NGOJA NITOE USHUHUDA WANGU LEO.
Haya mambo ya astra projection niliyafaham kipindi nipo chuo mwaka wa pili nilikuwa napenda sana kusoma mambo ya power of positive thinking na ability of brain kwa ujumla ndo siku moja nikajikuta nimeopen link iliyonifikisha kwenye AP.
Hii mada nilitokea kuipenda sana na nikashawishika kuendelea kuisoma zaid na zaid kwenye web mbalmbal huku nikipractice, ilinichukua kama wiki tatu hivi hadi kufanikisha, nakumbuka siku ya kwanza kutoka nje ya mwili wangu nilikuwa hostel nimelala usiku, siku hiyo nilifanikiwa kuamka na kushuka juu ya dabo deka mpaka chini nilivyogeuka kuangalia juu ya kitanda nilishituka sana kuuona mwili wangu ukiwa umelala pale juu ya kitanda nikaanza kulia sababu niliona kama nimekufa hivi lakn machoz yalikuwa hayatok nikaamua kupanda tena juu ya kitanda na kumwamsha jamaa niliyekuwa nalala naye (c unajua hostel bongo nikubebana) lakin kila nikimgusa nakuwa kama simkamat hivi ,yan mwili wangu nauona kama mwili ila unakuwa kama ni hewa hivi. nikaamua kuanza kupiga kelele za kuomba msaada kwa mayowe lakn kat ya watu saba waliokuwepo chumban hakuna hata moja aliyeshituka, nikaamua kutoka nje cha ajabu wakat nashika kitasa ili nifungue mlango kilikuwa hakikamatik nakuona kama mkono umeshatoka nje, nilivojisogeza karbu mlangon nikajikuta nishatokea nje hii nayo ilinishangaza sana ghafla kuna mtu alikuwa anatokea upande wa choon nikawa namuita ila ikawa km haniskii hiv nikaamua kumfata na kumgusa kwa nyuma ila ckuweza maana mwili wangu ulikuwa kama hewa tu, nikaamua kumzunguka na kusimama mbele yake ili anione lakn akanipita, nikaona isiwe shida nikasimama tena mbele yake huku nimetanua miguu na mikono ili kumzuia asipite maana ilikuwa koridon, lakini alipita katkat yangu bila pingamiz lolote.. hapo ndo nikaijiwa na mawazo kuwa mm ndo nshakufa hivo na tena nikikumbuka na story nilizowah kusikia kuwa marehem mnavyoenda kumzika huwa anaona na kusikia kila kitu ndo nikaamin moja kwa moja kumbe ndo anakuwa katika hali hii????? nikajua ndo maana wote niliowaita kumbe hawawez kuniona wala kusikia, lkn kuna wazo likaja kichwan kuwa mbona dunian wanasema israel ndo humtoa mtu uhai wake na mbona mm mpaka mda huu sijamuona israel mtoa roho akija??? mda wote nawaza hayo nimesimama katkat ya korido na watu wanaoenda au kutoka toilet wananipita tu, hakuna hata mmoja aliyeonyeshaa hata dalili kama ananiona. likaja wazo la kuwa nikiendelea kukaa hapa nje israel atanikuta na kunichukua hivo niliamua kurud had chumbani likaja wazo kuwa inawezekana ikawa sijfa kwa sabab had kufikia hali ile natambua nilichofanya, nikaona ngoja km nilivotoka niingie tena lkn cha ajab ni kuwa bado nikaona mwili wangu na huo mwingne ni tofaut kabsa wala hauendan kila nikijarbu kuinua mguu naoona unaamka ule ule mfano wa hewa lkn ule halis umekataa, kila nikijitingisha nothing. nikajikuta nipo kwenye deep feelings kwa mbal sana nikawa kama nasikia saut za watu zikipita kwenye korido nikawa najitingisha tingisha mara nikaona nimefumbua macho lakn nikajua tu bado nitakuwa kwenye hali ile ile tu ila nikajisemea hebu nijaribu kuinua mkono nikaona unananyuka kujaribu kuinua mguu nao unanyanyuka nikasema inaweza kuwa ni wenge tu kama mara ya kwanza nikaona nishuke tena chini ya dabo deka nakuangalia tena juu ya kitanda lakin sikuuona ule mwili kama mara ya kwanza nilivouona nikaamua nitoke nje kama mara kwanza ya kupenya mlagoni ila nilijigonga mlangon ndo nikagundua utofaut wa mwanzo na sasa maana mwanzo nilikuwa mwepes sana kama upepo hivi, aseee sikuamin ikibid nitoe Embassy mbili na kwenda kukaa nje na kujiuliza ivi nilichokifanya ni ndoto au ilikuwa kweli uku nikila pafu kadha wa kadha nikichek saa mida ya saa kumi na moja kasoro asubuh na nikivuta picha la hilo tukio haikuzid hata saa moja hivi.
Ikanibid kuingia kwenye wikpedia na kuuliza swali kwa kile nilcho experience nikaja kujua kumbe ni kitu cha kawaida tu ila sema ule wote ulikuwa uoga wangu tu.
ikabid siku nyingne nijaribu tena na ile hali nilivoiona sikuogopa tena.. hapo nikaanza kupiga misele ya mitaa kwa mitaa ila cha ajabu nilichoona ni kuwa kwa mfano ukafikiria niende sehem flan nilijikuta nishafika hapo nilipotaka mda huo huo. kuna kipindi niliwaza kumuona mtu fulan ambaye alishakufa mda tu ila cha ajabu nikuwa nikionana nae tunaongea fresh ila ajabu huwa najikuta kwenye hali ya kama nimelewa hivi na kushindwa kuendelea na story na hata nikrud kwenye mwili wangu nakumbuka kuwa nimeonana na mtu fulan tukakaa na kuongea ila nakuwa sikumbuki tuliongea nini? nishajarribu mara nyingne tena kuonana nae ila hali ya kuwa tunaongea nakuwa kama nimelewa hivi hutokea tena na kushindwa kuendelea na mazungumzo...#mpaka hapo kwa atakaye amin poa na asiye amin poa na ndio maana kuna waislam,wakristu,budha,pagan n.k ili kuthibitisha kuwa sio lazma binadam wote tuamin kitu kimoja#
Ila nilikuwa naomba msaada kwa yeyote mwenye experience ya kutoka nje ya dunia . kuelekea sayar nyngne mfano mars,Jupiter n.k anisaidie ..
»»»na ndio maana naamin ukweli ndio humweka mtu huru... ukimjua Mungu lazma utampenda na ukimjua shetan lazma utamshinda...usipojua hivi basi jiandae kuwa mfungwaHURU.
Ahsante sanA.