Jinsi ya Kusajili kampuni katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Nashukuru mkuu!

Ila nasikia kuna income tax, witholding tax na mengine mengi mpaka nimeshindwa kuelewa!

So ina maana makato ni hiyo 30% kwenye faida ghafi kwa mwaka mzima basi au kuna nyingine tofauti na hiyo 30%?

Thanks in adwance mkuu
 
MAKALA: Mambo muhimu ya kuzingatia kuhusu kodi kwa mtu anayeanza biashara

Pitia mada hii utapata faida kubwa sana kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu ktk masuala ya kodi japo tuliiweka kitambo kdg
Kiwanda kama kiwanda kina lipa kodi zipi na zipi nimepitia huo uzi wa elimu juu ya kodi sema nimeona una vitu vingi ngoja niulize jambo la kodi hapa


Kiwanda kidogo kina aina ngapi za kodi, na pia kwa kuwa shareholder mwenzangu ambae yupo nje ha nchi yeye atakua ana share kubwa kidogo je huu wekezaji atatambulika yeye ndiyo mwenye kiwanda na je kodi kwa hapo watachaji vipi TRA

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Sawa Mkuu
Kwa kampuni inakuwa na kodi zifuatazo:
1. Kodi ya mapato 30%
hii nikodi ambayo utailipa kwa namna mbili, ikiwa mwanzo utaanza kulipa kwa kujikadiria ie Provision Tax na baada ya kukamilika mwaka utaandaa mahesabu ya mizania kisha kuangalia ulichilipa awali ni sahihi au laah kwa mujibu wa faida/hasara uliyopata kutokana na mapato

2. Kodi ya zuio WHT
Zimegawanyika utalipa 10% kwa mikataba na gawio na pia utalipa 5% kwa huduma

3. PAYE na SDL
Hizi ni kodi kampuni yako itawajibika kusimamia ulipwaji sahihi wa PAYE kama mishahara itakuwa zaidi ya 270+k na pia kulipa SDL kama wafanyakazi watakuwa zaidi ya wanne

4. Kodi ya ongezeko la thamani - VAT 18%
Hii kama mauzo yatakuwa mil 100 au kuzidi itabidi usajili na kulipa kutokana na mizani ya mauzo na manunuzi katika biashara yako

5. Ushuru wa stempu 1%
Kampuni italipia katika masuala ya kurasimisha mikataba
 
Okey sawa sawa na je kwa kuwa partner wangu ni wa nje ya nchi na mwenye hisa kubwa, hapo TRA wataichukulia kama kampuni ni ya mwekezaji wa nje ya nchi na watamkadiliaje mapato ya kodi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Okey sawa sawa na je kwa kuwa partner wangu ni wa nje ya nchi na mwenye hisa kubwa, hapo TRA wataichukulia kama kampuni ni ya mwekezaji wa nje ya nchi na watamkadiliaje mapato ya kodi

Sent using Jamii Forums mobile app
Naam
1. Hapana hachukuliwi kama kampuni mali yake bali ni mali yenu wote wanahisa
2. Makadirio huwasilishwa mwisho wa mwaka kwa wakurugenzi wote wewe ba hy jamaa wa nje. Mtafanya 'assessment' ya kipato cha kila mkurugenzi kisha atalipa kodi kutokana na mapato ambayo huenda yanapatikana kutokana na kiwanda na shughuli nyinginezo binafsi za nje ya kiwanda
 
Umenisaidia sana kweli umeiva mzee baba, una knowledge ya kutosha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habar za mchana.

Naomba kuuliza je mtu anaefanya biashara ya kununua madini kwa wachimbaji wadogo ambao hawana risit au kufanya biashara ya kuchimba madini kisha ukauza kwa madalali au soko kuu je mtu kama huyu analipaje kodi ukiangalia anapochimba au kununua hapati risit?

Shukran
 
Ahsanteee
Karibu sana
Habar za mchana.

Naomba kuuliza je mtu anaefanya biashara ya kununua madini kwa wachimbaji wadogo ambao hawana risit au kufanya biashara ya kuchimba madini kisha ukauza kwa madalali au soko kuu je mtu kama huyu analipaje kodi ukiangalia anapochimba au kununua hapati risit?

Shukran
 
Salama Mkuu

Ni hivi kabla ya kuanza biashara yyt ile unatakiwa ukasajili Namba Maalum ya Mlipa Kodi ie TIN kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania ie TRA

Hii namba ndiyo itakuwezesha kulipa kodi. Baada ya kusajili kama ni mfanyabiashara na mauzo yk kwa mwaka yanazidi mil 4 utakadiriwa kiasi cha kodi cha kulipa kwa mwaka mzima. Hii haijalishi utakuwa wapata risit au laah. Japo sheria ya kodi imeweka wazi juu ya kutoa na kupata risit pindi unapofanya biashara.

Kupata risit ya mashine ie EFD Receipt inategemea wanunua kwa mfanyabiashara mwenye mapato kiasi gn kwa mwaka. Sheria imeweka wazi kama mauzo ni/zaidi ya mil 14 mfanyabiaahara hy analazimika kutoa risit ya mashine. Na kama ni chini ya hapo basi analazimika kutoa risiti ya mkono

Sasa kwa suala lako kodi ya madini utalipa kama ilivyoainishwa juu ktk makadirio na pia utalipia ushuru wa serikali ktk minada ya madini ya serikali

Pia pitia hapa kwa elimu ya kodi zaidi

MAKALA: Mambo muhimu ya kuzingatia kuhusu kodi kwa mtu anayeanza biashara
 
Nashukuru sana kiongozi.
Nimepata mwangaza.
 
Happy New Week,

#Jipatie

Logo kwa Tsh. 35000,

Flyers na Posters kwa 20000,

Brochures kwa 30000,

Business Card pc 110 kwa 35000

Tunafanya kazi zote za Graphic Designing,

Pia tunafanya Video Editing & Making.

Tucheki #0620275619

#NipeDili #ayendamethusela
 
Swali.
1) Je private LLC zinatakiwa ku file tax returns pia? Kama ndio zinatakiwa hata kama kampuni haikufanya kazi ktk kipindi hicho cha huo mwaka wa fedha? Na taratibu zikoje?

2) Taratibu za kufungua & kuendesha holding company ni zipi?
 
Broo nomba muongozo taratibu za kujisajiri TBS.
 
NAUZA CARWASH MPYA YA KISASA
MAELEZO: UJENZI, MACHINE ZOTE, VYOMBO, SIMTANK, KODI n.k
JUMLA: TZS 8,000,000

LOCATION: KINONDONI BLOCK 41
CALL: 0717 26 33 77
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…