Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwamba inakuwa pombeUsile kabisa. Unajui hii ikiachwa kwa siku moja tu ikachacha itageuka kuwa GIN.
Ndio naona kwako leoZinapikwa my dear Tena sana tu
Hii ni taarifa mhimu kwangu.mimi nazipenda hizi ndizi.Nilikuwa nachemsha tuu na maji na chumvi basi.haoa nimepata pishi lingine.Asante kwa elimuNatumaini mkopoa
Wapenz wa ndizi ,Ndizi mzuzu zikiiva msitupe
Leo nimewaletea recipe hii ya kupika ndizi mzuzu zilizoiva za Nazi
MAHITAJI
Naz
Ndiz zilizoiva
Iriki iliyosagwa ama nzima
Sukari kama hupendi tumia chumvi
Hatua ya kwanza
Menya ndizi kata vipande vinne
Kama unatumia Nazi ya kawaida chuja tui la kwanza zito (bubu)na tui la pili weka pekeyake
Kama unatumia ya pakti bas andaa Nazi Yako weka maji kidogo kwakuwa huwa nzito sana
Hatua ya pili
Bandika sufuria ama pan weka ndiz zako Kisha weka tui la Nazi
La pili lile jepes kama unatumia Nazi ya pakti weka maji(maji yasiwe mengi)Kisha weka iriki funika acha ichemke had maji yakikauka
Hatua ya Tatu
Maji yakikauka weka sukari kma hupendi weka chumvi Kisha mimina tui la lile zito tikisa sufuria taratibu had vichanganyike usikoroge koroge na mwiko vitapondeka acha vichemke Kwa dakika 5 zitakuwa tayari View attachment 3099784View attachment 3099785View attachment 3099786
Duuh,Maji yakikauka weka sukari
Haswa. Ndizi mbivu zilizopikwa zikaachwa siku mbili plus ulezi ni pombe huitwa MBEGE.Kwamba inakuwa pombe
Huyo jamaa apo juu kasema ikilala inakuwa kama gin ndo nikamuuliza kwani inakuwa pombe ikilala??Ukila ndiz mvivu zinakuwa pombe au kwakuwa zimepikwa😀