Jinsi ya Kusitisha Uchaguzi Usiofuata Sheria na Kuhakikisha Mshindi Halali Anatangazwa

Jinsi ya Kusitisha Uchaguzi Usiofuata Sheria na Kuhakikisha Mshindi Halali Anatangazwa

gentleman,
ikiwa wametekwa na kubebwa na dhana na nadharia potofu za ambao mara zote hukataliwa na wananchi kwenye sanduku la kura, watajikuta wnapewa stori tu na walioshiriki uchaguzi huo juu ya namna uchaguzi ujao wa october utakavyokua bora, wa kihistoria na wa mfano duniani,

na itawabidi wasubiri miaka mitano ijayo tena ili sasa na wao waeweze kupata fursa walioikosa kwa kupotoshwa kwenye uchaguzi huu.

ni vizuri kujua kwamba akili za kuambiwa ni muhimu changanya na zako.
daima ambatana na washindi ili nawe ushinde.
october2025 atatangazwa mshindi halali pekee.

Kuambatana na walioshindwa matokeo yake huwa ni mazito sana :pedroP:
Haya Gentleman, najiandaa kuangalia wakipigwa na kitu chenye ncha kali...
 
Serious? Hiyo hoja sio mpya, tayari kila anayeenda kwenye mkutano anajua hoja ni ipi. Kujitokeza ni dalili ya kukubaliana nayo, na huo mkusanyiko ni ishara ya kuunga mkono. Ni lipi jipya linaloongelewa kwenye hiyo operation ambayo haifahamiki hadi mtu aende physical?
Reforms zozote ambazo zinahitaji kupambaniwa kwa jasho na damu zinahitaji wakereketwa kwa nature ya siasa zetu wakereketwa wa mambo za kisiasa ni wachache kulinganisha na masuala mengine ya kijamii

Kwa Tanzania hii hakuna mwananchi wa kawaida atakae kuwa tayari kujeruhiwa na hata kufa kwa maswala ya kisiasa. Yani mtu afe kisa eti mbunge aingie madarakani kwa mwananchi wa kawaida hilo ni suala gumu kwanza hata mifumo ya uchaguzi ikiwa sawa lazima itumike nguvu kubwa kumshawishi mtu huyo akapige kura je kupigania huo mfumo inakuaje?

Hoja yangu hapa ni kuwa, kupitia matatizo ya kijamii kama vile suala la wafanyabiashara wa kariakoo kipindi kile, tozo za miamala wakati ule na matatizo mengine mtambuka yanayoanzishwa na serikali ambayo huwagusa wananchi wa kawaida moja kwa moja ndio yanaweza kuwa chachu rahisi katika kupigania reforms mbalimbali na sio za kisiasa tu kama kipindi hiki cha uchaguzi
 
Jinsi ya Kusitisha Uchaguzi Usiofuata Sheria na Kuhakikisha Mshindi Halali Anatangazwa:
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Ibara ya 21(1), inasema Hapa https://www.nps.go.tz/uploads/documents/sw-1708320157-KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA 1977 (1).pdf :

“Kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, ama moja kwa moja au kwa kupitia kwa wawakilishi walioteuliwa kwa hiari yake kwa njia ya uchaguzi ulio huru na wa haki.”

Hii ina maana kuwa uchaguzi usiofuata misingi ya uhuru na haki ni ukiukaji wa haki ya msingi ya raia. Ibara hii inaweza kutumika kama msingi wa kupinga uchaguzi utakao fanyika in breach of fundamental rights au uliojaa dosari.

Mfano halisi:
kifungu cha 111(1) kinasema:

“Mtu yeyote anaweza kufungua kesi ya kupinga uchaguzi wa Mbunge kwa misingi ya kutokuwepo kwa uhalali katika uchaguzi huo.”

