Hii kitu ni ndefu kidogo kuiandika hapa lakini nitaiweka kidogo kidogo katika hii space...
All in all hakuna kanuni dhahiri ya kuzingatia ili kupata mapacha...
Kuna aina mbili za upatikanaji wa mapacha:
1. Mapacha ambao ni matokeo ya yai lililokwisha kurutubishwa na mbegu ya uzazi ya mwanaume. Hii hupelekea kuzaliwa kwa watoto wenye kufanana.
2. Mapacha ambao ni matokeo ya urutubishwaji wa mayai mawili tofauti yaliyotolewa na ovari za mwanamke. Aina hii ya urubishaji husababisha kuzaliwa kwa watoto wasiofanana.
Hebu ngoja turejelee takwimu na baadhi ya facts kuhusiana na mapacha;
1. Mwanamke anapotunga mimba huwa kuna 3% tu ya kujifungua watoto mapacha.
2. Wanawake wenye asili ya Kiafrika wana nafasi/asilimia kubwa ya kupata mapacha kuliko wanawake wa jamii nyingine, watu kutoka Asia wana asilimia ndogo zaidi.
3. Mwanamke aliyejifungua watoto wengi awali ana nafasi kubwa kupata mapacha endapo ataendelea kubeba mimba.
4. Mapacha wanaofanana huweza kuzaliwa na mwanamke yoyote, hii ni kinyume kwa mapacha wasiofanana ambao ni kitu kinachotokana na urithi katika familia. Mwenye kuhitaji maarifa zaidi anaweza aka-google term moja inaitwa hyperovulation kwa uelewa zaidi.
Mambo ambayo yanaongeza uwezekano wa mwanamke kupata watoto mapacha:
Kuna watafiti ambao wameumiza vichwa na haya ni mambo wasemayo juu ya facts na nini kifanyike au kikifanyika basi uwezekano wa kupata mapacha huongezeka.
1. Ulaji wa suppliments wakati mwanamke akiwa mjamzito haswa zile zenye kuwa na folic acids. Kwa kawaida mama mjamzito hushauriwa kula tembe zenye folic acids kwa ajili ya kuzuia birth defects kwa mtoto lakini imeonekana zinaongeza chances za kupata mapacha kwa wamama ambao bado hawana ujauzito.
Pia ulaji wa tembe zenye magnesium/calcium kwa pamoja husemekana kuongeza chances za kupata mapacha.
ONYO: Hakikisha wapewa ushauri na daktari juu ya matumizi sahihi ya tembe hizi
2. Kwa wale wanawake wanaotumia vidonge vya uzazi wa mpango wana nafasi kubwa pia na huja pindi wanapoacha kwa ghafla matumizi ya vidonge hivyo.
Kuacha kutumia vidonge hivi humaanisha unauambia mwili urekebishe mfumo wa vichocheo kurudi kawaida na kabla ya kurudi kawaida husemekana mara kadhaa za mwanzo kwa baadhi ya wanawake, ovari zao hudondosha/hupevusha mayai mawili. (Mayai mawili maana yake mimba ya mapacha kama kukiwa na sperms).
3. Ulaji wa vyakula vyenye asili itokanayo na maziwa ya ng'ombe (diary products).
Inasemekana kuwa mwanamke mwenye kutumia products hizi nafasi yake ya kupata mapacha huongezeka mara 5 zaidi ya yule asiye mtumiaji kabisa wa dairy products.
Sababu ya kuamini hivi ni kutokana na uwepo wa IGF itengenezwayo na ini la ng'ombe ambayo huaminika ni kichocheo cha kutengeneza mapacha.
Inaaminika pia ukinywa maziwa yenye kuwekwa vichocheo vya rBGH huongeza uwezekano wa ovari za mwanamke kupevusha yai zaidi ya moja.
4. Jaribu kupata ujauzito wakati umri ukiwa umeyoyoma. Wanawake ambao wana umri kuanzia miaka 45 inaaminika wana nafasi kubwa ya kupata mapacha kwa 17%.
Katika umri mkubwa wanawake hutengeneza FSH nyingi. Kichocheo hichi ndio huusika kuziamuru ovaries kutengeneza mayai. Wingi wa vichocheo hivi na hatimaye mayai husababisha uwezekano wa upevushaji wa zaidi ya yai moja.
5. Imekuwa ikiaminika kuwa mwanamke alaye sana magimbi na mihogo ana nafasi kubwa ya kuzaa mapacha.
Hili ingawaje halijachunguzwa kisayansi isipokuwa ni kutokana na tendency ya wanawake wa jamii fulani huko Nigeria kuzaa mapacha sana kuliko sehemu yoyote juu ya uso wa nchi (Mara 4 zaidi ya wanawake wengine duniani).