Jinsi ya kupika chapati laini na zenye ladha nzuri

Jinsi ya kupika chapati laini na zenye ladha nzuri

daFakhrina na wengine ...Naomba kuelekezwa kupika pizza..nazipenda sana ila sijui kuziandaa
 
siagi inayoongelewa ni blueband au ile inayotolewa kwenye maziwa nachanganikiwa hapo msaada tagafhali
 
Asante Fakhrina..niulize swali hivi chapati ipi ni tamu na laini zaidi ..ya kukanda na maji baridi au ya kukanda maji moto..nasubiri maelekezo..nakuaminia

Chapati kuwa tamu haijalishi maji ya moto au ya baridi ispokua tu ulaini katika ukandaji...

Chapati tamu ni ile iliyowiva vizuri ndani na laini pia isiwe na mafuta mengi.....
 
Kwa wale ambayo mnatumia whole grains hii inawahusu...

Mahitaji

Unga wa ngano weupe nusu kilo

Unga wa atta nusu kilo...

Chumvi kiasi

Maji ya uvuguvugu....

Samli vijiko 6 vya kulia vijaze...

Extra virgin olive oil vijiko vitatu (waweza tumia mafuta yoyote)...

Namna ya kutaarisha...

Changanya unga na samli na mafuta pamoja na chumvi...

Weka maji ya uvuguvugu na ukande kama chapati za kawaida...

Ukimaliza kukanda weka unga wako katika mfuko mweupe na safi (wraps)....wacha kwa nusu saa

Zungusha chapati zako na uziache kdg...

Sukuma na kaanga kama chapati za kawaida....

Tayar kwa kuliwa...
 
Kwa wale ambao mbinu ya kuandia maji ya baridi haiku work jaribuni hii ya maji ya uvuguvugu alafu kuweka katika mfuko wa plastic
 
Attachments

  • 1416010230046.jpg
    1416010230046.jpg
    43.1 KB · Views: 544
  • 1416010248955.jpg
    1416010248955.jpg
    55.1 KB · Views: 545
Kwa wale ambao hawana muda wa kutosha kuandaa chapati waweza tengeneza siku ukiwa na mda na ukahifadhi katika friji...

Weka kwanza katika sahani na uweke katika friji kwa nusu saa zigandane...

Chukua mfupo safi na weka chapati zako ...

Kama hivi chini
 
Attachments

  • 1416010808710.jpg
    1416010808710.jpg
    40.6 KB · Views: 470
Kwa wale ambayo mnatumia whole grains hii inawahusu...

Mahitaji

Unga wa ngano weupe nusu kilo

Unga wa atta nusu kilo...

Chumvi kiasi

Maji ya uvuguvugu....

Samli vijiko 6 vya kulia vijaze...

Extra virgin olive oil vijiko vitatu (waweza tumia mafuta yoyote)...

Namna ya kutaarisha...

Changanya unga na samli na mafuta pamoja na chumvi...

Weka maji ya uvuguvugu na ukande kama chapati za kawaida...

Ukimaliza kukanda weka unga wako katika mfuko mweupe na safi (wraps)....wacha kwa nusu saa

Zungusha chapati zako na uziache kdg...

Sukuma na kaanga kama chapati za kawaida....

Tayar kwa kuliwa...
Hongera kwa mapishi yako farkhina
 
Last edited by a moderator:
Unga wa atta ndo wa ajee,,yaan mi kila nikitaka kupika chapati napata nawazo aiseee

Hivi farkhina na maandazi unaweza yakaanga kwa moto wa kawaida ili yaive ndan vizurii????
 
Back
Top Bottom