Jinsi ya Kusajili kampuni katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Jinsi ya Kusajili kampuni katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NAUZA BIASHARA YA CAR WASH:

LOCATION: KINONDONI BLOCK 41
NAMBA YA SIMU: 0717 26 33 77

MAELEZO:

MACHINE ZOTE, UJENZI, VYOMBO, SIMTANK, KODI n.k JUMLA: TZS 7,000,000
NIMEBAHATIKA KUPATA KAZI SERIKALINI NA KITUO CHANGU KIKO MKOANI, SO NIMEAMUA KUUZA HII BIASHARA.
 
brela iongeze staff ikiwezekana kama kweli inavutia wawekezajii .INAWEZEKANAJE UNATUMA MAOMBI KUFUNGUA KAMPUNI YANACHUKUA ZAIDI YA 24 WORKING HOURS KUJIBIWA? YAKIJIBIWA UNASAHIHISHWA ,UKITUMA UNAPEWA KOSA LINGINE AMBALO HAWAKUSEMA MWANZO .
 
idadi ya staff hilo siwezi kulisemea isipokuwa kuna vitu vinatakiwa uvifanye kabla ya kuwasilisha ombi lako ikiwa umekamilisha kila kitu huwezi pewa marekebisho hayo kama unakwama sehem yoyote wasiliana nasi kwa msaada zaidi
 
Wakuu hivi tayari wamesharuhusu mtu mmoja kufungua limited company?
 
UTANGULIZI
Kuanzia tarehe 1 Februari 2018 #BRELA ilitangaza kuanza kutumika kwa mfumo wake wa kuwawezesha wamiliki wa makampuni kusajili na kuwasilisha returns BRELA. Pia BRELA ilishatangaza kwamba mnamo tarehe 25 Machi 2018 mfumo wake wa awali wa OBRS uliokuwa unaruhusu kusajili jina la biashara na kufanya clearance ya jina la kampuni kupitia website ungefungwa rasmi ili kuuruhusu mfumo mpya wa ORS wenye uwezo wa kusajili majina ya biashara na makampuni kufanya kazi rasmi.

Hatua 10 za kufuata ili kusajili kampuni imeelezwa hapa chini, tafadhali fuatilia.

Kwa wale wanaohitaji kusajiliwa kampuni au jina la biashara chapu chapu tafadhali wasiliana nami kupitia kwenye ukurasa huu wa mawasiliano

HATUA 10 ZA USAJILI

Hatua #1: Taarifa za msajili
Ili kutumia mfumo huu mpya wa ORS mteja (msajili) anayetaka kusajili jina la kampuni anatakiwa kuwa na taarifa za msajili (msajili anaweza kuwa ni mmoja wa wakurugenzi, Katibu au Wanachama/Wenye hisa wa Kampuni tarajiwa).

