Nilikuwa busy sana Leo pole
Ngoja nikuelekeze mpendwa sasahivi
Tuanze na kuchoma mishkaki
Mahitaji(Mimi Huwa sipendi viungo vingi)
Nyama steki,chumvi,kitunguu swaumu,tangawizi,manjano,limao na mafuta kijiko kimoja Cha chakula
Kata nyama Yako weka kwenye bakuli hakikisha Haina maji
Chukua bakuli nyingine weka kitunguu swaumu ulichosaga na tangawiz weka chumvi limao manjano na mafuta koroga Kisha mimina mchanganyiko wako kwenye nyama Changanya Kisha funika Kwa muda kidogo kuanzia Lisaa na kuendelea Kisha weka nyama kwenye vijiti Anza kuchoma mishkaki Hadi itakapoiva