe VIZURI SANA kwenye kazi yako, yaani you have to be one of the best...!! Uwe COMPETENT kweli kweli, maana hizi nafasi unakwenda kushindana na mashine kutoka Nigeria huko, Kenya, USA, na kadhalika...! Na hao watu wako nondo kweli kweli, they do not joke, so na wewe inabidi uwe level hizo za hali ya juu! Ukienda kichwa kichwa, hata ukifanikiwa kuitwa interview utambwela balaa hadi utajiona bonge la kilaza!

1. Andaa resume yako na iwe imenyooka, iwe katika mfumo ambao ni very competitive. Kuna tools nyingi sana za kuandaa resume yako na kuifanya competitive. Kwa mfano, Canva:https://www.canva.com/resumes/templates/professional/; Novoresume, Free Resume Templates for 2024 [Download Now]
Ni muhimu sana uandae resume yako iwe ya kibabe kabisa, sio unaandaaa resume ya kichovu, hutafika popote katika competition ya kimataifa.

2. Hakikisha unakua na a very STRONG ONLINE PRESENCE: Unataka kufanya kazi remote na mashirika ya kimataifa halafu hata hauijui LinkedIn? Bro, are you serious? Kama hauna account LinkedIn, baada tu ya kusoma hii post, kitu cha kwanza unatakiwa kufanya haraka sana ni kwenda LinkedIn, kujisajili kule na kuhakikisha una profile very strong (5 star profile), baada ya hapo hakikisha unaomba connection na watu walio katika industry yako una connect nao as many as possible. Kisha, mdogo mdogo anza kupost masuala yanayohusiana na kazi yako au vitu unavyovifanya. Are you a tech wizard and you are working to solve a challenge through technology? Why not post what you are doing there? Are you employed somewhere and today you had a workshop with some stakeholders to discuss on something? Why not share over LinkedIn with some nice photos? Pamoja na LinkedIn, pia kuna platform zaingine kulingana na industry yako, mfano watu wa tech wana zile platform zao ambazo zinakua na communities, wana discuss ma solution, na ma code; wewe ni programer, kwa nini usijiunge huko?
Niwaambie kitu, hii kazi yangu niliyoipata, mimi hata sikuiomba, I was just contacted on LinkedIn na mtu ambae yupo huko, akaniambia kuna nafasi huku nilipo naona inakufaa sana based on what you have been sharing here on LinkedIn, akaniambia kama nipo interested aniunganishe na recruiter wao, ikawa imeisha hiyo.

3. Ongeza zaidi ujuzi wako:
Sawa, umemaliza degree ya Information, Communication, and Technology hapo UDSM; Lakini je, una nini cha ziada? Kuna platforms kama Coursera, Udacity wanatoa courses fupi fupi katika maeneo tofauti tofauti- Zipo za bure na za kulipia, anza na zile za bure angalia ipi itakuongezea kitu, zipige nyingi nyingi.... Ukijipanga pia ukapiga hata na zile za kulipia kwa kutoboka kidogo mfuko sio mbaya, YES. Kama unaweza kutoa hadi shilingi 150,000 - 200,000 kugharamia kumgonga demu why not usitumie gharama inayokaribiana na hiyo kujiongezea ujuzi na skills ambazo zitakusaidia pia? Pia, usisahau YOUTUBE kuna madini ya kutosha kule, bure kabisa. Badala ya kupoteza bundle lako kuangalia umbea wa insta, ingia kule ucheki madini ujiongezee SKILLS. Niwaambie tu, dunia ya sasa hivi skills na ujuzi wako ni muhimu sana sana, usije ukaingia kwenye mtego wa kukusanya vyeti huku huna unacho-gain...!! Mimi hadi nimepata hii kazi ya remote, hawajawahi kuniambia hebu tuone vyeti vyako hata mara moja..!! Kwa hiyo zingatia sana katika kuongeza ujuzi na skills zako, vyeti viwe ushahidi tu.