Taarifa zenyewe ni:-
  1. Kitambulisho cha Taifa kwa wenyeji na Passport kwa wageni
  2. Simu ya kiganjani
  3. Barua pepe yaani email
Hatua #2: Taarifa za kampuni
Taarifa za kampuni zinazotakiwa ni:-
  1. Aina ya kampuni kama ni ya hisa au isiyo na hisa, ya binafsi au ya uma nk
  2. Jina la kampuni
  3. Tarehe ya kufunga mahesabu - mfano 31 Desemba
  4. Kumbuka: TIN No., Namba ya usajili zitawekwa na mfumo automatically
Hatua #3: Ofisi za kampuni
Taarifa za ilipo au itakapokuwa ofisi za kampuni ambazo ni:-
  1. Aina ya eneo (Aidha limepimwa au la)
  2. Kama halijapimwa tayarisha anuani ya makazi yenye mfumo huu, jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji, kitongoji na ueleze kama eneo lipo karibu na alama zipi ambazo hazihamishiki kama shule ya msingi nk. Usiweke alama ambazo hazina uhakika wa kudumu hapo maana brela watazikataa)
  3. Kama limepimwa tayarisha yafuatayo: Jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji/mtaa, barabara, namaba ya kiwanja, kitalu na nyumba,
  4. Sanduku la posta, simu ya ofisi/kiganjani na barua pepe -email
Hatua #4: Shughuli za Kampuni
Hatua #5: Taarifa za wakurugenzi
Taarifa zinazotakiwa za Wakurugenzi ni:-
  1. Aina ya mkurugenzi kama ni mtu au taasisi
  2. Asili yake kama ni mwenyeji au mgeni
  3. Kitambulisho cha taifa kama ni mwenyeji au passport kama ni mgeni
  4. TIN
  5. Simu ya kiganjani
  6. Barua pepe yaani email
  7. Anuani ya makazi kwa kila mkurugenzi kwa kufuata mfumo wa anuani ya ofisi hapo juu
    1. Taarifa za za makazi zinazotakiwa ni:-
      1. Aina ya eneo (Aidha limepimwa au la)
      2. Kama halijapimwa tayarisha anuanii ya makazi yenye mfumo huu, jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji, kitongoji na ueleze kama eneo lipo karibu na alama zipi ambazo hazihamishiki kama shule ya msingi nk. Usiweke alama ambazo hazina uhakika wa kudumu hapo maana brela watazikataa)
      3. Kama limepimwa tayarisha yafuatayo: Jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji/mtaa, barabara, namaba ya kiwanja, kitalu na nyumba,
  8. Simu ya ofisi/kiganjani na barua pepe -email
Hatua #6: Taarifa za katibu wa kampuni
Taarifa za katibu wa kampuni (company secretary) zinazotakiwa ni:-
  1. Aina ya mtu kama ni mtu asili au taasisi
  2. Asili yake kama ni mwenyeji au mgeni
  3. Kitambulisho cha taifa kama ni mwenyeji au passport kama ni mgeni
  4. Simu
  5. Barua pepe - email
  6. Anuani ya makazi kwa kila mkurugenzi kwa kufuata mfumo wa anuani ya ofisi hapo juu
    1. Taarifa za za makazi zinazotakiwa ni:-
      1. Aina ya eneo (Aidha limepimwa au la)
      2. Kama halijapimwa tayarisha anuani ya makazi yenye mfumo huu, jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji, kitongoji na ueleze kama eneo lipo karibu na alama zipi ambazo hazihamishiki kama shule ya msingi nk. Usiweke alama ambazo hazina uhakika wa kudumu hapo maana brela watazikataa)
      3. Kama limepimwa tayarisha yafuatayo: Jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji/mtaa, barabara, namba ya kiwanja, kitalu na nyumba, sanduku la posta, simu ya ofisi/kiganjani na barua pepe -email
  7. Simu ya ofisi/kiganjani na barua pepe -email na (sanduku la posta kwa ajili ya memart)
Hatua #7: Taarifa za wanachama/wenye hisa
Taarifa za wanachama au wenye hisa zinazotakiwa ni:-
  1. Aina ya mtu kama ni mtu au taasisi
  2. Asili yake kama ni mwenyeji au mgeni
  3. Kitambulisho cha taifa kama ni mwenyeji au passport kama ni mgeni
  4. Simu
  5. Barua pepe - email
  6. Anuani ya makazi kwa kila mkurugenzi kwa kufuata mfumo wa anuani ya ofisi hapo juu
    1. Taarifa za za makazi zinazotakiwa ni:-
      1. Aina ya eneo (Aidha limepimwa au la)
      2. Kama halijapimwa tayarisha anuani ya makazi yenye mfumo huu, jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji, kitongoji na ueleze kama eneo lipo karibu na alama zipi ambazo hazihamishiki kama shule ya msingi nk. Usiweke alama ambazo hazina uhakika wa kudumu hapo maana brela watazikataa)
      3. Kama limepimwa tayarisha yafuatayo: Jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji/mtaa, barabara, namba ya
Hatua #8: Viambatanisho (Attachments in PDF)
Viambatanisho vinavyotakiwa kuambatanisha kwenye maombi (zote katika pdf) ni:-
  1. Memorandum and articles of association iliyosainiwa na wanachama/wenye hisa pamoja na mwanasheria wa uma (Notary Public)
  2. Form 14b iliyosainiwa na mmoja wa wakurugenzi na mwanasheria wa uma (Notary Public)
  3. Ethics and Integrity Forms iliyosainiwa na mmoja wa wakurugenzi
  4. Company consolidated form iliyosainiwa wakurugenzi wote na katibu wa kampuni
Hatua #9: Ada za usajili na kufaili (Different Fees)
Aina za ada ni kama ilivyoonyeshwa hapa chini
  1. Kusajili kampuni
  2. Kuhifadhi nyaraka na
  3. Stamp Duty
Hatua #10: Namna ya kulipa ada (Payment Methods)
Malipo ya ada yanafanyika kwa njia kuu tatu ambazo ni
  1. Kuweka Benki: Kwa njia y kuweka Fedha kwenye Tawi la Benki /Wakala wa Benki
    Nenda kwenye Tawi lolote la Benki / Wakala wa Benki ya CRDB /NMB kwa kutumia Namba ya Kumbukumbu ya Malipo uliyopewa kupitia PO yako
  2. Kwa njia ya Simu ya Mkononi: Tumia mtandao wa simu wa AirTell Money / Tigopesa/ MPesa/ HalloPesa kwa kuweka namba ya Kampuni 888999 na Kumbukumbu ya Malipo uliyopewa kupitia PO yako
  3. Kwa njia ya Kuhamisha Fedha: Unaweza kuhamisha Fedha moja kwa moja kutoka katika Benki yoyote kwenda kwenye Akaunti zetu zilizoko katika Benki ya NMB/ CRDB kwa njia ya TISS /SWIFT kwa kujaza: Namba ya Akaunti na Kumbukumbu ya Malipo uliyopewa kupitia PO yako
Kumbuka: Utaratibu wa malipo aidha kwa simu au benki utapewa ukishafikia hatua husika ya malipo

Soma zaidi kuhusu jinsi ya kufanya malipo BRELA Kupitia Simu Yako

HITIMISHO NA USHAURI
Brela sasa hivi hawataki usajili kwa njia ya zamani, yaani kupeleka makaratasi ngumu na kusubiri mlangoni kwa siku 6. Pia BRELA hawakubali mtu asiye na kitambulisho cha Taifa yaani #NIDA kusajili kampuni au jina la biashara.
Taarifa zilizotolewa hapo juu ni zile za lazima ambazo bila hizo huwezi kumalizia usajili na au usajili unaweza kukawia

Nashauri yafuatayo:
  1. Nashauri kama unataka kusajiliwa kampuni au jina la biashara kwa haraka wasiliana nasi kwa kutumia mawasiliano
  2. Kama huna kitambulisho cha Taifa na umeshaandikisha ili kupata kitambulisho cha Taifa, tembelea ofisi zozote za NIDA karibu na wewe ili wakupe angalau namba yako ya kitambulisho ili uweze kukitumia ukiambatanisha na Kibali cha BRELA ili Kupata Kitambulisho cha NIDA kwa haraka.
  3. Nashauri pia kama bado hujajiandikisha ni vyema ukawahi, hata kupitia kwenye eneo ambalo zoezi linaendelea ili uwahi kwa maana serikali imeanza kuzuia kupata huduma za public kama huna kitambulisho. ambatanisha pia Kibali cha BRELA ili Kupata Kitambulisho cha NIDA kwa haraka.
  4. Mwisho nashauri hizi taarifa zote uwe nazo mkononi kwa sababu huu mfumo wa usajili wa ORS unakupa siku sita (6 days) tu kukamilisha usajili kama baada ya hizo siku bado, taarifa zote zinafutika na itakubidi uanze upya from the scratch.
Kwa wale wanaohitaji kusajiliwa kampuni au jina la biashara chapu chapu tafadhali wasiliana nami kupitia kwenye ukurasa huu wa mawasiliano

Bofya hapa: Hatua 10 Rahisi za Kusajili Jina la Biashara Kupitia Website ya BRELA
Mkuu kwa sasa wamesharuhusu mtu mmoja individual anaweza kufungua limited company? Au bado ni kuanzia watu wawili
 
Mkuu kwa sasa wamesharuhusu mtu mmoja individual anaweza kufungua limited company? Au bado ni kuanzia watu wawili
Hapana limited company ni kuanzia watu wawili na kuendelea vinginevyo itakupasa kusajili business name hadi pale utapompata mtu wa kuweza kushirikiana nae
 
Wana JF naomba mwenye taarifa za taratibu za kusajili kampuni ya madini pale nyumbani Tanzania anisaidie.

Natanguliza shukrani zangu.

BAADHI YA MAJIBU YALIYOTOLEWA NA WADAU:

===

===

===

===
Welcome! Our services include:

  • Web design
  • Logo design
  • Online business or company registration
  • Airline and Bus ticketing (Domestic & International)
  • Passport and Visa Registration
  • Studying abroad programs
  • Online imports and export services
  • And other IT related services
 
Nina swali kuhusu products na jina la biashara au kampuni. Kwa mfano Azania inaitwa Azania food products ila ana product zake nyingi kama Azania sembe, ngano na mafuta.
Je kila product inasajiliwa brela separate au usajili wa kampuni unajitosheleza?
Pia ningependa kufahamu juu ya utofauti wa jina la kampuni na prooducts, kwa mfano SBC company limited wanatengeneza Pepsi, Mirinda, 7up. Je wamezisajili hizi soda peke yake au usajili wa kampuni unajitosheleza?
Kwa kuzingatia mifano hiyo michache nina imani nitajibiwa.
Aksanteni bila shaka nitajibiwa.
 
X
Welcome! Our services include:

  • Web design
  • Logo design
  • Online business or company registration
  • Airline and Bus ticketing (Domestic & International)
  • Passport and Visa Registration
  • Studying abroad programs
  • Online imports and export services
  • And other IT related services
 
brela iongeze staff ikiwezekana kama kweli inavutia wawekezajii .INAWEZEKANAJE UNATUMA MAOMBI KUFUNGUA KAMPUNI YANACHUKUA ZAIDI YA 24 WORKING HOURS KUJIBIWA? YAKIJIBIWA UNASAHIHISHWA ,UKITUMA UNAPEWA KOSA LINGINE AMBALO HAWAKUSEMA MWANZO .
Issue hapa sio kuongeza staff ni weledi wa staff. Pia umeona huo mfumo wa ORS unavyopandana? Kuna mtu nilisoma mada yake kuhusu ITs wa Tanzania na namna ilivyowachukua vijana waliopewa 15m kudevelop app ya kutrack magari na mwisho wa siku walishindwa na nilikubalina nae sisi watz hamna kitu yaani ni sufuri bin sufuri ila wapo wachache wenye ueledi. Naomba behaviorist asije hapa na ile mada yake yenye kula kwa urefu wa kamba ujumbe ambao anaambatanisha na video.[emoji12]

Its very sad and very shame ila kama Taifa tunatakiwa kupambana sana kujikwamua. Mimi ninaona MFUMO WA ELIMU YETU NDIO CHANZO CHA MATATIZO YOTE TULIYONAYO.
 
Naomba kuuliza swali

hivi mfano umefanya kazi na kampuni iliyosajiriwa brela ikakutapeli na kuhama location kutoka point A to B unafanyaje ili kuwapata?
 
Naomba kuuliza swali

hivi mfano umefanya kazi na kampuni iliyosajiriwa brela ikakutapeli na kuhama location kutoka point A to B unafanyaje ili kuwapata?
kimaadili haifai kuweka mbinu au njia hizo tafadhari nitafute inbox nikusaidie ni bure tu usije kuona neno inbox ukahisi pesa no
 
Naomba kuuliza swali

hivi mfano umefanya kazi na kampuni iliyosajiriwa brela ikakutapeli na kuhama location kutoka point A to B unafanyaje ili kuwapata?
Kampuni zote Zina anwani za kudumu, km simu, e-mail, box na hata a/c za bank walizotaka kukulipa kitapel, wanaweza kuhama mtaa kutokana na Kodi ya pango au jengo walilo allocate kuvunjwa nk lkn hawatakificha ipo siku watafanya kazi au kujitangaza utawapata tu. Mimi kuna kampuni nilizifungua Brela sikufanikiwa kufanya kazi nikaziua lakini bado kumbukumbu zipo Brela
Hiyo kampuni hawezi towels mwisho malizia Brela kuwatafuta
 
Asante mkuu
 
Remove for 14b for beneficial owner, that form should be submitted after having obtain incorporation number.

Naomba msaada nmekwama kwenye brela system wamenipa haya marekebisho nifanye ila hio form 14b kila nikiiondoa system inagoma kuendelea
 
Kuna 14 b ambayo si ya beneficial owner ambayo inasainiwa na declarant ambaye ( ni director au company secretary) pia inagongwa muhuri wa wakili ndio inatakiwa hapo. So ukiondoa hiyo uliyoambiwa unaweka hii nyingine ndio kazi ita proceed
 
Back
Top Bottom