Hii inahakikisha kuwa tume ya uchaguzi na mahakama zina mamlaka ya kushughulikia uchaguzi uliofanyika kinyume na taratibu. Msiniulize ktk uhalisia, ni jukumunla serikali kuhakisha kwamba raia wanapata hakli zao hata kama hawa uwezo wa kifedha kufungua kesi. Kukosa fedha kisiwe ni kichaka kukandamiza haki za watu.

Katika jamii yoyote yenye demokrasia ya kweli, uchaguzi ni msingi muhimu wa kuhakikisha kuwa sauti ya wananchi inasikika. Hata hivyo, kuna nyakati ambapo uchaguzi hauendeshwi kwa mujibu wa Katiba au sheria, na matokeo yanayopatikana hayawakilishi matakwa ya watu. Katika hali kama hiyo, ni jukumu la raia, vyombo vya sheria (wakiwemo polisi- vingenevyo nao pia wafunguliwe kesi- deliction of duties kwa kutowakamata wavunja sheria- kama wasimamizi wa uchaguzi- mchana kweupe ), vyombo vya habari, na taasisi huru kuhakikisha kuwa uchaguzi huo unasitishwa na mshindi halali ndiye anayekabidhiwa madaraka.

Hapa chini ni njia mbalimbali za kuzuia au kusitisha uchaguzi usiofuata taratibu:

1. Kutoa Malalamiko Rasmi Kupitia Tume Huru ya Uchaguzi. Tume lazima itoe majibu kabla ya uchaguzi kwamba itafuata miongozo iliyowekwa na mshindi halali kutangazwa.

Kila nchi humu duniani ina tume ya uchaguzi inayopaswa kusimamia uchaguzi kwa haki na uwazi. Endapo kuna ushahidi kuwa uchaguzi haukufuata sheria—kama vile kununua kura, vitisho kwa wapiga kura, au kuchezea matokeo—raia au vyama vya siasa vinaweza kuwasilisha malalamiko rasmi kwa tume hiyo. Ikiwa tume ni huru (kama inavypitwa) na ya haki, italazimika kusitisha au kurudia uchaguzi huo.

2. Kufungua Kesi Mahakamani kabla na baada ya uchaguzi:

Mfano halisi: Katika kesi ya Christopher Mtikila v. Attorney General (1995), Mahakama ilisisitiza kuwa haki ya kuchagua na kuchaguliwa ni ya msingi na inapaswa kulindwa kwa hali yoyote.

Huwezi kuona haki yako inachezewa au na inaenda kuchezewa na wewe kunyamaza tu. Mahakama ni chombo cha mwisho cha kutoa haki. Ikiwa tume ya uchaguzi haichukui hatua, vyama au wananchi wanaweza kuwasilisha kesi mahakamani- kupinga uchaguzi usifanyike maana ukifanyika ni kukiuka Katiba p- breach of fundamental rights and bills of rights- kwamba mara nyingi mshindi hatangazwi.

Katika historia ya mataifa mengi mfano kwa majirani Kenya, mahakama zimeweza kubatilisha uchaguzi uliojaa udanganyifu na kuamuru urejelewe au mshindi halali kutangazwa. Kesi zinapaswa kufunguliwa sasa katika kila Kijiji na hao wanaotaka kusimamisha uchaguzi hadi kesi ya msingi iamuliwe- referee wa uchaguzi – mteuliwa wa Raisi- hayuko qualified kusimamia uchaguzi. Hii kesi itachukua uda mrefyu sana kusikilizwa na maana yake ni kwamba, uchaguzi lazima utasimamishwa tu hadi kesi ya msingi ipatiwe majibu. Wanasheria vipanga wa chadema kazi mnayo.

3. Kushirikisha Vyombo vya Habari na Mitandao ya Kijamii.
Katika zama hizi za teknolojia, habari zinasambaa kwa haraka mpaka kwenye vitochi. Ikiwa kuna ushahidi wa wazi kuwa uchaguzi hautakuwa wa haki, ni muhimu kuushirikisha umma kupitia vyombo vya habari huru na mitandao ya kijamii. Shinikizo la umma linaweza kulazimisha mamlaka kuchukua hatua haraka kusitisha uchaguzi batili. Petition ni ya sahihi walau milioni 20 ni muhimu- zipelekwe tume, kwa Bunge, Raisi na wahusika, vinginevyo ni kukaribisha machafuko na mauwaji yasiyo ya msingi.

Na kwa mujibu wa Sheria ya Haki ya Kupata Habari ya mwaka 2016 (Access to Information Act), wananchi wana haki ya kupata taarifa kuhusu masuala ya uchaguzi. Vyombo vya habari vinaweza kusaidia kuonyesha kasoro zilizopo kwenye uchaguzi na kutoa majukwaa ya majadiliano ya wazi. Rejea kauli maarufu ya aliyekuwa Jaji Mkuu wa Kenya, David Maraga, wakati wa kufuta uchaguzi wa urais mwaka 2017 ni ya kuigwa:

“Mahakama haiwezi kuruhusu matokeo ya uchaguzi uliojaa ukiukwaji wa sheria, hata kama ni rais aliyechaguliwa. Sheria ni msumeno.”

Hii inasisitiza kuwa hakuna aliye juu ya sheria, na haki lazima itendeke sio hizi Habari za gori la mkono ambalo sasa wahusika wake wanajutia kutoa kaulimkama hizo.

4. Mikakati ya Amani ya Kiraia (Civil Resistance)
Kwa mujibu wa Mkataba wa Afrika kuhusu Demokrasia, Uchaguzi na Utawala Bora (African Charter on Democracy, Elections and Governance), nchi wanachama zimekubali kushughulikia changamoto za uchaguzi usio wa haki kwa kushirikiana na mashirika ya kimataifa. Ibara ya 17(1) ya mkataba huu inasema: “Nchi wanachama zitahakikisha kuwa uchaguzi unafanywa kwa njia huru, ya haki, uwazi, na kwa mujibu wa katiba ya taifa husika.”

Mashirika ya kiraia pia yana nafasi muhimu katika kufuatilia uchaguzi, kutoa elimu kwa wapiga kura, na kushinikiza marekebisho ya sheria, kazi ianze sasa, sio tu kusubiria Chadema ya Tundu Lisu ifanye kazi.

Wananchi wanaweza kutumia njia za amani kama maandamano, migomo, na kampeni za kutotii sheria (civil disobedience) ili kushinikiza kusitishwa kwa uchaguzi usio wa haki. Historia inaonyesha kuwa nguvu ya umma, inapofanywa kwa amani na mshikamano, inaweza kuleta mabadiliko makubwa. Mengine, mtajiongeza wenyewe.

5. Kushirikisha Jumuiya za Kimataifa.

Katika mazingira ambapo taasisi za ndani zimepoteza uaminifu, ni muhimu kuomba msaada kutoka kwa mashirika ya kimataifa kama Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika, au mashirika ya haki za binadamu. Taasisi hizi zinaweza kuweka shinikizo kwa serikali au kutoa uangalizi wa kimataifa ili kuhakikisha haki inatendeka.

6. Kushiriki katika Uchaguzi na Kuhakikisha Mshindi Halali Anatangazwa katika kila kituo cha uchaguzi.
Baada ya uchunguzi wa kutosha, ni muhimu kuhakikisha kuwa mshindi halali ndiye anatangazwa. Hii ni kwa mujibu wa Kanuni za Maadili ya Uchaguzi (Election Ethics Guidelines) zinazotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, ambazo zinasisitiza uadilifu, uwazi, na ukweli katika kutangaza matokeo.

Kauli ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, inasisitiza:

“Uongozi ni dhamana. Ni wajibu, si heshima tu. Na wajibu huo ni wa kusema kweli na kutenda haki.”

Baada ya kuchunguza ushahidi wote, ni muhimu kuhakikisha kuwa mshindi halali wa uchaguzi ndiye anayetangazwa. Hii hujenga imani kwa wananchi na kuimarisha demokrasia. Vyombo vyote vinavyohusika, kuanzia tume ya uchaguzi hadi mahakama, vinapaswa kutenda haki bila upendeleo, hata Nape Mnauye kasema anataka haki na anajutia kauli yake ya gori la mkono.

Mwisho, povu ruksa bila matusi na ukipenda kuongeza njia mbadala ongezea. Nchi ni yetu sote ikiwemo CCM. Ni dhahiri kuwa uchaguzi usiofuata sheria si tu unakiuka haki za wananchi bali pia unahatarisha amani ya taifa. Ni lazima kusimama kidete kutumia katiba, sheria, na taasisi huru kuhakikisha uchaguzi usiofata haki , utakuwa batili ab nitio na unasitishwa, na mshindi halali wa uchaguzi anatangazwa kama utafanyika. Kwa kufanya hivyo, tutalinda msingi wa demokrasia, haki, na utawala bora kwa vizazi vijavyo.

Uchaguzi usiofuata Matakwa ya wananchi, Katiba au sheria ni tishio kwa demokrasia, amani, na maendeleo ya taifa. Ni wajibu wa kila mwananchi kulinda mchakato wa kidemokrasia kwa kuhakikisha kuwa Katiba, haki, Amani, sheria zinafuatwa kikamilifu. Kwa kutumia njia za amani na za kisheria, inawezekana kusitisha uchaguzi haramu na kumrejeshea haki mshindi halali wa kura ya wananchi.
Demokrasia ya kweli hujengwa kwa haki, uwazi, na uwajibikaji. Tuwe walinzi wa haki hiyo.
Yote uliyoongea yalisha acha kufanya kazi Tanzania,mahakama iko mfukoni kwa mhimili uliojitangaza kujichimbia kwa uimara zaidi na yenyewe imekubali au imepandikizwa chawa wa muhimili mkuu na hawajui cha kufanya,Waandishi siotu wapo mfukoni kwa mhimili unaohinadi umejichimbia zaidi,huenda sasa wamewekwa sehemu mbaya zaidi au chafu zaidi,na hata wenyewe kugeuzwa chawa.WAsimamizi wa sheria na amani walishafanywa mazombie hata hawajuitena nini kinaendelea,hata kama sinema walisha poteza series.
 
sasa tufanye nini kama yote hayo ni kweli? Dr slaa alisha wapi kusema twende tu ili kuonesha kwamba haki haipo. kusimamisha uchaguzi inawezekana ni CDM na wanasheria wake kujipanga hata sasa...
 
Reforms zozote ambazo zinahitaji kupambaniwa kwa jasho na damu zinahitaji wakereketwa kwa nature ya siasa zetu wakereketwa wa mambo za kisiasa ni wachache kulinganisha na masuala mengine ya kijamii

Kwa Tanzania hii hakuna mwananchi wa kawaida atakae kuwa tayari kujeruhiwa na hata kufa kwa maswala ya kisiasa. Yani mtu afe kisa eti mbunge aingie madarakani kwa mwananchi wa kawaida hilo ni suala gumu kwanza hata mifumo ya uchaguzi ikiwa sawa lazima itumike nguvu kubwa kumshawishi mtu huyo akapige kura je kupigania huo mfumo inakuaje?

Hoja yangu hapa ni kuwa, kupitia matatizo ya kijamii kama vile suala la wafanyabiashara wa kariakoo kipindi kile, tozo za miamala wakati ule na matatizo mengine mtambuka yanayoanzishwa na serikali ambayo huwagusa wananchi wa kawaida moja kwa moja ndio yanaweza kuwa chachu rahisi katika kupigania reforms mbalimbali na sio za kisiasa tu kama kipindi hiki cha uchaguzi
Kama hakuna aliye tayari kufa, ndio maama cdm wanasema hawako tayari kushiriki chaguzi zinazowaacha na majeruhi ama kifo. Wanataka mambo haya yafanyiwe kazi, ndio maana ya NRNE.
 
sasa tufanye nini kama yote hayo ni kweli? Dr slaa alisha wapi kusema twende tu ili kuonesha kwamba haki haipo. kusimamisha uchaguzi inawezekana ni CDM na wanasheria wake kujipanga hata sasa...
Nguvu ya umma,nguvu ya waliojitambua,weledi wa kimataifa na sheria za kimataifa zakwetu ni mwendo wa kufinywngwa mwanzo mwisho kwa msaada wa chawa pandikizi na hisani ya wanasii hasa.
 
Kama hakuna aliye tayari kufa, ndio maama cdm wanasema hawako tayari kushiriki chaguzi zinazowaacha na majeruhi ama kifo. Wanataka mambo haya yafanyiwe kazi, ndio maana ya NRNE.
Chadema hawajasema wanasusia uchaguzi kuwa hawashiriki ila wanataka kuzuia uchaguzi kupitia nguvu ya umma ili usifanyike kwa maana wanataka kuhamasisha maandamano ya kupinga uchaguzi kwa watakaojitokeza kufanya uchaguzi na njia nyingine za nguvu na jasho

Swali ni je mwananchi gani wa kawaida atajitokeza kuzuia watakaojitokeza kupiga kura zaidi ya wanachadema wenyewe? Je watatosha kuwashinda watawala pamoja na dola?

Bila mwananchi wa kawaida kwa umoja wao kuhusika wanasiasa pekeyao hawawezi kuleta mageuzi amini nakwambia
 
Ndio maana wanapita kwenye hiyo operation kutaka nguvu ya umma.
 
Ndio maana wanapita kwenye hiyo operation kutaka nguvu ya umma.
Ndio nikakwambia hiyo nguvu ya umma hawawezi ipata kwa maswala ya kisiasa hasa kipindi hiki cha uchaguzi

Walitakiwa wapenyeze ajenda wakati wa matatizo mengine ya kijamii yanayowagusa wananchi moja kwa moja na mifano nimekupa

Yani mwananchi akikereketwa hasa na akapata kiongozi wa kumsaidia kupambana ilo jambo linakuwa rahisi kuliko mwanasiasa kukererketwa halafu apite kuomba kuungwa mkono na mwananchi wa kawaida

Nakuambia watachoma mafuta na siku ya uchaguzi wananchi watakuwa kama wamemwagiwa maji
 
Kutoa Malalamiko Rasmi Kupitia Tume Huru ya Uchaguzi. Tume lazima itoe majibu kabla ya uchaguzi kwamba itafuata miongozo iliyowekwa na mshindi halali kutangazwa.
Kesi zote zilizofunguliwa dhidi ya Tume ma serikali wananchi walishinda. Mpaka wakahamia Mahakama ya Afrika wakashinda pia.

Ni kwa sababu tu wadhulmaji hawataki
 
Ndio nikakwambia hiyo nguvu ya umma hawawezi ipata kwa maswala ya kisiasa hasa kipindi hiki cha uchaguzi

Walitakiwa wapenyeze ajenda wakati wa matatizo mengine ya kijamii yanayowagusa wananchi moja kwa moja na mifano nimekupa

Yani mwananchi akikereketwa hasa na akapata kiongozi wa kumsaidia kupambana ilo jambo linakuwa rahisi kuliko mwanasiasa kukererketwa halafu apite kuomba kuungwa mkono na mwananchi wa kawaida

Nakuambia watachoma mafuta na siku ya uchaguzi wananchi watakuwa kama wamemwagiwa maji
Tulia hivyo hivyo acha kutetemeka
 
Mwananchi wa kawaida ndio anaweza kupigania reforms chadema walitakiwa kuongoza katika matatizo ya kijamii sio kisiasa hawataungwa mkono na mwananchi wa kawaida
Acha kubadili falsafa usioijua. Chadema we are heading in every aspect na watanzania wanatuunga mkono. We endelea kulala usingizi wa pono
 
Haki inaambatana na wajibu gentleman,
ndio maana nashauri vijana na waTanzania wote kujitokeza kwa mamilioni yao kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu huru, wa haki na wa wazi utakao fanyika kwa amani sana october mwaka huu, maana hiyo ni miongoni mwa haki ya kikatiba ya kila mTanzania mwenye sifa ya kupiga kura.

kinyume na hapo ni ushirikina na kujidhulumu wenyewe :NoGodNo:
Mbona mnakuwa wagumu kuelewa. No Reforms No Election sasa nashindwa kuelewa uchaguzi upi unaongelea.
 
Acha kubadili falsafa usioijua. Chadema we are heading in every aspect na watanzania wanatuunga mkono. We endelea kulala usingizi wa pono
Sijabadili chochote hapo nimetoa maoni yangu kama mtanzania na wala Sina cha kutetemekea hapo ngoja tusubiri mwezi wa kumi sio mbali na wengine kwenye Chadema washaanza kuona kuwa huu mzigo watakuwa pekeyao bila hao wananchi ambao mnatarajia waje washaanza kugive up
 
Mbona mnakuwa wagumu kuelewa. No Reforms No Election sasa nashindwa kuelewa uchaguzi upi unaongelea.
pole gentleman kwa kushindwa kuelewa,

hivi kwa mtazamo wako huru,
no reform no elections inalenga kuikomoa chadema au wanachama wake? :NoGodNo:
 
Ndio nikakwambia hiyo nguvu ya umma hawawezi ipata kwa maswala ya kisiasa hasa kipindi hiki cha uchaguzi

Walitakiwa wapenyeze ajenda wakati wa matatizo mengine ya kijamii yanayowagusa wananchi moja kwa moja na mifano nimekupa

Yani mwananchi akikereketwa hasa na akapata kiongozi wa kumsaidia kupambana ilo jambo linakuwa rahisi kuliko mwanasiasa kukererketwa halafu apite kuomba kuungwa mkono na mwananchi wa kawaida

Nakuambia watachoma mafuta na siku ya uchaguzi wananchi watakuwa kama wamemwagiwa maji
Ikitokea kweye matatizo ya kijamii hao wanasiasa wa upinzani wakajiingiza ujue hilo tatizo halitapata utatuzi, maana itaonekana ni kutumiwa kisiassa. Ukweli huu huujui?

Hata wananchi wasipojitokeza kuandamana kwa ajili ya uoga, haimaanishi madai ya cdm si ya msingi, ama wanakubaliana na hizo chaguzi za kihuni. Isitoshe cdm watakuwa wametekeleza wajibu wao, kuliko kukaa kimya uhuni ukifanyika.
 
Sijabadili chochote hapo nimetoa maoni yangu kama mtanzania na wala Sina cha kutetemekea hapo ngoja tusubiri mwezi wa kumi sio mbali na wengine kwenye Chadema washaanza kuona kuwa huu mzigo watakuwa pekeyao bila hao wananchi ambao mnatarajia waje washaanza kugive up
Hayo mapandikizi yasikupotezee mudao. Mungu ni Mwema hatukua tunawajua.
 
Ikitokea kweye matatizo ya kijamii hao wanasiasa wa upinzani wakajiingiza ujue hilo tatizo halitapata utatuzi, maana itaonekana ni kutumiwa kisiassa. Ukweli huu huujui?

Hata wananchi wasipojitokeza kuandamana kwa ajili ya uoga, haimaanishi madai ya cdm si ya msingi, ama wanakubaliana na hizo chaguzi za kihuni. Isitoshe cdm watakuwa wametekeleza wajibu wao, kuliko kukaa kimya uhuni ukifanyika.
Hata wasipoingilia pia matatizo huwa hayatatuliwi kwani tozo mpaka sasa hazipo? Yale ya wafanyabiashara kariakoo hayapo?

Inshu ni kupata muungano na wananchi ili kupigania reforms na sio kutatua matatizo hii serikali toka lini ikatatua matatizo ya wananchi zaidi ya kuwapumbaza akili
 
Back
Top Bottom