4. CONNECTION
Usijifungie tu chumbani kwako, connect na ongea na watu mbalimbali kwenye industry yako hasa walio katika nafasi za juu kimaamuzi na wale waliokuzidi uzoefu. Hkikisha wanajua ujuzi na skills zako na what you can bring on the table. Hii ianzie kote kuanzia kwenye mtandao, ndio maana kwenye point namba 2 nikaongelea presence yako kwenye mitandao kama LinkedIn, ukiwa kule unaweza ku connect na watu walio katika industry yako na wakiangalia posts zako na profile yako wanajua kuwa huyu ana skills hizi na zile. Pia, vile vile offline hudhuria zile events zinazohusiana na sekta yako na hakikisha unaongea na wale watu waliokuzidi na kubadilishana nao mawazo.. Ni rahisi mtu kukupa referral namna hiyo, kama ambavyo ilinitokea mimi alienipa referral alifanya hivyo kutokana na kuona posts zangu na profile yangu LinkedIn.

5. Platform unazoweza kupata remote jobs: Hapa chini nitapost link za platforms ambazo unaweza pata hizi kazi za remote zile ambazo nazifahamu. Wadau wengine wanaweza kuongezea links zaidi.
Jobgether is the Largest Remote Job Platform worldwide with more than 160k remote jobs available across the world.

Karibuni kwa yoyote mwenye swali au anaetaka kujua zaidi kuhusu chochote, nipo hapa, maswali yote yaulizwe hapa na nitajibu kila kitu hapa hapa sebuleni!!

DA HUSTLA karena
Stv Mkn
Asante sana mkuu kwa hii post yako, na asante pia kuni tag, nimeanza kupata jibu la post niliyo i post siku kadhaa nyuma, hakika wewe ni hazina na JF iishi milele.

Naona nyingi zinataka uwe resident wa huko US au sijaelewa hii sentence "Remote USA"?
 
Uzi mzuri sana huu
 
Yes, kuna ambazo zimeandikwa hivyo, maana yake zinakutaka uwe kule USA. Target zile zilizoandikwa "Remote Anywhere", au "Remote Africa"
DA HUSTLA
 
Mbona sijaona anataja mshahara wake.!

Hiyo $7500 vp..!?
Kuna uzi alianzisha mkuu. Anasema anakaa nyumbani bongo analipwa $7500 kwa mwezi.

Usikate tamaa. Unajua na mimi pia nimesomea kutibu watu (udaktari) kama wewe? Ila baada ya kuona kuvaa makoti wodini hakuleti pesa nyingi, ikabidi niwe mjanja kidogo nikachepukia kwenye issues za data, na ndizo zinazonipa hizi $$ kwa sasa mkuu.
Baba Swalehe
Data gani umesomea hadi ulipwe $7500 kwa mwezi bila ya uthibitisho au ushahidi wowote? Tuwekee mfano wa kazi ya "data" unayodai ambayo mtu analipwa $7500 kwa mwezi kwa kufanya kazi remotely, ambapo Mwajiriwa yupo Africa na Mwajiri yupo USA au hata Mwajiriwa na Mwajiri wote wapo USA penyewe, na Mwajiriwa anatakiwa kwenda ofisini kila siku huko USA. Weka angalau mfano wa hiyo job listing.
 
Uzi Mzuri sana.
Binafsi niliwahi kufanya miaka ya nyuma kupitia 'upwork' nilipata kwenye startup fulani ipo USA.
Naomba utoe ujizi wako kwenye hizi changamoto kwa hizi 'freelance work'
1. Changamoto ya malipo iliyopo kwa nchi yetu tz na PayPal na mifumo mingine ya malipo eg. Direct transfer kwenye upande wa makato[transfer fees]
2. Kazi nyingi huwa ni za muda mfupi [ nini huwa unafanya katika hili?]
3. Kwa watanzania ninaona shida yetu kubwa kwenye hili sio kuwa competent kwenye ujizi usika bali ni kwenye matumizi ya supporting tools e.g ms office tools sanasana kwenye excel na PowerPoint na email kwa wachache sana[ tafdhali toa maoni katika hili]
4. Lugha [ hapa naomba utoe ushauri mwingi sana maana kwa mtazamo wangu ndio kiini cha hizi kazi]
 
Kati ya watu wote milioni 300 wanaoishi USA, Mwajiri akulipe wewe $7500 kwa mwezi kwa kazi ya "Data" ukiwa Bongo Africa ilhali kutwa upo humu Jamiiforums? Hizo job sites ulizoweka hazijulikani. Nadhani unataka kuwapiga watu kupitia gia ya hizo job sites feki.
 
Back
Top Bottom