Jinsi ya Kupata watoto Mapacha kwa njia ya kawaida

Zinduna, kuna ushahidi wowote juu ya hizi njia ulizotoa?

kiasili tunajua kwamba watoto mapacha wanaendana na history ya mzazi, kama kwenu huwa mna nature ya kuwapata hao, basi utakakooa aua kuolewa, kuna uwezekano pia wa kupata watoto mapacha...
 
Last edited by a moderator:
Aina ya mapacha wanaotokea mara nyingi ni wale wanaotokana na mayai mawili tofauti (Fraternal twins). Hawa wanatokea wakati mayai mawili yanapotoka na kurutubishwa na mbegu (sperms) mbili tofauti. Kwa upande wa pili, mapacha wanaofanana (identical twins) wanatokana na kugawanyika kwa yai moja lililorutubishwa na mbegu moja wakati wa hedhi. Ni nadra sana kupata mapacha wa namna hii kwa njia ya asili.

Unaweza kuongeza uwezekano wa kupata mapacha kwa njia ya kawaida (asili) lakini nyingi ziko nje ya uwezo wa mwanamke. Kuwa na historia ya kuzaliwa mapacha katika ukoo wako, inaweza kuongeza matumaini ya kupata mapacha, hasa kwa mapacha wasiofanana. Hii inatokana nasababu za ki-jenetiki kutoka kwa mmoja wa ndugu wa wazazi. Hii Gene ya mapacha (twin-gene) inaweza kupasishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Hii hali, haihusu sana mapacha wanaofanana.

Hali nyingine inayoweza kupelekea kupata mapacha ni asili pamoja na umri. Wanawake wa asili ya kiafrika wana uwezekano mkubwa wa kuzaa mapacha kuliko wazungu au wahindi. Aidha wanawake wenye umri mkubwa wana uwezekano mkubwa wa kuzaa mapacha kuliko vijana. Mambo mengine ya kufanya ili kuwa na uwezekano mkubwa wa kuzaa mapacha ni haya: - Kunywa kidonge cha folic acid. Kuna uwezekano mkubwa wa kupata mapacha ukitumia kidonge cha aina hiyo wakati wa kuelekea hedhi. - Ongeza uzito.

Baadhi ya tafiti, kwa mfano ile iliyotolewa mwezi Machi mwaka
2005 (Obstetrics & Gynecology study) inaonyesha kwamba, mtu mwenye uzito mkubwa ana uwezekano mkubwa wa kuzaa mapacha. - Unywaji wa maziwa pamoja na kula vyakula vinavyotokana na maziwa (dairy products) kunapelekea uwezekano mkubwa wa kuzaamapacha. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Dr. Gary Steinman, daktari wa Long Island Jewish Medical Center, wanawake wanaokula vyakula hivyo wana uwezekano wa kupata mapacha mara tano zaidi ya wale wasiotumia. - Kuendelea kunyonyesha. Kama unanyonyesha mtoto na unataka kuzaa mapacha, endedelea kufanya hivyo unapokuwa umetunga mimba. Utafiti mmoja unaonesha kwamba, mwanamke anayenyonyesha wakati ameshika mimba, chances za kupata mapacha ni mara tisa zaidi ya yule asiyenyonyesha.

Kila la kheri BINTI77
 
Hii ya Genetics kama ina ukweli hivi

Kwetu katika kila generation kuna twins na in every case in a boy and a girl. Babu yangu alikuwa na wadogo zake mapacha. Naye akaja akazaa mapacha(one of them my father). Akawa anawajukuu mapacha (again a boy and a girl). Bado generation yetu wajukuu....
 
Mimi ni fratenal twin,na mama yangu alipata mapacha mara mbili,i min mdogo wangu nae ana pacha wake...i really hope nami nitapata pacha.
 
yap..habari za eat yams zote stori tuu, pacha huzaa pacha
 
yap..habari za eat yams zote stori tuu, pacha huzaa pacha
Mkiwa katika familia mupo pacha basi watoto zenu watakuwa pia mapacha mimi kwenye familia yangu tupo mapacha mara mbili dada zangu wakubwa wawili mmoja ameshafariki na mimi a ndugu wangu wa kike tulikuwa tupo mapacha na dada zangu wengine wamezaa mapacha akitaka mtu mapacha anitafute mimi nitampa. Kwa sababu mimi mwenyewe mapacha.
 

Nimeipenda sana hii njia ya Kula "Yams' YAANI VIAZI VIKUU AU VILE AMBAVY VIAZI VYAKE VINAOTA KATIKA MAJANI BADALA YA KTK MIZIZI NI VIZURI SANA KUONGEZA UWEZEKANO WA KUPATA MTOTO HATA KWA WALE AMBAO WANA SHIDA YA KUPATA WATOTO VITUMIE NA NAAMINI UTAPATA MATOKEO MAZURI.
PIA USISAHAU KUWA MUNGU NDIE ANAYETOA ZAWADI YA WATOTO
 
Hao mapacha jamani raha wakikua ila wakiwa wadogo kama wasumbufu afu mwenzako akiwa sio mlezi utahangaika nao unaweza sema sizai tena ila wakikua rahaaa
Kwa utamaduni wetun huuuu!! Wanaume tuachieni wenye wee tu baadhi yetu tupo OVYOOO ! twatoka nje nakujisifu ati nimpiga kazi nimeleta pacha!! Lakini hatutoi msaada wala uji hatuwezi saidia. sembuse malezi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…