Norshad
JF-Expert Member
- Jun 3, 2013
- 5,211
- 12,538
Mi hata sielewi sasa huko unapoenda unapaonaje, kwa mfano tuu, mm nataka kwrnda America, c ndio, ila mimi siijui America kabisa, zaidi ya kuiona ktk media, sasa si naweza kufika nchi nyingine alaf nikahisi nipo tayar America? Kingine mm naweza kutoka ktk mwili wangu, ila nikiona nimeucha tuu asee huwa nahisi nishakufa na najitahidi sana niamke, sasa shida nyingine niliyonayo mimi huwa hii hali yanitokea bila kujiandaa kama nilivyosoma awali, pili mm hunitokea nnapolala mchana, yaani karibia wakat wote ni mchana, pia kuna tukio flani hivi niliwahi cjui ndio kuota au kutoka ktk mwili/ mtanisamehe bure kama nakosea, ila na mm nahitaji kufaham na nnaamin hapa majibu yapo, niliwahi ota ama toka, wakati huo nilikuwa mwananyamala dar/ nilipotoka/ ota nikajiona nipo Iringa natembeatembea mitaa ya miyomboni, lakini ghafla nikaona kama kuna dada ana asili ya kihindi yupo upande wa pili wa barabara anamuita kijana mmoja ambaye yupo upande niluosimama mimi, anamwita mfano wa kumwita mtu kwa ishara bila ya sauti, kishawakati yule kijana anaenda kulikuwa na basi linakuja kwa kasi, yale mabasi ya kizamani leyland, likamgonga yule kijana, ajabu nikamuona yule dada muhindi anafurahia kisha akaanza kunywa damu ya yule kijana, hapo nikajigundua kuwa naota, ila wakati najilazimisha kuamka, nikaamka na kuuona mwili wangu ukiwa umelala na mimi nimeusimamia kwa pembeni, wakati nashangaa, akaja yule dada mwarabu/ muhindi niliyomuona kule iringa, akaniambia kwamba mbona umenikimbia kule, sikia umejua mimi ni nani na umejua kama ile ajar nimeisababisha sasa unayaona yale maji, mle chumbani kulikuwa na beseni huwa tunaifadhia vyombo ama maji, na wakati naenda kupumzika ile saa nne asubui kulikiwa na maji, akaniambia unaonabile damu ktk beseni? Nikamjibu yale ni maji, akasema angalia vizur, nikaangalia nikaona yanabadilika kuwa dam nikaona huu sasa msala, nikaanza jilazimisha niamke huku yeye akiuliza unataka kwenda wapi? Akaanza nikaba, kwa kweli nilifurukuta hata nipoamka niliamka kama mwehu hivi, nikajigusa shingoni nikiwa na alama za kucha, sasa hapa sijajua nilikuwa nakabwa kweli au nilikuwa najikaba mwenyewe