Jinsi ya kupika tambi

Jinsi ya kupika tambi

Yani nlikua nawaza nipike nini leo na mboga ndani sina jioni nayo yaingia!! nkawaza maharage ila nimechelewa!! Lol si ndo nimeona hili pishi la tambi!! !! Nimefurah hadi basii!! Nazipika hizi hiz na mrejesho ntakupa kesho.
 
Uweke na share yangu
 
Vipi ilikwendaje?
 
Tambi au pasta ni moja ya vyakula ninavyovipenda sana.Ni rahisi kuandaa na kuna namna nyingi sana ya kuziandaa na kuzipika.
Kutokana na uandaaji au upishi tambi zinaweza kutumika kama appetizer,kama chakula kikuu na kama dessert.

Mahitaji
Tambi paketi moja(Santa Lucia)
Sukari ¼ kikombe au kwa ladha upendayo
Iliki Kijiko 1 cha chakula au kwa ladha upendayo(mbegu za iliki zilizosagwa)
Maji kikombe 1 1/2 au zaidi
Maziwa fresh kikombe 1 au tui zito la nazi
Mafuta yatokanayo na mimea 1/2 kikombe au zaidi

Njia
1.Chemsha maji,weka kando.Chemsha maziwa,weka kando.
2.Katika sufuri au kikaango weka mafuta,ongeza tambi,kaanga tambi kwa moto mdogo sana adi zibadilike rangi na kua Brauni.

3.Ongeza maji ya moto (kua makini mvuke usikuunguze),ongeza sukari na iliki,changanya,funika vichemke.Ongeza moto uwe wa wastani.

4.Maji yakielekea kwisha ongeza maziwa ya moto,changanya.Acha vichemke uku ukigeuza mara kwa mara ili tambi na maziwa visinate kwenye sufuria.
5.Maziwa yakielekea kukauka,punguza moto,acha adi maziwa yakauke kabisa kisha fanya kama unakaanga tambi ili kuhakikisha zinakauka .Zikiwa tayari tambi zitakua na matone meupe madogomadogo kama zimemwagiwa nazi ya unga.Tayari kwa kula.

JUA:Mafuta ni kiungo muhim kweneye pishi hili,ukiweka mafuta kidogo sana,hutapata matokeo mazuri.Tambihazitakaangika vizuri mwishoni.
Chakula hiki hupendwa sana na watoto,ni vyema kukiloanisha na mchuzi au sosi ili mtoto ale kwa urahisi.
Unaweza remba chakula hiki kwa kutengeneza uso wa mdoli,mauwa na michoro mengine kwa kutumia mboga za majani au matunda ili kumvutia mtoto kula.

MUONEKANO MZURI WA CHAKULA HULETA HAMU YA KULA.

Asante kwa pishi zuri kweli linavutia ngoja na mm nimwandalie toto angu
 
Sie twaita tambi za kukaanga...ungeziweka na zabibu kavu hapo umemaliza kila kitu!!
 
Nimeutengeneza huu mlo, kwa kweli ni nomaa hapo sijaweka njegere. Uko juu mkufunzii
 
nyongeza:- baada ya upika ivo unaweza kula pamoja na kishushio cha maziwa fresh. NB: ni mzoefu wa pishi hili nami pia.
 
Back
Top Bottom