Jinsi ya kutoka nje ya mwili (Astral Projection)

Namba 2,
Kisha mimi napata faida gani wao wakiangamia?
Huwa mnafikiri mnavyoviandika au unaandika kutegemeana na akili imekwambia nini siku husika?

Rakims
 
Nyie ndio hufanya watu kuziona dini ni ngumu na kusababisha watu kutokujua mambo kwa vitisho na uelewa wenu finyu.
Na unapopewa hoja huzalisha hoja nyingine ili ukimbie hoja husika na kuigiza mwenye hekima hali hekima yenyewe huna

Rakims
 
Unatakiwa kusoma na kujifunza zaidi mkuu si kila anaesoma au aliyesoma teyari ni mwalimu hivyo usiunganishe mambo kwa kuchanganya changanya na itikadi fulani kisha ukatoa quote ambazo baadae kwa watu wenye uelewa wataona huyu kaongea nini!?

Si kila mtu anaetoka nje ya mwili hutoka nje ya mwili anavyodai wengine huishia ndotoni na kujihisi wametoka nje ya mwili
Nachotaka kufahamu ni jambo moja ili niendelee kujibu maswali yako.

Je, ulishawahi kutoka nje ya mwili?
Tuanzie hapo kisha nitakuuliza maswali kuthibitisha kama kweli umeshawahi kutoka au laa.

Maana nimeshajaribu kuelewesha watu wamekuja na hoja zao za kutoka nje ya mwili hali ya kuwa ni vitu wanavisualize na kuimagine sasa tutaendelea mjadala kama tu umewahi kutoka nje ya mwili zaidi ya hapo siwezi kubishana na mtu asiyejua kitu anachobishania

Rakims
 
Mchango wako ni mzuri hapa mkuu lakini kadri siku zinavyokwenda ndio nazidi kuelewa uelewa wa kila mtu kuhusu haya mambo,

Watu wa mwanzo kuyafanya haya si kikundi cha Rosae Crusis kama ulivyokuwa Brain washed na Google ama wazungu mtu wa kwanza kuyafanya haya alikuwa ni mtu wa kwanza kuitembelea dunia kwa mara ya kwanza na elimu hiyo alikuwa nayo kabla ya kufika hata duniani,
Rejea katika vitabu vyote vya dini na historia vitakutajia mtu huyo jina lake na elimu alizokuwa nazo.

Katika watu wote ambao nilikuwa naamini kwa kiasi kidogo sana wanaweza kuwa enlightened na haya mambo ni wewe mkuu kumbe pia bado unahitaji kujifunza zaidi na kuacha kuamini kuwa kila elimu ipo under secret society.
Ni ujinga kuamini kila kitu kimeanzishwa na watu weupe au vyama vya siri

Swali lako pia;
Je, ulishawahi kutoka nje ya mwili?

Karibu tujadili,

Rakims
 
Huku ndio watu wenye uelewa mpana kidogo huita kufikiria nje ya boksi,

Asilimia 90 ya watu waliotoka nje ya mwili hawapendi watu ambao bado hawajaweza au kujua kuhusu Oobe waweze kujua na kutoka nje ya mwili wengi huchukua experience za kushtusha kisha kuanza kuzishikia mabango ili siku ujijaribu ukizifikia ujue sasa hiki ndio kile kipengele. Nilikuwa naambiwa naondoka nimefika kisha unarudi na kuamua kuachana nayo.

Kila mtu hupenda kuwazidi wengine pia kuwatawala maana yoyote mwenye elimu ya kitawala si rahisi kufundisha watu wengine kwa kuogopa kutawaliwa nao.

Si kila mtu mwenye maarifa anaweza kuyatumia kwa faida ya watu wengine,
Hivyo kabla hujaaminishwa vitu basi inakubidi uvijue na uvielewe tupo karne ya 21 na Mungu kaumba dunia ambayo inakwenda na wakati jini alivyopanga na anavyotaka yeye sasa kuna watu wanalazimisha watu wabaki karne ya 15 ili wazidi kuwaona wao ni Miungu watu hali ya kuwa teyari hao watu wameshapata ufunuo wa karne ya 22 hapo ndio nguvu ya mabavu huingia na kuleta majanga.
Watu wanahisi kutoka nje ya mwili humfanya mtu awe mbali na Mungu kwa uelewa wao finyu.
Hali ya kuwa kutoka nje ya mwili kutakufanya uzidi kuwa karibu na Mungu wa kweli
"ambaye ni Mungu mmoja tu, yeye tu ambaye anafaa kuabudiwa na anaestahiki,
Yeye tu ambaye hana mshirika na ni vyake vilivyomo ardhini na mbinguni yeye ambaye anamiliki kiti cha enzi yeye tu ambaye hata kama vya mbinguni na ardhini vikikusanyika vyote na na kwenda anavyotaka au kinyume nae havimpunguzii wala havimuongezei,
Yeye ambaye alikuwa na atabaki kuwa Mungu".

