Jinsi ya kupika UGALI Fasta Fasta (Full Steps)

Jinsi ya kupika UGALI Fasta Fasta (Full Steps)

mambo zenu wakuu leo ntafundisha jinsi ya kupika ugali

Fuata Steps Hizi

MAHITAJI

Maji,unga wa sembe/Dona + Sufuria,Ubanio,Mwiko na jiko la aina yoyote mkaa au umeme au gesi..

Step 1

Sikia Injika sufulia yako jikoni ikiwa na maji yenye unga kidogo. hakikisha maji utayoweka yatakutosha.Pia hakikisha moto unakua sio mwingi ni wastan.

Step 2
Haya anza kukorogea hadi pale maji yatapochemka na kua uji uji unaotokota.

Step 3

Umeshafanikiwa step 2? ,Haya weka unga kiasi kwenye sufuria huku ukianza kuusonga taratiiibu na ubanio. Staili ya kuusonga ni kama unauminya huku unauzungusha kwa mwiko.

Step 4

Utaona mabadiliko ule uji utakua mgumu kila unapoendelea kuusonga.Ukishaona mabadiliko Hayo jua ndo ivo tena ugali umeshaiva.

Step 5 (Mwisho)

Andaa Sahani au hotpot kisha uipue ugali wako.

HONGERA! Nguna ipo tayari kuliwa na mboga yoyote ile uliyoiandaa,inaweza ikawa samaki wa kukaanga or whatever.

Asanteni

View attachment 229008

haki ya nani umenifurahisha sana, yani we umepika kiuhalisia sio wale wanao google vyakula ambavyo hawajawahi

hata kusikia halufu yake wanatuletea hapa, mi hiyo sahanim kwanza nimechoka yani unakula ugali + kutu, halafu kwa

mbali naona kabisa ugali mbichi kabisa huo. ila hongera you made ma day.
 
Soon nitakuja kukutembelea michicha yako siitaki kabisaa.Kitu cha kwanza andaa visheti vyakuwa natafuna mda wote😀

Hahhahaha karibu...vya kiomani au vya kipemba??....au vikokoto vile hadi ukimaliza kutafuna meno yanaomba pooo..lols
 
Mbona hauna shape,na una scarface,huo sio usongaji wa ugali,ugali ukisongwa ili ujue umeiva hutoa presha na kutoa harufu ya kuungulia halafu unakuwa hauna makovu kama huu uliotuletea hapa,unatakiwa uwe smooth bila mipasuko,yafaa upewe talaka kwa kutuletea ugali wa kisukuma humu JF

mkuu mwanaume ntapewaje talaka si uboya huo?

LIKE Niku ADD
 
Last edited by a moderator:
haki ya nani umenifurahisha sana, yani we umepika kiuhalisia sio wale wanao google vyakula ambavyo hawajawahi

hata kusikia halufu yake wanatuletea hapa, mi hiyo sahanim kwanza nimechoka yani unakula ugali + kutu, halafu kwa

mbali naona kabisa ugali mbichi kabisa huo. ila hongera you made ma day.

karibu mkuu

LIKE Niku ADD
 
Last edited by a moderator:
Mie niliambiwa unakata size ya tonge lako na kuuweka mkononi huku umekunja ngumi kwa nguvu. Ukiweza kuhesabu 1 mpaka 10 bila kuungua na hivyo kuifungua ngumi yako basi ni mbichi na kama umeiva hufikishi 10. Zoezi lifanywe mara tu baada ya kuusonga.

Vile vile ugali ulioiva haushiki mikononi unapofinyanga tonge, ukiona mikono inachafuka ukifinyanga jua mbichi.
 
yani mimi naona kupika ugali ni kazi kuliko ubwabwa asee maana unatumia kama uzoefu flani ivi,hzi tutorial zinatufaa
 
Hahahaha ule ugari wa juzi nlifanya ujanja huo mana me ugari upishi wake nababaisha tu sinaga ujuzi
haku akitu rahisi kama ugali,mi wali ndio nabahatisha ,njoo nikufundishe
 
haku akitu rahisi kama ugali,mi wali ndio nabahatisha ,njoo nikufundishe

Hahahaha BAK alishauri nifanye mazoezi nshaweza thanks iyo nafasi ya mafunzo mpatie mwengine lol
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
Nyote nyie mnauzungumzia ugali wa sembe peke yake sijui nasisi waswahili wa kula ugali wa muhogo tutanufaika vipi na huu ufundi wa kupika au unaweza kupika namna jinsi unavyopika sembe?Nisaidieni mimi mahali nilipo unga wa muhogo iunapatikana na tayari ninao lakini nimebakia kuutizama tuu kuupika siwezi ,mimi nimezowea ugali wa bada ule mweusi kwa dagaa wa mawese au kisamvu na samaki naomba nielekezwe namna nitakavyoweza kuupika kirahisi,nitashukuru sana. Msherwampamba.
 
Hahahaha BAK alishauri nifanye mazoezi nshaweza thanks iyo nafasi ya mafunzo mpatie mwengine lol

Jaan karibu nimejifunza leo....lol... nakutania km kawa ugali nipikiwe
Nimeula ki kussum style leo...
 

Attachments

  • 1425567821917.jpg
    1425567821917.jpg
    72.2 KB · Views: 165
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom