Jinsi ya Kusitisha Uchaguzi Usiofuata Sheria na Kuhakikisha Mshindi Halali Anatangazwa

Box la kura lipo kila uchaguzi au huko kwenu mnaweka kwenye magunia..acheni maigizo jipangeni kwa uchaguzi CCM ni dhaifu Lissu ana uwezo mwingi sasa kwanini mnaogopa uchaguzi!
Safi sana... waingie kwenye uchaguzi na wahakikishe mshindi anatangazwa , hapo pa kutangazwa mshindi ndipo penye Tatizo.
 
Mwananchi wa kawaida ndio anaweza kupigania reforms chadema walitakiwa kuongoza katika matatizo ya kijamii sio kisiasa hawataungwa mkono na mwananchi wa kawaida
Mwananchi wa kawaida by definition ni nani? wewe umo au haumo?
 
Mwananchi wa kawaida ndio anaweza kupigania reforms chadema walitakiwa kuongoza katika matatizo ya kijamii sio kisiasa hawataungwa mkono na mwananchi wa kawaida
Hao wanaotokea kwenye mikutano yao kwa hiari sio wananchi wa kawaida. Au wananchi wa kawaida huwa wako wapi?
 
Cdm hawajawahi kuogopa uchaguzi na hawatakaa waogope. Kinachotakiwa ni uchaguzi wa haki. Na ilivyo hakuna uchaguzi wa haki.
Kweli tupu na sijui ni kwa nini watu hawapendi haki na uwazi utamalaki kwemye uchaguzi... vificho vya nini kama sisi sio wapiga ramli?
 
We ndio unajiita msomi? Upupu wote ulioandika ni aibu
 
Safi sana... waingie kwenye uchaguzi na wahakikishe mshindi anatangazwa , hapo pa kutangazwa mshindi ndipo penye Tatizo.
Kura zikiwa za kutosha sidhani kama ni tatizo... nilichoking'amua upinzani hushindwa kwa mambo mengi kuto kujipanga na kuweka watu makini kwa maana ya mawakala mfano ni serikali za mitaa nimekuta chadema walikuwa wanaokoteza watu barabarani na kuwapa fomu ili mradi tu wawe wametimiza wajibu!
 
Zuzu mwenzie hili hapa
 
Hao wanaotokea kwenye mikutano yao kwa hiari sio wananchi wa kawaida. Au wananchi wa kawaida huwa wako wapi?
Watu kushiriki kwenye mikutano haimaanishi wanaunga mkono hoja moja kwa moja bali wanasikiliza hoja
 
We ndio unajiita msomi? Upupu wote ulioandika ni aibu
reference yako kwa mimi kujiita msomi kwa kutoa maoni yangu ni ipi? Au hapa ndipo ulipoishia... heshimu mawazo ya wengine bila mkwaruzo kama kichuguu., mchwa na nguchiro wanaoishi bila mkwaruzano ingawaje ni wahasimu wakubwa.
 
nakubarina na mawazo yako ndio maana nimewapa mbinu mbadala tuone kama watazifuata ili kutimiza agenda yao ya no reforms no elections.
 
Rubbish za junior lawyers
na Rubbish za senior lawyer sijui zikoje? binafsi huwa sipendi watu kukejeli mawazo ya wengine bila kutoa ufafanuzi. Kuna watu humu wanakwaza sama wengine kwa kweli. Yaani wao ni matusi na kejeli, but yote ni maisha
 
Watu kushiriki kwenye mikutano haimaanishi wanaunga mkono hoja moja kwa moja bali wanasikiliza hoja
Serious? Hiyo hoja sio mpya, tayari kila anayeenda kwenye mkutano anajua hoja ni ipi. Kujitokeza ni dalili ya kukubaliana nayo, na huo mkusanyiko ni ishara ya kuunga mkono. Ni lipi jipya linaloongelewa kwenye hiyo operation ambayo haifahamiki hadi mtu aende physical?
 
Tlaatlaah , hivi wewe hupendi haki , uwazi au sheria? Binafsi napenda Haki, Amani na sheria zitamalaki gentleman sijui wewe mwenzangu?
Haki inaambatana na wajibu gentleman,
ndio maana nashauri vijana na waTanzania wote kujitokeza kwa mamilioni yao kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu huru, wa haki na wa wazi utakao fanyika kwa amani sana october mwaka huu, maana hiyo ni miongoni mwa haki ya kikatiba ya kila mTanzania mwenye sifa ya kupiga kura.

kinyume na hapo ni ushirikina na kujidhulumu wenyewe
 
Gentleman, je uchaguzi utakuwa wa uhuru, wazi na wa haki na mshindi halari kutangazwa? ndio swali linalosumbua akili za watu.
 
Gentleman, je uchaguzi utakuwa wa uhuru, wazi na wa haki na mshindi halari kutangazwa? ndio swali linalosumbua akili za watu.
gentleman,
ikiwa wametekwa na kubebwa na dhana na nadharia potofu za ambao mara zote hukataliwa na wananchi kwenye sanduku la kura, watajikuta wnapewa stori tu na walioshiriki uchaguzi huo juu ya namna uchaguzi ujao wa october utakavyokua bora, wa kihistoria na wa mfano duniani,

na itawabidi wasubiri miaka mitano ijayo tena ili sasa na wao waeweze kupata fursa walioikosa kwa kupotoshwa kwenye uchaguzi huu.

ni vizuri kujua kwamba akili za kuambiwa ni muhimu changanya na zako.
daima ambatana na washindi ili nawe ushinde.
october2025 atatangazwa mshindi halali pekee.

Kuambatana na walioshindwa matokeo yake huwa ni mazito sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…