Sasa watu wengi hawapendi watu kuijua kweli na kuachana kuwa tegemezi kwa watu ndio maana utaona wanapiga sana vita anapotokea mtu kuwafungua watu akili.

Chunguza humu Jf mimi ndio member wa kwanza kuleta hii makala na imefungua wengi na kusaidia wengi kujifahamu Sasa watu kama Pascal na John wakishaona una lengo na kusaidia watu kujitambua wanaamini kabisa utawakosesha watu wanaoamini ujinga waliowaaminisha kabla

Rakims
 
Mkuu ningependa kuongeza maarifa kidogo juu ya mtu huyu unaweza kunitumia link au jina la kitabu nikasome niongeze uelewa?
 
Especially hapo kwenye mtu wa kwanza kunitembelea dunia na elimu aliyokuwa nayo kabla ya kufika duniani
 
Mkuu Rakims , hebu twende mdogo mdogo, bandiko lako hili ni la

Jinsi ya kutoka nje ya mwili (Astral Projection)​

 
Swali lako pia;
Je, ulishawahi kutoka nje ya mwili?

Karibu tujadili,

Rakims
Sijawahi kutoka nje ya mwili, ila nakiri, sijafanya efforts zozote kutaka kutoka nje ya mwili kwasababu kwa mujibu wa imani ya dini yangu, kutoka nje ya mwili ni ushetani!.

Na kwa members wengine humu msio jua, ukisikia wanga, ndio hawa wanaotoka nje ya mwili, na wanga hutoka kwa ajili ya kucheza tuu na kuwachezea watu, kuwawangia, ila ukizoea, unageuka mchawi, sasa sio tena kuwawangia watu bali kuwaloga, na kwenda kwenye zile karamu zao za kula maiti makaburini, na ukiwa ni mmoja wao, kupaleka chakula mezani ni zamu kwa zamu, hivyo ikifika zamu yako, ni lazima upeleke chakula mezani kwa kumtoa mpendwa, wako, watu wa kutolewa wakiisha, inakuwa zamu yako, na hapo ndio huwa mwisho wao!.
P
 
Leta ushahidi sehemu ambayo wameandika ni ushetani....EVIDENCE
 
Kama kutoka nje ya mwili ni ushetani basi moja kwa moja unamaanisha hata Mungu naye ni shetani. Kwasababu, tunaamini binadamu akishakufa roho hutengana na mwili kwajinsi mwenyezi Mungu alivyoamua iwe hivyo. je utengano huu siyo uchawi?
 
Nilichogundua binadamu tunapenda sana kuita ni dhambi au ushetani ambavyo hatuvijui......nimeshangaa kijana mmoja anasema michezo yote kama vile mpira basketball n.k ni dhambi, kumeditate ni dhabi,yoga ni dhambi nikasema basi motoni tutakuwa wengi
 
Watu wakiwa usingizini usiku huwa wanatoka nje ya mwili bila kujijua. Sasa kama ni dhambi basi watu wote duniani tutaenda motoni.
 
Kwa fikra zako hizi,bado sana mkuu.
Ww unafikra gani? Umeassume wote tuliokuwa humu ni wakristo au..at least sisi tuliambiwa itafute elimu popote ili..hapo huja consider waaio na dini...fikiria kabla ya kutenda
 
Mkuu John7371, Luciferi ni very tricky when deceiving kutafuta wafuasi, kuna wakati anaji disguise as God na kufanya hata miujiza ili watu wajue ni Mungu !. Hiki kinachofundishwa hapa ni ushetani mtupu, kuna watu wanafuata tuu kama mazuzu. Mimi ndiye mchangiaji wa 4 wa bandiko hili na niliwapa angalizo muhimu kabisa, but its very unfortunately, wanaomkubali na kumfuata shetani ni wengi kuliko wanaomfuata Mungu. Njia ya kwenda mbinguni ni nyembamba, ya kwenda motoni ni nene!.

Haya mambo hata Uislamu hauyakubali yanaitwa shirki, ni dhambi !.
P
 
Ww unafikra gani? Umeassume wote tuliokuwa humu ni wakristo au..at least sisi tuliambiwa itafute elimu popote ili..hapo huja consider waaio na dini...fikiria kabla ya kutenda
Kila mtu anakuwa defined na jinsi au namna anavyojenga hoja zake-Wakati mwingine mtu au watu huamua kukaa kimya kutokujibu jambo au mtu kutokana na ufinyu wa hoja zake.Safari ipo 🤣 🤣 🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…