Shing Yui
JF-Expert Member
- Aug 8, 2015
- 15,168
- 38,049
hivi inawezekana kutoka nje ya mwili na kutembelea sayar kama mars,Jupiter,Pluto n.k
Umeweza hatua za mwanzo kwanza?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
hivi inawezekana kutoka nje ya mwili na kutembelea sayar kama mars,Jupiter,Pluto n.k
Umeweza hatua za mwanzo kwanza?
NGOJA NITOE USHUHUDA WANGU LEO.
Haya mambo ya astra projection niliyafaham kipindi nipo chuo mwaka wa pili nilikuwa napenda sana kusoma mambo ya power of positive thinking na ability of brain kwa ujumla ndo siku moja nikajikuta nimeopen link iliyonifikisha kwenye AP.
Hii mada nilitokea kuipenda sana na nikashawishika kuendelea kuisoma zaid na zaid kwenye web mbalmbal huku nikipractice, ilinichukua kama wiki tatu hivi hadi kufanikisha, nakumbuka siku ya kwanza kutoka nje ya mwili wangu nilikuwa hostel nimelala usiku, siku hiyo nilifanikiwa kuamka na kushuka juu ya dabo deka mpaka chini nilivyogeuka kuangalia juu ya kitanda nilishituka sana kuuona mwili wangu ukiwa umelala pale juu ya kitanda nikaanza kulia sababu niliona kama nimekufa hivi lakn machoz yalikuwa hayatok nikaamua kupanda tena juu ya kitanda na kumwamsha jamaa niliyekuwa nalala naye (c unajua hostel bongo nikubebana) lakin kila nikimgusa nakuwa kama simkamat hivi ,yan mwili wangu nauona kama mwili ila unakuwa kama ni hewa hivi. nikaamua kuanza kupiga kelele za kuomba msaada kwa mayowe lakn kat ya watu saba waliokuwepo chumban hakuna hata moja aliyeshituka, nikaamua kutoka nje cha ajabu wakat nashika kitasa ili nifungue mlango kilikuwa hakikamatik nakuona kama mkono umeshatoka nje, nilivojisogeza karbu mlangon nikajikuta nishatokea nje hii nayo ilinishangaza sana ghafla kuna mtu alikuwa anatokea upande wa choon nikawa namuita ila ikawa km haniskii hiv nikaamua kumfata na kumgusa kwa nyuma ila ckuweza maana mwili wangu ulikuwa kama hewa tu, nikaamua kumzunguka na kusimama mbele yake ili anione lakn akanipita, nikaona isiwe shida nikasimama tena mbele yake huku nimetanua miguu na mikono ili kumzuia asipite maana ilikuwa koridon, lakini alipita katkat yangu bila pingamiz lolote.. hapo ndo nikaijiwa na mawazo kuwa mm ndo nshakufa hivo na tena nikikumbuka na story nilizowah kusikia kuwa marehem mnavyoenda kumzika huwa anaona na kusikia kila kitu ndo nikaamin moja kwa moja kumbe ndo anakuwa katika hali hii????? nikajua ndo maana wote niliowaita kumbe hawawez kuniona wala kusikia, lkn kuna wazo likaja kichwan kuwa mbona dunian wanasema israel ndo humtoa mtu uhai wake na mbona mm mpaka mda huu sijamuona israel mtoa roho akija??? mda wote nawaza hayo nimesimama katkat ya korido na watu wanaoenda au kutoka toilet wananipita tu, hakuna hata mmoja aliyeonyeshaa hata dalili kama ananiona. likaja wazo la kuwa nikiendelea kukaa hapa nje israel atanikuta na kunichukua hivo niliamua kurud had chumbani likaja wazo kuwa inawezekana ikawa sijfa kwa sabab had kufikia hali ile natambua nilichofanya, nikaona ngoja km nilivotoka niingie tena lkn cha ajab ni kuwa bado nikaona mwili wangu na huo mwingne ni tofaut kabsa wala hauendan kila nikijarbu kuinua mguu naoona unaamka ule ule mfano wa hewa lkn ule halis umekataa, kila nikijitingisha nothing. nikajikuta nipo kwenye deep feelings kwa mbal sana nikawa kama nasikia saut za watu zikipita kwenye korido nikawa najitingisha tingisha mara nikaona nimefumbua macho lakn nikajua tu bado nitakuwa kwenye hali ile ile tu ila nikajisemea hebu nijaribu kuinua mkono nikaona unananyuka kujaribu kuinua mguu nao unanyanyuka nikasema inaweza kuwa ni wenge tu kama mara ya kwanza nikaona nishuke tena chini ya dabo deka nakuangalia tena juu ya kitanda lakin sikuuona ule mwili kama mara ya kwanza nilivouona nikaamua nitoke nje kama mara kwanza ya kupenya mlagoni ila nilijigonga mlangon ndo nikagundua utofaut wa mwanzo na sasa maana mwanzo nilikuwa mwepes sana kama upepo hivi, aseee sikuamin ikibid nitoe Embassy mbili na kwenda kukaa nje na kujiuliza ivi nilichokifanya ni ndoto au ilikuwa kweli uku nikila pafu kadha wa kadha nikichek saa mida ya saa kumi na moja kasoro asubuh na nikivuta picha la hilo tukio haikuzid hata saa moja hivi.
