Fixed Point
JF-Expert Member
- Sep 30, 2009
- 11,304
- 12,746
ha haaaa, mi najipikilisha mwenyewe kwa kutumia google, FB group fulani na JF chef. Practice alone.Ha ha ha ha, FP bana.
Utanisahauje? Ila ninatamani kajikundi hata ka watu 3-5 ka kujipikilisha tu kwa ajili ya familia.
Yes rafiki.....
jana nimetumia blue band kukandia chapati, na nikatumia maji ya baridi ya frijini......
yaani chapati zilikuwa laini mno. la maana tu ni katika kukanda, hakikisha unazikanda mda mrefu mpaka donge liwe laini sana, ukishika likakuwa kama limepikwa.
ha haaaa, mi najipikilisha mwenyewe kwa kutumia google, FB group fulani na JF chef. Practice alone.
Juzi nimemwaga mkate wa kumimina...... nilikosea sikuloweka sana...... this time sikuchemsha uji, uliiva vizuri but tulikuwa tunatafuna kama mchele uliookwa............ nikaona isiwe tabu ya kujaza watu matumboooooo......
zoezi litaendelea kesho. Leo usiku naloweka mchelwa wangu overnight.....
hii kazi ilishashindikana kwangu, au kwa vile mikono ya mwanamume migumu?!
ha haaaa, mengi tu rafiki........JF Chef ndio inanisaidia, ila mie hii ni hobby mpya 🙁
Kumbe na nyie kuna mengi yanawasibu? Mie huwa nadhani alone tu.
Dina, trick kwa chapati laini ni kuukanda unga saaanaaaa, yaani lile donge mpaka linakuwa kama ugali wa muhogo, lol!Nafikiri akina sie tunakwama hapo kwenye ukandaji, manake tunaishia kutoa chapati mpaka unatamani kufunga turubai kuita watu wakusaidie kulia...
Ngoja mie nianze na maswali machache:
1. Katika hatua ya ukandaji, unga ukiwa mgumu sana kuna kutegemea chapati laini hapo au tricky ni kuongeza juhudi ya kuukanda?
2. Na je kama maji yameteleza yakawa mengi na hivyo kuufanya unga 'chapa chapa', nitakosea kama nikitumia unga mkavu kuuweka vizuri?
3. Ni sahihi kutumia mafuta kwenye unga uliokandwa wakati wa zoezi la kuulainisha?
Ha ha ha ha, itabidi uoe sasa
Dina, trick kwa chapati laini ni kuukanda unga saaanaaaa, yaani lile donge mpaka linakuwa kama ugali wa muhogo, lol!
Kuhusu kutelezwa maji au unga, kwa upande wangu kama maji yameteleza huwa naongeza unga kidogo kidogo mpaka napata ugumu ninaoutaka, na kwa donge kuwa gumu pia huwa naongeza maji kidogo kidogo sana ili kuepuka kuongeza unga, maji, unga, maji........
Mimi huwa naweka mafuta mara mbili..... mwanzo kabla sijaweka unga maji, nasugua unga na mafuta, then baada ya kuukanda, kabla sijamalizia kabisa naweka mafuta kidogo kuulainisha
ha haaaaa, natamani nijue kupika hizo chapati kama kaukau ili watu wangu wapoteze hamu ya kula chapati, wataniua kwa kupenda chapati...... wao hata kila siku ukiwapa wanafurahi. kuna kipindi nilifanya hiyo njia ya kukanda chapati nyingiiii nikaziweka kwa friji basi kila siku nachoma za kuwatosha nikajua baaba ya siku 3 watanipiga stop...... wapi....... kazi yao ilikuwa kubadilisha cha kulia tu.... leo na maharage, kesho na supu, keshokutwa na mchuzi...... nilijuuutaaaa.
ha haaaa, nalikumbuka sana hilo tangazo..... mimi huwa natumia trick moja kama nakanda chapati nyingi.... anaanza dada kukandaaaaa, then namalizia. maana namwonea huruma kukanda mwanzo mwisho, na mimi siwezi kukanda mwanzo mwisho.... kwa hiyo tunapokezana, lakini mimi nahakikisha ndo namalizia ili niulainishe ipasavyo.Kwa njia ya maandishi nimeelewa (subiri unga uwe machoni....)....Na haya mafuta ndio wakati mwingine unatumia blue band au?
Out of topic: Unakumbuka kwenye tangazo la Azam (kama upo TZ) wakati wana-introduce zile chapati zao za ready made, kuna mama alikuwa anakanda unga huku jasho linamtoka? Kila nikimkumbuka huwa nacheka mwenyewe....
ha haaaa, kama nawaona watakavyogombana nazo hizo kaukau, maana sidhani kama wataziachia. Ila kali ni ile ya Kongosho ya kuteleza kwenye meno, I cant imagineHahahahaha lol!!!! unataka kutengengeneza kaukau siyo badala ya chapati lol!? Omba recipe hapa kwa watengeneza kau kau kisha unatengeneza kau kau, ukiulizwa hizi chapati za leo ni aje? jibu lako, "sijui huu unga wa safari hii ukoje." 🙂🙂
Za kusukuma zina utamu wake, tofauti na za kumimina........Hapo kwenye kusukuma sasa...ndo maana mimi huwa napikaga tu za kumimina!
ha haaaa, kama nawaona watakavyogombana nazo hizo kaukau, maana sidhani kama wataziachia. Ila kali ni ile ya Kongosho ya kuteleza kwenye meno, I cant imagine
ha haaaa, nalikumbuka sana hilo tangazo..... mimi huwa natumia trick moja kama nakanda chapati nyingi.... anaanza dada kukandaaaaa, then namalizia. maana namwonea huruma kukanda mwanzo mwisho, na mimi siwezi kukanda mwanzo mwisho.... kwa hiyo tunapokezana, lakini mimi nahakikisha ndo namalizia ili niulainishe ipasavyo.
Mimi huwa natumia blueband na haijawahi kuniangusha. Ila naiyeyusha kwanza kwenye microwave ndo naitumia ikiwa ya joto. na maji natumia ya baridi sana.
Kila la heri, utajua tu.
Mi nimehamia kwenye mkate wa kumimina, bado sijaupatia. nipo kwenye process ya kumwaga nyunga zangu, lol!
nitakushtua nikigraduate.........Ukimaliza hapo kwenye mkate usisahau kunistua...wanasema practice makes perfect. Ila udongo ungeongea kwa kupokea nyunga....Kuna siku watu ndani wanasikia harufu ya chapati ili hali chapati hazionekani....nilikuwa nachekea tumboni tu..
Kuna mahali tulikutana kwenye kashughuli kalikohusisha kubeba vyakula vya kiasili...alikuja mwenzetu na chapati hizo...daah...tulibaki kumkodolea macho na kumtaka atupatie ujuzi....yeye mwenyewe alikuwa anaongelea kirahiisiii utafikiri kunywa maji na kikombe....Halafu sasa michapati yenyewe miiingi ajabu...tukabaki kumtamania tu na kusema yaani pamoja na uwingi wa unga lakini chapati quality....