Kwa wale ambayo mnatumia whole grains hii inawahusu...
Mahitaji
Unga wa ngano weupe nusu kilo
Unga wa atta nusu kilo...
Chumvi kiasi
Maji ya uvuguvugu....
Samli vijiko 6 vya kulia vijaze...
Extra virgin olive oil vijiko vitatu (waweza tumia mafuta yoyote)...
Namna ya kutaarisha...
Changanya unga na samli na mafuta pamoja na chumvi...
Weka maji ya uvuguvugu na ukande kama chapati za kawaida...
Ukimaliza kukanda weka unga wako katika mfuko mweupe na safi (wraps)....wacha kwa nusu saa
Zungusha chapati zako na uziache kdg...
Sukuma na kaanga kama chapati za kawaida....
Tayar kwa kuliwa...