Ikanibid kuingia kwenye wikpedia na kuuliza swali kwa kile nilcho experience nikaja kujua kumbe ni kitu cha kawaida tu ila sema ule wote ulikuwa uoga wangu tu.
ikabid siku nyingne nijaribu tena na ile hali nilivoiona sikuogopa tena.. hapo nikaanza kupiga misele ya mitaa kwa mitaa ila cha ajabu nilichoona ni kuwa kwa mfano ukafikiria niende sehem flan nilijikuta nishafika hapo nilipotaka mda huo huo. kuna kipindi niliwaza kumuona mtu fulan ambaye alishakufa mda tu ila cha ajabu nikuwa nikionana nae tunaongea fresh ila ajabu huwa najikuta kwenye hali ya kama nimelewa hivi na kushindwa kuendelea na story na hata nikrud kwenye mwili wangu nakumbuka kuwa nimeonana na mtu fulan tukakaa na kuongea ila nakuwa sikumbuki tuliongea nini? nishajarribu mara nyingne tena kuonana nae ila hali ya kuwa tunaongea nakuwa kama nimelewa hivi hutokea tena na kushindwa kuendelea na mazungumzo...#mpaka hapo kwa atakaye amin poa na asiye amin poa na ndio maana kuna waislam,wakristu,budha,pagan n.k ili kuthibitisha kuwa sio lazma binadam wote tuamin kitu kimoja#
Ila nilikuwa naomba msaada kwa yeyote mwenye experience ya kutoka nje ya dunia . kuelekea sayar nyngne mfano mars,Jupiter n.k anisaidie ..
»»»na ndio maana naamin ukweli ndio humweka mtu huru... ukimjua Mungu lazma utampenda na ukimjua shetan lazma utamshinda...usipojua hivi basi jiandae kuwa mfungwaHURU.
Ahsante sanA.
Unazidi kunitamanisha!
Mimi nilijaribu nikafikia stage ambayo nilihisi mwili ni wa baridi alafu nikashindwa kufanya chochote zaidi ya akili kufanya kazi,
Yaani hata mkono ulikuwa haunyanyuki.
Ilikuwa mchana nimefunga mlango wa geto fresh, madirisha na taa nikazima.
Lakini ule muda ambao nilikwama kwa kushindwa hata kugeuza shingo, nikasikia mtu anatembea mule ndani kwa sauti kubwa kama vile amevaa ndala
Nikitaka kujigeuza ili nmuone nashindwa.
Nilikaa kwenye ile hali kama dakika 7 hivi ndio nikaweza kukurupuka
Bennie 369 hongera sana we uko hatua za juu, leo usiku lala mapema kisha jaribu kwenda mars ukiona kuna tatizo basi geuza.
Kinachokuunganisha mwili wako unaouacha na huu mpya ni silver cord.
Mi pia sikuwahi kuamini kuwa mtu anaweza kufa kama mwili wake wa zamani utaguswa, kwasababu najua hata likitokea janga lolote lile lazima silver cord itakurudisha
Unazidi kunitamanisha!
Mimi nilijaribu nikafikia stage ambayo nilihisi mwili ni wa baridi alafu nikashindwa kufanya chochote zaidi ya akili kufanya kazi,
Yaani hata mkono ulikuwa haunyanyuki.
Ilikuwa mchana nimefunga mlango wa geto fresh, madirisha na taa nikazima.
Lakini ule muda ambao nilikwama kwa kushindwa hata kugeuza shingo, nikasikia mtu anatembea mule ndani kwa sauti kubwa kama vile amevaa ndala
Nikitaka kujigeuza ili nmuone nashindwa.
Nilikaa kwenye ile hali kama dakika 7 hivi ndio nikaweza kukurupuka
Ulikuwa peke yako? Sa huyo aliyekuwa anatembea ni nani?
Mi pia huwa nafika hiyo hatua, lakini mimi sijawahi kuhisi mtu anatembea, ila nilikuwa nikihisi kama mwili wangu hauna ushirikiano wenyewe kwa wenyewe, huwa naogopa na kudhani kuwa nataka kukata roho hivyo najilazimisha kuamka.
Cc Bennie 369 & aretasludovick
Ni kweli. Mfano ukitaka kunyanyua mkono au mguu au kugeuka huwezi, mara ya mwisho nilipofumbua macho nikawa nimeduwaa tu.
Baada ya sekunde chache za kuduwaa pale chumbani ndio nikaweza kukurupuka.
Kilichonishangaza sikumuona aliyekuwa anatembea mule ndani
Mi nahisi ni uoga tu ulikuzidi, mi nataka nirudie nirudie wiki ijayo mpaka nifanikiwe kutoka. Acha wikiendi ipite kwanza
Hahahaa! Nilivyo na hamu na hii makitu siwezi subiri wikiend.
Uoga ulinikumba ndio maana nilipokurupuka nilifungua mlango na kuwahi nje
Mi pia huwa nafika hiyo hatua, lakini mimi sijawahi kuhisi mtu anatembea, ila nilikuwa nikihisi kama mwili wangu hauna ushirikiano wenyewe kwa wenyewe, huwa naogopa na kudhani kuwa nataka kukata roho hivyo najilazimisha kuamka.
Cc Bennie 369 & aretasludovick
sio wewe tu. wengi wao hata mimi wakat naanza hiyo hali ilikuwa inanitokea ila ukiogopa tu utajikuta usharud kwenye physical body. then inabid uanze tena hivo we jikaze tu na vyote utakavyohis au kuona ujue ni hali ya kawaida ambayo huwapata weng tu. cha msingi ni focus na hali kama hizo ukuona usiogope chukulia km unachofanya unakijua... we endelea zenyewe tu zitakata...fanya jaribio mara kwa mara utajikuta unafanikiwa