Jinsi ya kupika wali wa mbogamboga(wali wa maua) wa Nazi

Jinsi ya kupika wali wa mbogamboga(wali wa maua) wa Nazi

Ni siku nyingine natumaini mnaendelea vyema na mapumziko

Nimeona niweze kushare na nyie jinsi ya kupika wali huu mtamu na unaonukia vizuri
Mahitaji
Hoho,karoti,iriki iliyosagwa au hata nzima,binzari nyembamba,kitunguu na njegere,chumvi,tui la Nazi mchele,chumvi na mafuta ya kula

Hatua ya kwanza
Kata karoti pamoja na hoho vipande vidogovidogo kadri utakavopenda pamoja na kitunguu
Weka tayari tui la Nazi hata ya dukani inafaa
Wingi wa viungo inategemea na mchele wako View attachment 3084266

Hatua ya pili
Bandika sufuria jikoni weka mafuta kidogo sana sababu tunatumia Nazi
Yakipata moto weka kitunguu kaanga kikilainika weka viungo vyako karoti,hoho,binzari nyembamba,iriki pamoja na njegere kaanga Kwa dakika Kama 2View attachment 3084268

Hatua ya Tatu
Weka chumvi Weka Nazi koroga weka ikichemka weka mchele uliooshwa tayari vizuri koroga funikaichemke Hadi ikauke Kisha punguza moto acha wali uive View attachment 3084270
Kisha geuza achatena kidogo wali wako utakuwa tayari
Huu wali ni mtamu na unaharufu nzuri na ladha ya kipekee
Unaweza kula na mboga upendayoView attachment 3084272
Kwa wanaopenda viungo Zaid unaweza ongeza kitunguu saumu pia unaweza karotbna hoho nying wewe upendavyo Mimi sikutaka vingi kulingana na kias Cha mchele wangu
Nawatakia weekend njema 😍😍
Asante Auntie
 
Back
Top Bottom